STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, January 5, 2018

Dk 70 Yanga bado ipo mbele ya kwa mabao 2-0


AJIB anakosa bao la wazi dakika ya 70, matokeo bado ni yale yale, Yanga inaongoza mabao 2-0. Pambano ni kali kwelikweli Uwanja wa Amaan.

Mkomola anaiandikia Yanga bao la pili

Yohana Mkomola
STRAIKA Yohana Mkomola ameiandikia Yanga bao la pili muda mfupi uliopita kutokana na uzembe wa mabeki wa Taifa. Yanga 2 Taifa 0. Dakika ya 63.

Dakika ya 60 matokeo bao 1-0 Yanga inaongoza

Kikosi cha Yanga
PAMBANO la Yanga na Taifa linaendelea kwenye Uwanja wa Amaan, Unguja na mpaka sasa matokeo bado yakiwa ni bao 1-0, Yanga ikiendelea kuongoza.

Simba kazi wanayo kwa Azam

Kocha Masudi Djuma akimkumbatia nahodha msaidizi, Mohammed Hussein 'Tshabalala', huku aliyekuwa Kocha Mkuu Joseph Omog na Mratibu, Abbas Ali wakishuhudia
Wachezaji wa Simba wakijifua mazoezini

RAHIM JUNIOR
HAKUNA namna ila kushinda tu. Ndivyo ambavyo Simba inapaswa kufanya wakati kesho Jumamosi itakaposhuka Uwanja wa Amaan, mjini Unguja kupepetana na Azam katika mechi ya kisasi itakayoamua hatma yao ya kutinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani hapa.
Simba ambayo ilipata ushindi wa kishindo usiku wa jana kwa kuikandika Jamhuri Pemba kwa mabao 3-1, itavaana na Azam usiku wa kesho na timu yoyote ikishinda itajihakikishia nafasi ya kutinga nusu fainali na kusubiri kujua itaungana na nani.
Azam inayotetea taji hilo ililolipata mwaka jana kwa kuichapa Simba kwa baoa 1-0 katika fainali, huo utakuwa ni mchezo wao wa mwisho na kwa sasa ikiwa na alama sita baada ya mechi tatu, kutokana na kupigwa 1-0 jioni ya leo na URA ya Uganda.
Simba yenyewe ipo nafasi ya tatu katika Kundi B ikiwa na alama nne baada ya mechi mbili, huku URA wakiongoza msimamo na pointi zao saba baada ya mechi tatu. Pambano la mwisho la Waganda hao litakuwa ni dhidi ya Simba  litakalopigwa Jumatatu jioni.
Hata hivyo Simba chini ya Kocha, Masudi Djuma imeonyesha kuwa na mabadiliko makubwa kulinganisha na ilipokuwa chini ya Mcameroon, Joseph Omog aliyetimuliwa na kama itacheza kama ilivyocheza mechi yao iliyopita, Azam ni lazima ijipange kwa Vijana hao wa Msimbazi.
Mrundi huyo aliyewapa taji Rayon Sports ya Rwanda, anatarajiwa kuendelea kumtegemea nahodha wake, John Bocco 'Adebayor' kuongoza mashambulizi akisaidiana wa nyota wengine, huku beki kiraka, Asante Kwasi aliyetupia kambani jana katika mechi yake ya kwanza akiwa na uzi wa Simba akitarajiwa kufanya yake.
Kwasi alisajiliwa na Simba hivi karibuni akitokea Lipuli na ameanza kuonyesha makeke yake na kuwafanya mashabiki wa Simba kutabasamu kwa kuamini kuwa timu yao inazidi kunoga, ikiwa siku chache tangu watolewa na kutemeshwa taji la Kombe la FA kwa kufungwa na timu ya Daraja la Pili, Green Warriors.
Azam iliyokuwa haijafungwa bao lolote katika michuano hiyo tangu mwaka jana walipobeba taji bila kupoteza, sio ya kubeza kwanui ukuta wake unaoongozwa na Mghana, Yakubu Mohammed na safu kali ya ushambuliaji chini ya Mghana mwingine, Bernard Arthur na chipukizi Paul Peter na Zayd na Shaaban Idd huenda isikubali kirahisi kupoteza mchezo huo na kutemeshwa taji la michuano hiyo.
Mbali na mchezo huo mapema jioni Singida United itakuwa uwanjani kupepetana na JKU katika mechi nyingine.

