STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, February 1, 2013

DURU LA LALA SALAMA FDL KUANZA KESHO NCHINI


KIVUMBI cha Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara (FDL) duru la pili kinatarajiwa kuanza kutimka rasmi leo kwenye viwanja tisa tofauti nchini.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa mapema wiki hii na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kivumbi cha ligi hiyo kuwania nafasi tatu za kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao, kitahusisha timu 18 kati ya 24 zinazoshiriki michuano hiyo.
Ratiba hiyo inaoonyesha kuwa kundi A litakuwa na mechi tatu ambapo Mbeya City ya Mbeya itakayoikaribisha timu ya Burkina Faso ya Morogoro kwenye uwanja wa Sokoine, mjini Mbeya, Majimaji-Songea dhidi ya Kurugenzi Lindi mechi itakayochezwa uwanja wa Majimaji, Ruvuma na Polisi Iringa kuivaa Mkamba Rangers ya Morogoro uwanja wa Samora, Iringa.
Kundi B litakuwa na mechi mbili tu kati Transit Camp dhidi ya Ndanda itakayochezwa Uwanja wa Mabatini, Pwani na Moro United itaumana na Villa Squad uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Mechi nne zitapigwa kwa timu za kundi C ambapo Polisi Dodoma na Kanembwa JKT zitaumana Jamhuri, Dodoma), Morani itaumana na Mwadui mjini Kiteto-Manyara, Polisi Mara dhidi ya Pamba mjini Musoma na Polisi Tabora na Rhino Rangers wataumana uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mjini Tabora.
Ligi hiyo itaendelea siku ya Jumapili kwa mechi za kundi B ambapo Tessema ya Temeke itavaana na Green Warriors ya Kinondoni kwenye uwanja wa Mabatini-Pwani na Ashanti United itaavana na 'Vijana wa Kova' Polisi Dar kwenye uwanja wa Karume Dar.
Ligi hiyo imepangwa kumalizika mwishoni mwa Machi mwaka huu ambapo kila mshindi wa kwanza wa kundi atafuzu moja kwa moja kwa Ligi Kuu msimu wa 2013-2014.

No comments:

Post a Comment