STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, March 8, 2014

Al Ahly yazidi kuimarika, ila Yanga wapo kamili kuwaua kesho

Rabia
Rami Rabia
Nahodha Nadir Cannavaro (kati) aliyewaua Al Ahly wiki iliyopita akiwa na nyota wenzake, Athuman Idd Chuji na Haruna Niyonzima. Bila shaka kesho wataendelea kuwapa raha Watanzania kwa kuing'oa Ahly.
KUREJEA kwa nyota wake wawili beki Rami Rabia aliyekuwa kaumia bega wakati akiitumikia timu yake ya taifa ya Misri katika mechi ya kirafiki dhidi ya Bosnia siku ya Jumatano na kiungo Moussa Yedan kunaweza kuiweka pagumu Yanga dhidi ya mechi yao ya kesho dhidi ya Al Ahly huko nchini Misri.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Misri, wachezaji hao wanatarajia kushuka dimbani kesho kukabiliana na Yanga kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayochezwa kwenye uwanja wa Mexx, jijini Alexandria.
Kuongezeka kwa wachezaji hao kunaifanya Mashetani hao Wekundu wa Misri kuchekelea wakiamini Yanga itakufa kama walivyouwawa wao ugenini kwa kuwalaza bao 1-0 kwa goli la kichwa cha kuchupia cha nahodha, Nadir Haroub Cannavaro.
“Rabia yu tayari kwa mechi dhidi ya Young Africans baada ya kupoma jeraha la bega aliloumia wakati akiichezea Mafarao na kusshinda 2-0," mtandao wa Ahly uliandika taarifa hiyo.
“Aliungana na wenzake katika mazoezi ya Ijumaa, akiwa hana tatizo lolote," taarifa hiyo iliongeza.
Taarifa hiyo iliongeza pia kiungo wao Moussa Yedan naye atakuwepo katika mechi hiyo ya Jumapili, ingawa itawakosa mshambuliahji wao Emad Meteb aliye majeruhi wa misuli.
Hata hivyo Yanga waliokamili gado jijini humo, inaripoti wana ari kubwa baada ya kufanya mazoezi leo katika uwanja huo watakaoutumia kesho baada ya kushtukizwa na wenyeji wao kwamba mechi imehama toka Cairo.
Kitu cha kufurahisha mechi hiyo haitakuwa na watazamaji na kuwapa nafasi nzuri Yanga kuwashikisha adabu Wamisri hao na ikiwezekana kuwavua taji kwenye ardhi yao ya nyumbani kama walivyowahi kufanya watani zao Simba dhidi ya Zamalek waliokuwa watetezi wa michuano ya mwaka 2003.
Taarifa kutoka Misri zinasema kuwa kikosi cha wachezaji wa Yanga wapo fiti wakiwa hakuna majeruhi haya mmoja na kwamba iwe isiwe ni lazima Mashetani Wekundu hao wafe licha ya hila zao za kuchelewa kutajwa uwanja wa mchezo huo kama inavyotakiwa na taratibu za soka za kimataifa.
Mungu ibariki Tanzania Ibariki Yanga kesho iweze kuvunja rekodi kwa kuing'oa Al Ahly kwao.

