STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, December 16, 2013

Bondia aumia mazoezini akijifua


BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Shafii Ramadhan ameumia akiwa mazoezini  akijiandaa na pambano la Desemba 22 kwenye ukumbi wa Friends Corner Hotel.

Ramadhani alikuwa aumane na Hassan Kiwale 'Moro Best' alikutana na mkasa huo mazoezini kwake kwa mujibu wa taarifa ya kocha wake, Jafari Ndame.

Pambano la wawili hao lilikuwa la kusindikiza pambano la kuwania ubingwa wa Taifa-PST kati ya bingwa mtetezi, Japhet Kaseba na Alibaba Ramadhani.

Kutokana na kuumia kwa bondia huyo hatapanda tena ulingoni kuzipiga na mpinzani wake siku ya Jumapili kama ilivyokuwa imepangwa.

Mratibu wa pambano hilo Ibrahim Kamwe alisema Moro Best sasa atazipiga na Issa Omar 'Nampepeche'.

Kamwe toka Bigright Promotion, tayari wamemalizana na Moro Best kucheza pambano hilo na Nampepeche.

Mbali na pambano hilo la siku hiyo kutakuwa na michezo mingine ukiwano wa ubingwa kati ya Fadhil Awadh atakayepigana na Karage Suba.

Bondia Mbaruku Heri na Lusekelo Daudi nao wataonyeshana kazi, kama itakavyokuwa kwa Adam Yahya atayezipiga na Harman Richard.

Mkongwe Ernest Bujiku 'Tyson' atacheza na Shaha Kassim, Jocky Hamis dhidi ya Mbena Rajabu na Shaban Kitongoji atapigana na Mwinyi Mzengela.

Kamwe alisema pia siku hiyo kutakuwepo na pambano la mateke (kickboxing) la mtanzania anayeishi Canada Kareem Kutchi dhidi ya Said Juma `Tata Boy`.

No comments:

Post a Comment