STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, February 1, 2013

EPL kuendelea kesho, Jumapili ni vita ya Man City dhidi ya Liverpool

KITATANGE cha Ligi Kuu ya England kinatarajiwa kuendelea kesho kwa mechi kadhaa za ligi hiyo, lakini macho ya mashabiki yakielekezwa kwenye pambano la Jumapili kati ya Mabingwa watetezi Manchester City dhidi ya Liverpool.
Mechi zitakazochezwa kesho ni QPR dhidi ya Norwich City, huku Arsenal itavaana na Stoke City, wakati Everton itakuwa nyumbani kuumana na Aston Villa.
Mapambano mengine ya ligi hiyo kesho ni kati ya Newcastle United dhidi ya Chelsea, huku Reading itakwaruzana na Sunderland na West Ham United itavaana na Swansea City.
Michezo mingine ya kesho ni kati ya Wigan Athletic itakaoikaribisha Southampton na Fulham itakuwa uwanja wa nyumbani kuwaalika vinara Manchester United.
Mbali na pambano la Jumapili kati ya Liverpool itakayoalikwa ugenini uwanja wa Al Itihad dhidi ya watetezi Manchester City, siku hiyo pia kutakuwa na mechi nyingine kati ya West Bromwich itakayoialika Tottenham Hotspur.

No comments:

Post a Comment