Wababe wa Azam wang'oka Kombe la Shirikisho


WABABE wa waliokuwa wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Azam timu ya Ferroviario de Beira imeondolewa kwenye michuano hiyo baada ya kunyukwa bao 1-0 na ZESCO ya Zambia katika mechi ya marudiano iliyochezwa leo jijini Lusaka.
Ferroviario iliiondosha Azam kwenye raudni ya awali kwa kuilaza jumla ya mabao 2-1 baada ya awali kulala 1-0 nyumbani Tanzania na kwenda kushinda kwao 2-0, ilishindwa kuhimili vishindo vya Wazambia ambao katika mechi ya awali ugenini ililazimisha sare.
Katika mechi nyingine za michuano hiyo zilizochezwa leo, Etoile du Sahel imepata ushindi mnono nyumbani kwa kuicharaz a CARA Brazzaville kwa maba0 3-0 na kufuzu kwa jumla ya mabao 3-1 kwani mechi iliyopita walilala ugenini bao 1-0 mjini Brazzaville Congo.
Nayo timu ya ASEC Memosa ya Ivory Coast, imepenya raundi ya pili baada ya kulazimishwa sare nyumbani na COB ya Mali lakini ikifaidika na ushindi wa mabao 2-0 iliyopata ugenini wiki iliyopita, huku How Mine ya Zimbabwe ikiing'oa St Michel United ya Sychelles kwa jumla ya mabao 6-4 baada ya leo kulala ugenini mabao 3-1 kwa Washelisheli hao, ila katika mechi yao iliyoipita walishinda nyumbani mabao 5-1.
AS Kigali nayo ilipenya hatua ya pili baada ya kuingoa Al Ahly Shendi ya Sudan Kusini kwa mikwaju ya penati baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 ugenini wiki moja baada ya kushinda ushindi kama huo nyumbani.
Timu ya  Bayesla United ya Nigeria ilifuzu hatua inayofuata baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Kondzo ya Kongo ambao walitoka nao suluhu ya kutofunga katika mechi yao wiki iliyopita.
Katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika zilizochezwa leo mbali na mechi tuliyoripoti mapema kati ya KCCA na Nkana, timu ya Kaizer Chiefs ya Agfrioka Kusini ilifuzu raundi ya pili kwa kishindo baada ya kuibutua Liga Maculmana ya Msumbiji kwa kuilaza mabao 3-0 na kufuzu kwa jumla ya mabao 7-0 baada ya wiki iliyopita kushinda nyumbani kwa mabao 4-0.
Nayo timu ya Leopards de Dolisie ya  Kongo imeingoa 1st de Agosto ya Angola kwa jumla ya mabao 4-3 baada ya leo kukubali kipigop ugenini mjini Luanda cha mabao 2-00 lakini ikibebwa na ushindi mnono iliypata nyumbani kwao wiki iliyopita ilkipoifumua Waangola mabao 4-1.
Mabingwa wa zamani wa Afrika Enyimba ya Nigeria licha ya kushinda bao 1-0 ugenini dhidi ya Real Bamako imejikuta iking'oka mashindanoni baada ya mechi ya kwanza kulala nyumbani mabao 2-1 kwa wapinzani wao na kufanya matokeo kuwa 2-2 ila Bamako kunufaika na faida ya mabao ya ugenini.
Nao ES Setif ya Algeria kufuzu hatua ya pili baada ya kulazimisha suluhu ugenini dhidi ya ASFA-Yannenga ya Burkina Faso baada ya wiki iliyopita kupata ushindi mnono nyumbani wa mabao 5-0.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea kesho kwa michezio mingine kadhaa ya kuhitimisha mechi za marudiano na kufahamika timu zilizotinga hatua ya 16 Bora, ambapo moja ya mechi hizo itazikutanisha watetezi Al Ahly ya Misri dhidi ya Yanga ambayo ilishinda mechi ya kwanza nyumbani Tanzania kwa bao 1-0.
Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu itachezwa kwenye jiji la Alexandria, baada ya wenyeji kuhofia mashabiki wao wakorofi jijini Cairo ambao walichukizwa na kipigo ilichopewa timu yao ugenini na Yanga.

Chelsea yaibutua Spurs 4-0 darajani

Et'oo akishangilia bao lake
Samuel Eto'o is congratulated by teammate Branoslav Ivanovic after putting Chelsea ahead
Eto'o akipongezwa baada ya kufunga bao la utangulizi
John Terry
Nahodha John Terry akimpongeza Eto'o
VINARA wa Ligi Kuu ya England ikiwa katika kiwango tishio imeitubua Tottenham Hotspur kwa mabao 4-0 katika mfululizo wa mechi za ligi hiyo, huku mtokea benchi Demba Ba akifunga mabao mawili dakika za jioni kwenye uwanja wa Stanford Bridge.
Samuel Ot'oo alikuwa wa kwanza kuifungia Chelsea bao dakika tano baada ya kuanza kwa kipindi cha pili kabla ya Edin Hazard kuongeza la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 65 baada ya Younes Kaboul kumchezea vibaya Et'oo kosa lililomfanya alimwe kadi nyekundu na kutolewa uwanjani.
Kocha Jose Mourinho alifanya mabadiliko ya haraka haraka akimtoa Etoo na nafasi yake kuchukuliwa na Demba Ba ambaye hakuwa na ajizi baada ya kufunga mabao mawili katika dakika ya 88 na 90 yaliyotosha kuihakikisha Chelsea kukaa kileleni ikiwa na pointi 66 saba zaidi ya iliyonayo Liverpool na Arsenal zenye 59 kila moja..
Katika mechi nyingine za mapema Cardiff City ikiwa nyumbani iliisasambua Fulham kwa kuicharaza mabao 3-1, Southampton ikiwa ugenini ilipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Crystal Palace, huku Norwich City na Stoke City ilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