Ajibu atupia kambani, Yanga 1-0 Taifa Jang'ombe

RAHIM JUNIOR
IBRAHIM Ajib ameitanguliza Yanga mguu mmoja kwenye nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuifungia bao la kuongoza dakika chache kabla ya kwenda mapumziko akimalizia mpira wa shuti kali ha Yohana Nkomola kuokolewa na kipa wa Jang'ombe.
Kwa sasa pambano hilo lipo mapumziko na kama matokeo yatasalia hivyo, basi Yanga itaifuata Singida United iliyotangulia mapema leo mchana kwa kuilaza Mlandege.
Katika mchezo wa leo unaochezwa Uwanja wa Amaan usiku huu, Yanga imechezesha kikosi cha vijana zaidi, huku wakongwe kama kina Youthe Rostand, Nadir Haroub 'Cannavaro', Amissi Tambwe, Papy Kabamba Tshishimbi wakiwa jukwaani.

Chirwa apigwa stop, Kocha Mbao ala kibano

Obrey Chirwa
Kocha wa Mbao, Etienne Ndayiragije
RAHMA WHITE
MZAMBIA Obrey Chirwa ambaye ameididia klabu ya Yanga kucheza na kutimkia kwao Zambia, amesimamishwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuitimulia timu yake kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu.
Chirwa ameasimamiwa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi maarufu kama Kamati ya Saa 72 iliyokutana jana Alhamisi na kujadili mechi mbalimbali za Ligi Kuu (VPL) Daraja la Kwanza (FDL) na Daraja la Pili (SDL).
Soma maamuzi ya kamati hiyo na adhabu zake katika ligi hizo;

LIGI KUU YA VODACOMMechi namba 72 (Mbeya City 0 vs Simba 1).Kamishna wa mechi hiyo Billy Mwilima amepewa Onyo Kali kwa kuruhusu mchezaji Hamisi Msabila wa Mbeya City kucheza mechi bila kuonyesha leseni, hivyo kukiuka Kanuni ya 14(16 na 17) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. 
Mechi namba 81 (Ndanda 1 vs Njombe Mji 1). Klabu ya Ndanda imepigwa faini ya sh 500,000 (laki tano) kwa kutowasilisha orodha ya wachezaji wake (team match list) kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (pre- match meeting) kama ilivyoainishwa katika Kanuni ya 14(2k) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo. Adhabu dhidi ya Ndanda katika mechi hiyo iliyofanyika Novemba 24, 2017 kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu.
Pia Kamati imeiomba Sekretarieti ya Bodi ya Ligi kutoa Waraka mwingine kwa klabu kuzikumbusha kuhusu kutoa orodha ya wachezaji kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (pre-match meeting).
Mechi namba 83 (Yanga 1 vs Tanzania Prisons 1). Tanzania Prisons imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi (pre-match meeting) ikiwa na maofisa watatu badala ya wanne, hivyo kwenda kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Adhabu dhidi ya Tanzania Prisons katika mechi hiyo iliyochezwa Novemba 25, 2017 Uwanja wa Azam Complex ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu.
Wachezaji Lambart Sabiyanka wa Tanzania Prisons na Obrey Chirwa wa Yanga wamesimamishwa kwa kuzingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu kutokana na kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu, wakisubiri malalamiko dhidi yao kusikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF.
Pia Kamati imeiomba TFF iipatie Bodi ya Ligi uamuzi (ruling) wa Kamati ya Nidhamu juu ya mchezaji wa Yanga kusimamishwa baada ya mechi dhidi ya Mbao FC wakati akisubiri mashtaka yake ili kuufanyia kazi kwa ajili ya mapendekezo ya marekebisho ya Kanuni.
Mechi namba 84 (Mbao 1 vs Mwadui 0). Klabu ya Mbao FC imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kuruka uzio wa ndani na kwenda kushangilia katika eneo lisiloruhusiwa katika mechi iliyochezwa Novemba 25, 2017 Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Adhabu dhidi ya Mbao FC ni uzingativu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Mechi namba 90 (Lipuli 0 vs Tanzania Prisons 1).Mtunza Vifaa wa Lipuli FC, George Mketo amesimamishwa akisubiri suala lake la kuwatukana waamuzi katika mechi hiyo iliyofanyika Desemba 30, 2017 Uwanja wa Samora mjini Iringa kusikilizwa na Kamati ya Nidhamu. Uamuzi wa kumsimamisha umezingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu kuhusu Usimamizi wa Ligi.
Mechi namba 94 (Mbao 2 vs Yanga 0). Kocha wa Mbao FC, Etiene Ndayiragije amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya kuondolewa kwenye mchezo (ordered off) na Mwamuzi kwa kushindwa kuheshimu taratibu na kuonywa mara tatu.
Adhabu hiyo dhidi ya Kocha Ndayiragije katika mechi hiyo iliyofanyika Desemba 31, 2017 Uwanja wa CCM Kirumba imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 40(11) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha.
Pia klabu ya Mbao FC imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya kuonyeshwa kadi zaidi ya tano katika mechi hiyo. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42(10) kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Mechi namba 96 (Mwadui 2 vs Ruvu Shooting 1).Klabu ya Mwadui imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya kuonyeshwa kadi zaidi ya tano katika mechi hiyo iliyochezwa Januari 1, 2018 Uwanja wa Mwadui Complex. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 42(10) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu

