STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, February 1, 2013

Chamoyo, Man Bizo wana mpya

Cha Moyo akiwa katika pozi zake za 'kiteja'

Man Bizzo katika pozi


WACHEKESHAJI wanaotamba kupitia kipindi cha 'Vituko Show', Abdallah Soud 'Cha Moyo' na Ally Boffu 'Man Bizo' wapo mbioni kuachia wimbo wao mpya wa pamoja uitwayo 'Ma Mjengo'.
Kibao hicho kinafuatia baada ya wasanii hao kuachia wimbo mwingine unaoendelea kutamba katika vituo vya redio na televisheni cha 'Mamido'.
Akizungumza na MICHARAZO, Cha Moyo, anayeigiza kama 'teja' lisema wimbo huo mpya umekamilika na kwa sasa wanafanya mipango ya kuusambaza ili urushwe hewani.
Cha Moyo alisema wimbo huo wa 'Ma Mjengo' ni miongoni mwa nyimbo 10 zitakazokuwa katika albamu yao waliyopanga kuitoa mwaka huu itakayofahamika kwa jina la 'Tufe Sote'.
Msanii huyo alisema wamepanga kuachia wimbo mmoja mmoja kuitambulisha albamu hiyo kabla ya kuitoa hadharani sambamba na video yake.
"Baada ya 'Mamido' kwa sasa mie na Man Bizo' tunajiandaa kuitoa hadharani wimbo wetu mwingine uitwao 'Ma Mjengo' ikiwa ni maandalizi ya kupakua albamu kamili itakayokuwa na nyimbo 10 itakayofahamika kama 'Tufe Sote'," alisema Cha Moyo.
Cha Moyo alisema wakati wakiwa katika harakati za kufyatua albamu hiyo, pia wao na wasanii wengine wa kundi lao wanaendelea kuandaa filamu za komedi katika utaratibu wa kuwapa raha mashabiki wao.

Mwisho

No comments:

Post a Comment