STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, February 1, 2013

Mshindi Tigo kushuhudia marudiano Barca, Real



Meneja Ubunifu na Ofa wa TIGO, David Sekwao (kati) akizungumza na mshindi wa promosheni yao ya 'Smartcard' jana
JULIUS Kanza, mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam ameibuka mshindi wa droo ya promosheni ya ‘smartcard’ na hivyo kupata zawadi ya kugharimiwa usafiri, malazi, chakula na tiketi ya kwenda kushuhudia mechi ya robo fainali ya Kombe la Mfalme itakayowakutanisha vigogo Real Madrid na Barcelona kwenye Uwanja wa Camp Nou.
Mechi hiyo itachezwa Februari 27 ambapo Kanza atakuwa ni miongoni mwa mashabiki takriban 100,000 watakaofurika uwanjani kushuhudia pambano hilo ambalo litakuwa na msisimko zaidi baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 katika mechi yao ya kwanza iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Meneja wa ubunifu wa ofa za Tigo, David Sekwao, ndiye aliyemtangaza mshindi wakati akizungumzia promosheni hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Sekwao alisema kuwa droo hiyo ilizinduliwa mwaka jana kwa ajili ya wateja wao, na hasa wanaotumia simu za Blackberry, Android na iphone.
“Droo hizi zinaendelea kufanyika kila mwezi, robo mwaka, na kila mwaka,” alisema Sekwao, huku akitaja zawadi nyingine mbalimbali kuhusiana na droo hiyo, zikwiamo za vocha za kununulia bidhaa mbalimbali, tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi Dubai na malazi ya siku 5, na vilevile tiketi na gharama za kwenda na kurudi Uingereza kuangalia ‘live’ mechi ya ligi kuu kati ya Arsenal na Man U itakayochezwa Aprili mwaka huu.
Alisema washindi hupatikana kwa njia ya kujibu  maswali yanayoulizwa kwa washiriki kupitia simu zao.



No comments:

Post a Comment