LIGI DARAJA LA KWANZAMechi namba 37 Kundi B (JKT Mlale 1 v Mufindi United 0). Klabu ya Mufindi United imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na Kiongozi wake Hussein Turuka kutoa lugha chafu kwa Mwamuzi katika mechi hiyo iliyofanyika Desemba 31, 2017 mjini Songea. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Mechi namba 40 Kundi B (Mawenzi Market 1 v Polisi Dar 0). Klabu ya Mawenzi Market imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kutaka kuwapiga waamuzi na kuwashawishi ball boys kuchukua mipira iliyotoka nje na kuwapelekea jukwaani.  Adhabu hiyo katika mechi hiyo iliyochezwa Desemba 31, 2017 ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Pia Kocha Mkuu wa Mawenzi Market amepewa Onyo Kali kwa kuchelewa kwenye kikao cha maandalizi ya mechi (pre-macth meeting) kwa dakika saba. Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo.
Mechi namba 39 Kundi C (Dodoma FC 3 v Alliance Schools 2). Klabu ya Alliance Schools imepigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) kwa timu yake kuonyeshwa kadi zaidi ya tano katika mechi hiyo iliyofanyika Desemba 30, 2017 mjini Dodoma. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42(10) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Mchezaji Shaban William wa Alliance Schools amesimamishwa, hadi suala lake la kumpiga Mwamuzi litakaposikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF. Uamuzi wa kumsimamisha umezingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Usimamizi wa Ligi.
Waamuzi wote wanne; Andrew Shamba, Abdallah Mkomwa, Athuman Athuman na Omari Juma wamefungiwa miaka mitatu kila mmoja kwa kuchezesha mechi hiyo chini ya kiwango. Adhabu dhidi ya waamuzi hao imezingatia Kanuni ya 38(1a) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.
Pia Kamishna wa mechi hiyo Mackshem T. Nzunda amefungiwa miaka mitatu kwa kushindwa kutoa taarifa ya mchezo kwa usahihi. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 39(1) ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Udhibiti wa Kamishna.
Kamati imeomba suala la waamuzi hao ambao baadhi yao ni wa Ligi Kuu, kupitia TFF liwasilishwe kwenye chombo chenye dhamana ya kisheria ya rushwa kufanyiwa uchunguzi zaidi.