Barcelona yazamishwa tena Hispania

Fausto Rossi celebrates
Fausto Rossi akishangilia bao lake lililoizamisha Barcelona leo
Lionel Messi looks upsetBAO pekee lililofungwa na Fausto Rossi katika dakika 17 lilitosha kuizamisha Barcelona ikiwa ugenini wakati ikiumana na Real Valladolid katika mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania na kuifanya watetezi hao kushindwa kuwaengua kileleni Real Madrid watakaoshuka dimbani kesho.
Barcelona licha ya kuchezesha kikosi chake cha hatari kikiwajumuisha nyota wake kama Lionel Messi, Neymar na wengine ilishindwa kabisa kufurukata mbele ya wenyeji wao na kuwafanya walale na kuwaacha Real wakipumua kileleni wakitofautiana pointi moja, Real wakiwa na 64 na Barca wakiwa na 63 wakitishiwa kuporomoshwa zaidi hadi nafasi ya tatu iwapo Atletico Madrid itakayoshuka dimbani baadaye kama itaibuka na ushindi ugenini dhidi ya Celta Vigo.
Katika mechi nyingine iliyochezwa jioni hii timu ya Real Betis iliifunga Getafe kwa mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa nyumbani kwa washindi.

Mbeya City yaishusha Yanga, Ruvu yazinduka


Mbeya City iliyotakata nyumbani
Ruvu Shooting ilizinduka
WAKATI watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wakiwa ugenini kujiandaa na mechi yao ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly, nyumbani wameenguliwa kutoka nafasi ya pili ya Ligi Kuu baada ya Mbeya City kupata ushindi wa 3-1 dhidi ya Rhino Rangers.
Mbeya City ikiwa uwanja wa nyumbani wa Sokoine, jijini Mbeya ilipata ushindi huo na kufikisha jumla ya pointi 39 na kuwa nyuma ya pointi moja dhidi ya Azam wanaoongoza msimamo ikiwa na pointi 40 licha ya kutofautiana michezo iliyocheza.
Mabao ya washindi hao waliwekwa kimiani na Saada Kipanga aliyefunga mabao mawili akiiangamiza timu yake ya zamani aliyoipandisha daraja ambayo inaendelea kukaa mkiani kwa msimamo wa ligi hiyo inayoelekea ukingoni kabla msimu haujamalizika.
Kabla ya Kipanga kufunga mabao hayo, beki wa Mbeya City Yohana Morris alijifunga katika dakika ya pili ya mchezo huo katika harakati za kuokoa shambulizi kali la Rhino Rangers.
Kipanga alisawazisha dakika ya 8 kabla ya kuongeza jingine dakika ya 24 na baadaye Deusi kaseke kufunga bao la tatu dakika ya 35.
Kipindi cha pili hakukuwa na jipya zaidi ya matukio ya kibabe yanayodaiwa kufanywa na wachezaji wa Rhino na kocha wao msaidizi, Tumaini Shija kupewa kadi nyekundu kwa kumtolea matusi mwamuzi Godfrey Tumaini.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo 'wazee wa wiki' Ruvu Shooting ikiwa uwanja wa nyumbani Mabatini-Mlandizi, ilipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya maafande wenzao wa Oljoro JKT na kuwafanya wakwee hadi nafasi ya saba ya msimamo ikiwa na pointi 28.
Bao lililoipa ushindi Ruvu ambayo katika mechi zake mbili zilizopita ilizipoteza kwa Simba na Yanga na kufungwa mabao 10-2, liliwekwa kimiani na Ayoub Kitala katika dakika ya 65.
Nao mabingwa wa zamani wa soka nchini Coastal Union ya Tanga ilishindwa kutamba baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na Ashanti Utd kwenye uwanja wa Mkwakwani.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi kati ya Prisons-Mbeya itakayoikaribisha Simba kwenye uwanja wa Sokoine na jijini Dar kwenye uwanja wa Chamazi, JKT Ruvu iliyokea Kagera ilipoenda kukumbana na kipigo kwa Kagera Sugar itaumana na Mtibwa Sugar.

