STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, March 8, 2014

Wababe wa Azam wang'oka Kombe la Shirikisho


WABABE wa waliokuwa wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Azam timu ya Ferroviario de Beira imeondolewa kwenye michuano hiyo baada ya kunyukwa bao 1-0 na ZESCO ya Zambia katika mechi ya marudiano iliyochezwa leo jijini Lusaka.
Ferroviario iliiondosha Azam kwenye raudni ya awali kwa kuilaza jumla ya mabao 2-1 baada ya awali kulala 1-0 nyumbani Tanzania na kwenda kushinda kwao 2-0, ilishindwa kuhimili vishindo vya Wazambia ambao katika mechi ya awali ugenini ililazimisha sare.
Katika mechi nyingine za michuano hiyo zilizochezwa leo, Etoile du Sahel imepata ushindi mnono nyumbani kwa kuicharaz a CARA Brazzaville kwa maba0 3-0 na kufuzu kwa jumla ya mabao 3-1 kwani mechi iliyopita walilala ugenini bao 1-0 mjini Brazzaville Congo.
Nayo timu ya ASEC Memosa ya Ivory Coast, imepenya raundi ya pili baada ya kulazimishwa sare nyumbani na COB ya Mali lakini ikifaidika na ushindi wa mabao 2-0 iliyopata ugenini wiki iliyopita, huku How Mine ya Zimbabwe ikiing'oa St Michel United ya Sychelles kwa jumla ya mabao 6-4 baada ya leo kulala ugenini mabao 3-1 kwa Washelisheli hao, ila katika mechi yao iliyoipita walishinda nyumbani mabao 5-1.
AS Kigali nayo ilipenya hatua ya pili baada ya kuingoa Al Ahly Shendi ya Sudan Kusini kwa mikwaju ya penati baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 ugenini wiki moja baada ya kushinda ushindi kama huo nyumbani.
Timu ya  Bayesla United ya Nigeria ilifuzu hatua inayofuata baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Kondzo ya Kongo ambao walitoka nao suluhu ya kutofunga katika mechi yao wiki iliyopita.
Katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika zilizochezwa leo mbali na mechi tuliyoripoti mapema kati ya KCCA na Nkana, timu ya Kaizer Chiefs ya Agfrioka Kusini ilifuzu raundi ya pili kwa kishindo baada ya kuibutua Liga Maculmana ya Msumbiji kwa kuilaza mabao 3-0 na kufuzu kwa jumla ya mabao 7-0 baada ya wiki iliyopita kushinda nyumbani kwa mabao 4-0.
Nayo timu ya Leopards de Dolisie ya  Kongo imeingoa 1st de Agosto ya Angola kwa jumla ya mabao 4-3 baada ya leo kukubali kipigop ugenini mjini Luanda cha mabao 2-00 lakini ikibebwa na ushindi mnono iliypata nyumbani kwao wiki iliyopita ilkipoifumua Waangola mabao 4-1.
Mabingwa wa zamani wa Afrika Enyimba ya Nigeria licha ya kushinda bao 1-0 ugenini dhidi ya Real Bamako imejikuta iking'oka mashindanoni baada ya mechi ya kwanza kulala nyumbani mabao 2-1 kwa wapinzani wao na kufanya matokeo kuwa 2-2 ila Bamako kunufaika na faida ya mabao ya ugenini.
Nao ES Setif ya Algeria kufuzu hatua ya pili baada ya kulazimisha suluhu ugenini dhidi ya ASFA-Yannenga ya Burkina Faso baada ya wiki iliyopita kupata ushindi mnono nyumbani wa mabao 5-0.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea kesho kwa michezio mingine kadhaa ya kuhitimisha mechi za marudiano na kufahamika timu zilizotinga hatua ya 16 Bora, ambapo moja ya mechi hizo itazikutanisha watetezi Al Ahly ya Misri dhidi ya Yanga ambayo ilishinda mechi ya kwanza nyumbani Tanzania kwa bao 1-0.
Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu itachezwa kwenye jiji la Alexandria, baada ya wenyeji kuhofia mashabiki wao wakorofi jijini Cairo ambao walichukizwa na kipigo ilichopewa timu yao ugenini na Yanga.

No comments:

Post a Comment