LIGI DARAJA LA PILIMechi namba 18 Kundi B (Africans Sports 1 v Kitayosce 2). Kitayosce imepigwa faini ya sh. 50,000 (elfu hamsini) baada ya kuhudhuria kikao cha maandalizi ya mechi (pre-match meeting) ikiwa na maofisa watatu badala ya wanne, hivyo kwenda kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Taratibu za Mchezo.
Adhabu dhidi yao katika mechi hiyo iliyofanyika Desemba 29, 2017 jijini Tanga imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu taratibu za Mchezo.
Mechi namba 16 Kundi C (Mighty Elephant 1 v Green Warriors 3). Kocha wa Green Warriors, Azish Kondo amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) baada ya kuondolewa kwenye mchezo (ordered off) na Mwamuzi kwa kutumia lugha chafu.
Adhabu hiyo dhidi ya Kocha Kondo katika mechi hiyo iliyofanyika Desemba 29, 2017 mjini Songea imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 40(10) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Udhibiti wa Makocha.
Mechi namba 18 Kundi C (Mkamba Rangers 0 v Boma 1). Klabu ya Mkamba Rangers imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wake kuingia uwanjani (pitch).  Adhabu hiyo katika mechi hiyo iliyochezwa Desemba 29, 2017 ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42(1) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Mechi namba 16 Kundi D (Area C v Nyanza). Timu ya Nyanza FC imeshushwa madaraja mawili na matokeo ya michezo yako yote imefutwa kwa kutofika uwanjani bila kutoa sababu yoyote na kusababisha mechi yao dhidi ya Area C iliyokuwa ichezwe Desemba 29, 2017 mjini Dodoma isifanyike.
Uamuzi huo dhidi ya Nyanza FC umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 28(1) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Kutofika Uwanjani. Pia kwa mujibu wa Kanuni ya 28(2) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Kutofika Uwanjani, imepigwa faini ya sh. 2,000,000 (milioni mbili) ambapo sh. 1,000,000 (milioni moja) itachukuliwa na Bodi ya Ligi, na sh. 1,000,000 (milioni moja) italipwa timu pinzani.
Vilevile Kamati imeiomba Sekretarieti kukiandikia barua Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Manyara (MARFA) ili kujua tatizo la timu hiyo.

MVUVUMWA VS FRIENDS Kamati imeipa Friends Rangers ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya Mvuvumwa kuchezesha wachezaji ambao hawajasajiliwa (non qualified) katika mechi ya Kundi A Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kati ya timu hizo iliyochezwa Oktoba 29, 2017. Mvuvumwa ilishinda mechi hiyo mabao 4-1.
Uamuzi huo dhidi ya Mvuvumwa umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(18) na 42(20) za Ligi Daraja la Kwanza. Nayo Friends Rangers imepewa ushindi kwa kuzingatia Kanuni ya 14(37) na ya Ligi Daraja la Kwanza kuhusu Taratibu za Mchezo. 
Vilevile viongozi wa Mvuvumwa waliohusika kughushi leseni zilizotumiwa na wachezaji hao ambao hawakusajiliwa watafikishwa kwenye Kamati ya Maadili ya TFF kwa ajili ya hatua zaidi.

ALLIANCE SCHOOLSKamati imepitia malalamiko ya Alliance Schools kupinga uchezeshaji wa Mwamuzi wa mechi yao dhidi ya Dodoma FC iliyofanyika Desemba 30, 2017 Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Baada ya kupitia hoja zote, Kamati haikukubaliana na malalamiko hayo kwa vile hayakuwa na vielelezo wala kanuni za kuyathibitisha. Pia kwa suala la muda, Kamati imejiridhisha kuwa kazi ya kutunza muda ni ya Mwamuzi.