Timu ya Babi, UiTM yazidi kuzama Malaysia

Photo: Thamani.yangu na uwezo .wangu na nithamu yangu ndio inayonifanya .nipewe ukepten..ndani ya nchi na nje ya .nchi..nawatakia kila la heri YANGA..
Abdi Kassim (kushoto wa kwanza) akiwa na utepe wa unahodha katika timu yake uya UiTM
TIMU ya UiTM ya nchini Malaysia anayoichezea kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Kassim 'Babi' imeendelea kuwa urojo katika Ligi Kuu ya nchi hiyo baada ya jana kukubali kipigo cha tatu mfululizo kwa kufungwa na 'vibonde' wa ligi hiyo Perlis.
Babi aliyekuwa nahodha katika mchezo huo, aliishuhudia UiTM ikilambwa mabao 2-1 katika mechi hiyo iliyochezwa uwanja wa Darul Aman mjini Alor Setar.
Hicho kilikuwa ni kipigo cha tatu mfululizo kwa timu hiyo, kwani baada ya kushinda mechi yao ya kwanza dhidi ya Kuala Lumpur kisha kutoka droo na Johor, ilijikuita ikifungwa mechi mbili mfululizo kabla ya jana kuotewa tena na kuifanya timu hiyo isaliwe na pointi zake nne ikiwa nafasi ya 9 katia ya timu 12 za ligi hiyo.
Katika mechi nyingine zilizochezwa jana baada ya wiki kusimama kwa wiki mbili,timu ya PDRM ilizididi kujizatiti kileleni baada ya kushinda mechi yake ya tano mfululizo kwa kuizamua DRM -Hicom kwa mabao 2-1 ikiwa ugenini, Sabah ikishinda nyumbani kwa mabao 3-2, PBAPP ikilala nyumba 2-1 na Palau Pinang, Felda United ikitoshana nguvu ya kufunga 2-2 na Johor naNegeri Sembilan na Kuala Lumpur SPA zikitosa sare ya bila kufungana.KCCA yakwama kwa Nkana Ligi ya Mabingwa Afrika

The KCC FC team that started against Zambia's Nkana Red Devils in Kitwe
KCCA iliyong'olewa jioni hii kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kukubali kipigo nyumbani
MABINGWA wa Kombe la Mapinduzi, KCCA ya Uganda muda mfupi uliopita imejikuta ikiaga mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungwa mabao 2-1 na Nkana Red Devils ya Zambia katika mechi ya marudiano iliyochezwa jijini Kampala Uganda.
KCCA ilipata sare ya mabao 2-2 ugenini wiki iliyopita mjini Lusaka, ilijikuta ikienda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao 1-0 kabla ya kulirejesha na kuonekana kama ina nafasi ya kusonga mbele kabla ya kuruhusu bao la ushindi la wageni linalowafanya Waganda hao kung'oka kwa jumla ya mabao 4-3.
Washindi wa mchezo huo, Nkana sasa itavaana na Zamalek ya Misri katika mechi ya mkondo unaofuata baada ya jana Wamisri hao kulazimishwa sare ugenini ya bila kufungana na Kabuscorp ya Angola na kufuzu kwa jumla ya bao 1-0 kwa vile mechi iliyopita Zamalek ilishinda nyumbanio bao 1-0.

Arsenal yatinga Semi Fainali ya FA, yaifumua Everton 4-1

Arteta kifungwa mkwaju wake wa penati

Arsenal v Everton
Lukaku akishangilia bao lake ambalo halikuisaidia Everton kwa Arsenal leo
Giroud scores
Mtokea benchi Oliver Giroud akiwatoka washindi na kufunga moja ya mabao yake mawili leo

