STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, December 16, 2013

Tanzanite kuagwa kesho, kurudiana na Wasauzi J'mosi

MECHI ya marudiano ya raundi ya pili kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia kwa wasichana wenye umri chini ya miaka 20 kati ya Tanzania (Tanzanite) na Afrika Kusini (Batsesana) itachezwa Jumamosi, Desemba 21 mwaka huu.
Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Dobsonville ulioko Soweto, Johannesburg kuanzia saa 9.30 alasiri kwa saa za Afrika Kusini. Tanzanite itaondoka Jumatano, Desemba 18 mwaka huu saa 4 asubuhi kwa ndege ya Fastjet ikiwa na msafara wa watu 29 wakiongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Khalid Abdallah.
Kikosi hicho kitaagwa kesho (Desemba 17 mwaka huu) saa 6 katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Katika pambano la kwanza lililochezwa jijini Dar es Salaam Tanzanite ilikumbana na kipigo cha mabao 4-1 toka kwa wasichana wenzao hao, hivyo kuwa na kazi ya kupata ushindi usiopungua mabao manne iwapo inataka kufuzu hatua ya mwisho kuwania nafasi mbili ya kucheza fainali za Dunia zitakazofanyika Canada mwakani.

No comments:

Post a Comment