Yanga, Azam, Singida wasipojipanga wamekwisha Kombe la FA


Kikosi cha Yanga

Azam FC
RAHMA WHITE
VIGOGO wa Ligi Kuu Bara, Yanga, Azam na Singida United, lazima zijipange baada ya kupewa wababe katika mechi za Raundi ya Tatu ya michuano ya Kombe la FA.
Katika droo ya michuano hiyo iliyofanyika asubuhi ya leo ikihusisha timu 32 zilizopenya hatua hiyo, Yanga imepewa wababe wa Mbeya City, Ihefu FC ya Mbalali, huku Singida wakikabidhiwa watemi wea Simba, Green Warriors.
Azam yenyewe imepangwa kupepetana na Shujaa FC katika mechi itakayochezwa Uwanja wa Mkamba CCM, mjini Morogoro ili kusaka tiketi ya kuingia Robo fainali.
Katika raundi hiyo ya imehusisha timu nne za Mabingwa wa Mikoa (RCL), tatu za Ligi Daraja la Pili (SDL), 12 za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na klabu 13 za Ligi Kuu zilizopenya kwenye mechi zao za raundi ya pili zilizochezwa mwishoni mwa mwaka jana.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mechi za raundi hiyo zitachezwa kati ya Januari 31 na Febaruari Mosi kwenye miji tofauti kulingana na ratiba ilivyo.
Kabla ya mechi hizo za raundi ya tatu kuchezwa tayari zimechezwa mechi 59 na magoli 137 yamefungwa.

Cheki ratiba kamili ilivyo na viwanja vyake:

Kagera Sugar     v Buseresere FC- Kaitaba, Bukoba
Shupavu FC       v Azam FC- Mkamba CCM, Morogoro
Majimaji Rangersv Mtibwa Sugar - Ilulu, Lindi
Kariakoo Lindi     v Mbao FC- Ilulu, Lindi
Prisons               v Burkina Fc- Sokoine, Mbeya
Green Warriors    v Singida FC-Azam Complec, Dar
Mwadui FC          v Dodoma FC- Mwadui, Shinyanga
Ihefu FC              v Yanga SC-Sokoine, Mbeya
JKT Tanzania        v Polisi Dar- Uhuru, Dar
Polisi Tanzania      v Friends- Ushirika, Moshi
Pamba SC            v Stand United-Kirumba, Mwanza
Ndanda FC           v Biashara United-Nangwanda Kiluvya United      v JKT Oljoro-Mabatini, Pwani
Njombe Mji          v Rhino Rangers-Sabasaba Njombe
Majimaji Fc          v Ruvu Shooting -Majimaji, Songea
KMC                    v Toto Africans- Uhuru, Dar