KIUNGO Mesut Ozil amefunga bao boa na kusaidia jingine lililtumbulizwa kimiani na Oliver Giroud wakati Arsenal ikiifumua Everton kwa mabao 4-1 na kutinga hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la FA kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2009.
Ozil ambaye amekuwa na wakati mgumu kwa mashabiki wa Arsenal tangu alipokosa mechi ya Arsenal dhidi ya Liverpool walipofungwa mabao 5-1 na kuja kukosa penati kwenye Ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern, alionyeha kiwango cha juu katika mchezo huo uliochezwa uwanja wa Emirates.
Kiungo huyo wa Ujerumani alifunga bao la kuongoza dakika ya 7 kwa pasi ya Santi Cazorla kabla ya Romelu Lukaku kuisawazishia Everton bao dakika ya 32 na kufanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa sare ya 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa Arsenal kujiongezea bao la pili kwa amkwaju wa penati  dakika ya 68 iliyofungwa na Mikel Arteta kabla ya mtokea benchi Giroud kufunga mengine mawili dakika za saba za mwisho za mchezo huo.
Mchezaji huyo alifunga bao lake la kwanza na la tatu katika mchezo huo dakika ya 83 akimalizia kazi ya Bacary Sagna na dakika mbili baadaye kuongeza jingine baada ya kazi nzuri ya Ozil na kuiofanya Arsenal kuibuka kidedea kwa maba0 4-1 na kutina Nusu Fainali ya michuano ya Kombe hilo.

Michezo mingine ya Robo Fainali ya michuano hiyo itachezwa kesho kwa mechi itakayozikutanisha Sheffield United dhidi ya Charlton Athletic mechi itakayochezwa mapema kabla ya Hull City kuvaana na Sunderland na Manchester City usiku kuvaana na Wigan Athletic.

Manchester Utd yaifumua West Brom 3-0

http://news.bbcimg.co.uk/media/images/73455000/jpg/_73455370_73455369.jpg
Wayne Rooney akifunga bao la pili la Manchester Utd leo
Man Utd defender Phil Jones heads his side into the lead at West Brom
Jones akifunga bao la kwanza la Mashetani Wekundu kwa kichwa

MASHETANI wekundu wakiwa ugenini muda mfupi uliopita imepata ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya West Bromwich kiatika mechi ya Ligi Kuu ya England na kuifanya timu hiyo kuiengua Everton kwenye nafasi ya sita ikiifupumua Tottenham Hotspur inayoshuka dimbani baadaye dhidi ya Chelsea.
Mabao ya Phil Jones la dakika ya 34 kwa pasi ya Robin van Persie  lililidu kipindi cha kwanza na mengine ya kipindi cha pili kupitia wa Wayne Rooney dakika ya 65 na Danny Welbeck  kwa pasi ya Rooney dakika ya 82 ilitosha kuifanya Manchester United kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 na kufikisha pointi 48 sawa na Everton, lakini wakitangulia mbele kwa uwiano wa mabo ya kufunga na kufungwa.
Ushindi huo wa ugenini umekuwa afueni kwa kocha David Moyes kuelekea kwenye mbio za kupata nafasi ya ushiriki wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani baada ya mbio za ubingwa kuwa mbali kwao kwa sasa na kuelekea kutemeshwa taji lake.

Tambwe, Mgosi walimwa faini, kisa...!

Tambwe wa Simba
Mgosi
STRIKA nyota wa Simba, Amissi Tambwe amepigwa faini ya Sh 500,000 kwa kuonyesha ishara ya matusi wakati akishangilia bao lake.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema Tambwe alionyesha alama ya matusi kutumia kidole chake wakati anashangilia.

Tambwe alifanya hivyo baada ya kuifungia Simba bao wakati ilipoivaa Mbeya City mjini Mbeya.

Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya bao 1-1, Tambwe raia wa Burundi akiwa ni shujaa wa Simba.

Hadi sasa Mrundi huyo ana mabao 17 akiwa kileleni kwa upachikaji mabao.

Naye, mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Musa Mgosi amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kosa la kupiga uwanjani kwenye mechi dhidi ya Ashanti United ambapo vilevile atakosa mechi tatu za ligi. Coastal Union imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa washabiki wake kumrushia chupa za maji kipa wa Mbeya City.

IDFA yaitakia kila la heri Yanga kesho Misri

Yanga yenye kibarua kizito kesho mjini Alexandria
UONGOZI wa Chama cha Sokla Wilaya ya Ilala (IDFA) umeitakia kila la heri na kuwaomba watanzania kuiombea dua njema wawakilishi pekee wa michuano ya kimataifa, Yanga katika mchezo wao wa kesho dhidi ya Al Ahly ya Misri.
Yanga wataumana na wenyeji wao katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo Al Ahly ndiyo watetezi wake, ili kuamua hatma ya  kuvuka hatua ya 32 Bora kutinga 16 Bora ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika kwa ngazi ya klabu, mechi ikichezwa mji wa Alexandria badala ya Cairo.
Kwa kutambua Yanga ina kibarua kizito mbele ya Ahly hiyo kesho, uongozi wa IDFA ambao ni walezi wa klabu za Ilala ikiwamo Simba na Yanga, wamewaomba watanzania kuiombea dua njema timu hiyo na wao wenyewe (IDFA)  wakisema wanaitakia kila la heri kuweza kuwang'oa Wamisri.
Katibu Mkuu wa chama hicho, Daud Kanuti aliiambia MICHARAZO kuwa, IDFA ipo katika maombi kuiombea Yanga ifanye vyema na kuendelea kupeperusha bendera ya taifa na kuwaomba wadau wengine wa soka bila kujali itikadi zao kuwaombea dua njema wawakilishi hao wavuke hatua hiyo.
Kanuti alisema kufanya vyema kwa Yanga katika mechi hiyo na michuano hiyo ya Mabingwa, ni sifa kwa Tanzania na kuongeza, anaamini wachezaji wa Yanga wakicheza 'jihad' na tahadhari kubwa dhidi ya wapinzani wao wanaweza kurejea kilichofanywa na Simba.
Kanuti alisema anaamini wachezaji  wameandaliwa kisaikolojia ili kuhimili vitimbi wanavyoweza kukutana navyo Misri kama ilivyo kawaida ya mechi za timu za kiarabu wanapokuwa uwanja wa nyumbani.
"IDFA tunaitakia kila la heri na kuiombea dua njema ili ifanye vyema kwenye mechi yake ya Jumapili, chama tumefurahishwa na ilichokifanya katika mchezo wa kwanza na tunaamini watarejea tena ugenini," alisema.
"Wana nafasi ya kurejea ilichofanywa na watani zao walipoing'oa Zamalek katika ardhi yao mwaka 2003, ila ni muhimu wachezaji wakaandaliwa kupambana na kuweka akili zao katika pambano hilo ili kuivusha Yanga katika hatua hiyo," aliongeza Kanuni.
Kanuti alisema IDFA inatambua mchezo huo wa kesho utakuwa mgumu kwa vile Al Ahly itakuwa nyumbani na rekodi zinaonyesha timu za kiarabu huwa wagumu kufungwa kwao, lakini Yanga ikipambana itawaondosha watetezi hao kama ilivyofanya Simba kwa Zamalek mwaka 2003.
Katika mwaka huo Simba ilishinda nyumbani bao 1-0 dhidi ya Zamalek pia ya Misri waliokuwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa mwaka huo kisha kwenda kukubali kipigo kama hicho ugenini mjini Cairo na kupigiana penati na Simba kuibuka kidedea kuingia hatua ya makundi.
Iwapo Yanga itafanikiwa kuing'oa Ahly huenda ikakutana kwenye raundi inayofuata kati ya timu ya Berekum Chelsea ya Ghana au Ahly Benghazi ya Libya ambazo zilitoka sare ya 1-1 katika mechi yao ya awali na zinatarajiwa kurudiana leo.

Ushirikina waiponza Simba, TFF yakunjua kucha

Kikosi cha Simba na kocha wao, Logarusic (kulia waliosimama)
BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeipiga faini ya jumla ya sh. milioni moja klabu ya Simba kutokana na makosa mbalimbali ikiwemo vitendo vinavyoashiria ushirikina uwanjani.

Simba ilifanya vitendo hivyo katika mechi yake dhidi ya Mbeya City ambapo imepigwa faini ya sh. 500,000. Pia imepigwa faini nyingine ya sh. 500,000 kwa makocha wake Loga, Selemani Matola na Idd Pazi kuingia uwanjani na kumzonga mwamuzi kwenye mechi hiyo.

Mbeya City imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa washabiki wake kuingia uwanjani kwenye mechi dhidi ya Kagera Sugar iliyochezwa mjini Bukoba. Klabu za Yanga na Coastal Union zimepigwa faini ya sh. 500,000 kila moja kwa washabiki wao kurusha chupa za maji uwanjani wakati timu hizo zilipopambana jijini Tanga.