Singida United yatangulia nusu fainali, Azam yatibuliwa Mapinduzi Cup

Kikosi cha Azam ambacho jioni hii kimelala mbele ya URA

Wachezaji wa Singida wakipongezana katika mechi yao ya Kombe la Mapinduzi

Danny Usengimana akijiandaa kupioga penalti iliyoiandikia Singida bao la kuonmgoza jioni ya leo
TARIQ JUNIORVIJANA wa Hans Pluijm, Singida United sio wa mchezo mchezo, baada ya jioni ya leo kuwa timu ya kwanza kutinga nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi 2018 kwa kuichakaza Mlandege kwa mabao 3-0, huku Azam ikitenguliwa udhu na Watoza Ushuru wa Uganda.
Singida imefikisha pointi 9 ikiwa imecheza mechi tatu na kukata tiketi moja ya Kundi A ambalo lina timu ya Yanga inayoshuka dimbani usiku huu kuumana na Taifa Jang'ombe katika mechi nyingine kali ya michuano hiyo.
Walima Alizeti hao wamejihakikishia nafasi hiyo kutokana na ukweli timu zilizopo nyuma yake ni Yanga pekee inayoweza kuzipiku pointi ilizonazo, huku pia ikiwa na michezo miwili mkononi ya kufungia makundi.
Mabao ya Danny Usengimana aliyefungwa kwa penalti dakika ya 29 na mengine Kenny Ally la dakia ya 37 na lile la Lubinda Mundia la dakika ya 56 yalitosha kuipa ushindi Singida inayoshiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza mwaka huu.
Wakati Singida ikichekelea kutangulia nusu fainali, watetezi wa taji hilo, Azam ilinyooshwa na URA ya Uganda kwa bao 1-0 na kutenguliwa rekodi yao iliyokuwa ikishikilia kwa kutoruhusu bao lolote tangu michuano ya 2017.
Azam ilibeba taji hilo Januari mwaka jana kwa kucheza mechi zake zote bila kuruhusu bao lolote achilia mbali kupoteza mchezo, lakini URA wakiwa na utulivu mkubwa waliwaotea Matajiri nao na kuwatengua 'udhu' kwa bao la dakika ya 32 lililofungwa na Nicholaus Kabaga akipiga tobo kipa Razak Abalora.
Hata hivyo Azam bado ina nafasi ya kupenya hatua ya nusu fainali kama itapata matokeo mazuri katika mechi yao ya mwisho kesho dhidi ya Simba ambayo inafuatia nyuma yao kwa alama zao nne baada ya kucheza mechi mbili.
URA imefikisha pointi saba na kuongoza msimamo wa kundi hilo la B, kisha Azam ikifuata na alama zao 6. Timu zote tatu zina nafasi sawa ya kutinga nusu fainali kupitia kundi hilo na zinatarajiwa kukutana zenyewe kuamua hatma yao.
Cheki matokeo ma msimamo mzima wa michuano hiyo inayoingia mwaka wa 11 tangu kuasisiwa kwake mnamo Mwaka 2007;
Kombe la Mapinduzi 2018
Kundi A
Mlandege, JKU, Zimamoto, Yanga, Taifa Jang'ombe, Singida United

Kundi B
Jamhuri, Mwenge, Simba, Azam, URA

Des 29, 2017
Mlandege 2-1 JKU
Jamhuri 0-1 Mwenge
Zimamoto 2-1 Taifa Jang’ombe

Des 30, 2017
Zimamoto 0-1 JKU
Taifa Jang’ombe 1-0 Mlandege

Des 31, 2017
Azam 2-0 Mwenge
Jamhuri 1-1 URA

Jan 01, 2018
Mlandege 2-1 Zimamoto
JKU 0-0 Taifa Jang’ombe

Jan 02, 2018
Singida United 3-2 Zimamoto
Simba 1-1 Mwenge
Yanga 2-1 Mlandege

Jan 03, 2018
URA 1-0 Mwenge
Azam 4-0 Jamhuri
Taifa Jang’ombe 1-3 Singida United

Jan 04, 2018
JKU 0-1 Yanga
Simba 3-1 Jamhuri

Jan 05, 2018
Mlandege 0-3 Singida United
URA 1-0 Azam
Yanga v Taifa Jang’ombe

Jan 06, 2018JKU v Singida United
Simba v Azam

Jan 07, 2018Zimamoto v Yanga

Jan 08, 2018Simba v URA
Yanga v Singida United

Nusu FainaliJan 10, 2018Kinara Kundi A v
Mshindi wa Pili Kundi B

Kinara Kundi B v
Mshindi wa Pili Kundi A
Saa 2:15 usiku

FAINALIJan 13, 2018Saa 2:15 usiku

Msimamo:
Kundi A
               P   W   D    L   F   A    Pts
 

1.Singida 3    3    0    0    9    3    9
2.Yanga   2    2    0    0    3    1    6
3.M'ndege5   2    0    3    5    7    6
4.Taifa     4    1    1    2    3    5    4
5.JKU      4    1    1    2    2    3    4
6. Z'moto 3    1    0    2    3    4    3

Kundi B
              P   W    D   L    F   A    Pts
 

1.URA     3    2    1    0    3    1     7
2.Azam   3    2    0    1    6    1    6
3.Simba  2    1    1    0    4    1    4
4.Mwenge4    1    1    2    2    4    4
5.Jamhuri4    0    1    3    2    9    1