Kiungo wa Mtibwa Sugar, Shabani Nditi amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kumpiga mchezaji wa Simba, wakati Salvatory Ntebe pia wa Mtibwa Sugar amepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kumtukana refa kwenye mechi dhidi ya Mbeya City.

Nayo JKT Ruvu imepigwa faini ya sh. 300,000 kwa kuchelewa kufika uwanjani kwenye mechi dhidi ya Simba iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Vilevile wamiliki wa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wameandikiwa barua ya kufanya marekebisho ya vyumba vya wachezaji, kwa vile havina hewa ya kutosha.

Kwa upande wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) klabu zilizopigwa faini kutokana na makosa mbalimbali ni Friends Rangers (sh. 200,000), Lipuli (sh. 200,000), Majimaji (sh. 400,000), Polisi Morogoro (sh. 400,000) na Transit Camp (sh. 200,000).

Kocha Msaidizi wa Polisi Morogoro, John Tamba atapelekwa kwenye Kamati ya Maadili kutokana na vitendo visivyo vya kimaadili katika mechi dhidi ya Burkina Faso.

Kiongozi wa Lipuli, Hamis Kiemba na wachezaji Boniface Sawaka, George Enock na Green Paul watapelekwa katika Kamati ya Nidhamu kutokana na utovu wa nidhamu waliofanya kwenye mechi dhidi ya Kimondo.

Naye mchezaji Sangalau Nyamoka wa JKT Kanembwa aliyelalamikiwa uhalali wake na Polisi Tabora suala lake linapelekwa Kamati ya Nidhamu.

Huyu ndiye kocha mpya wa Taifa Stars


Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
KOCHA mpya wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ni Martinus Ignatius ‘Mart’ Nooij ambaye anatarajiwa kutambulishwa rasmi Machi 24 mwaka huu na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi.
Tangu TFF kusema inatafuta kocha mpya atakayerithi mikoba ya Mdenmark, Kim Poulsen, BIN ZUBEIRY imekuwa ikifuatilia kwa undani mwalimu mpya wa Stars atakuwa nani na sasa inaibuka na jibu ni Mart Nooij.
Tayari Nooij ambaye kwa sasa ni kocha wa St George ya Ethiopia amekwishasaini Mkataba wa miaka miwili na TFF na atakuja nchini mwishoni mwa mwezi huu.
Atatutoa?; Kocha mpya wa Taifa Stars Mart Nooij anatarajiwa kutua nchini mwishoni mwa mwezi huu

Ulikuwa mchakato makini, uliohusisha wataalamu na washauri wa kimataifa juu ya masuala ya ufundi ya soka ambao umefanikisha kupatikana mwalimu huyo wa Kiholanzi aliyezaliwa Julai 3, mwaka 1954 mjini Beverwijk, Uholanzi.
Nooij amewahi kuwa mwalimu maalum katika programu za maendeleo ya soka katika Chama cha Soka Uholanzi (DFA) na pia amewahi kufundisha timu ya EVC 1913 ya Marekani na baadaye Kazakhstan.
Alikuwa kocha wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Burkina Faso katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2003 na mwaka 2004 alikuwa kocha wa muda wa klabu ya FC Volendam ya Uholanzi.
Mwaka 2007 aliteuliwa kuwa kocha wa Msumbiji na akaiwezesha kufuzu kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2010, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza Mambas wanashiriki AFCON baada ya msoto wa miaka 12.
Hata hivyo, katika fainali hizo, Msumbiji ilishika mkia katika kundi lake baada ya kuambulia sare moja na kufungwa mechi mbili. Baada ya kukosa tiketi ya  AFCON 2012, Nooij akajiuzulu Septemba mwaka 2011 na nafasi yake kuchukuliwa na Mjerumani, Gert Engels.
Aprili 19 mwaka 2012, aliajiriwa na klabu ya Santos ya Afrika Kusini, ambako hata hivyo alifukuzwa Desemba 18, mwaka 2012 na kunyakuliwa na St George ya Ethiopia anakoendelea na kazi hadi sasa.
Baada ya kusaini Mkataba wa miaka miwili na TFF kuja kuifundisha Stars, Nooij anasubiri barua maalum ya kuruhusiwa kuondoka baada ya kukamilisha taratibu za kuvunja Mkataba uliokuwa unaelekea ukingoni na klabu hiyo ya Addis Ababa.
Yanga SC pia inafundishwa na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm.
Chanzo: Bin Zubeiry