STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, January 28, 2014

Kumekucha Tamasha la Busara 2014


Picha wa tatu kulia,ni Mwenyekiti wa Bodi ya Sauti za Busara Promotions,Bwa.Simai Mohamed akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun,jijini dar kuhusiana na ujio wa tamasha la muziki la Sauti za Busara la 11 katika kusherehekea utamaduni na muziki wa Afrika.Bwa.Simai amefafanua kuwa mwaka huu tamasha hilo litafanyika kuanzia tarehe 13 mpaka februari 16 katika viwanja vya kihistoria vya Ngome Kongwe,Zanzibar.

Jumla ya Vikundi 32 vitafanya maonyesho jukwaani kwa asilimia 100 live.Bwa Simai amesema kuwa vikundi hivyo vimechaguliwa kutokana na maombi zaidi ya 560 na vinawakilisha nchi 19,ameongeza kuwa zaidi ya wasanii 200 watafika Zanzibar kufanya maonyesho ya muziki,wasanii hao wanatoka Afrika Mashariki,Afrika Kusini na Magharibi,maeneo ya mto Nile na pia kutoka Puerto Rico.

Kutoka Tanzania,Wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ni Jhikoman,Ashimba,Swahili Vibes,Hoko Roro,Seven Survivor,Abantu Mandingo,Segere Original na Kazimoto.

Pichani ni Mmoja wa wanamuziki watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo,aitwaye Jhiko Man pichani akipiga gitaa lake live ikiwa ni sehemu ya kionjo chake kwa Wanahabari waliofika kwenye mkutano huo uliofanyika mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun jijini Dar.

Mmoja wa wanamuziki watakaotumbuiza kwenye tamasha la Sauti za Busara,aitwaye Ashimba pichani nae akipiga gitaa lake live ikiwa ni sehemu ya kionjo chake kwa Wanahabari waliofika kwenye mkutano huo uliofanyika mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Southern Sun jijini Dar.
Kwa Tarifa mbalimbali za tamasha hilo tembelea www.busaramusic.org.

Yanga tayari kuitia adabu Coastal kwao


Yanga

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young Africans kesho itashuka dimbani kupambana na wenyeji Coastal Union katika muendelezo wa michezo ya VPL, mchezo utakaopigwa katika daimba la Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Young Africans ambayo imeshawasili jijini Tanga tangu jana leo imefanya mazoezi mepesi asubuhi majira ya saa 2 katika uwanja wa mkwakwani kujiandaa na mchezo huo wa kesho ambao ni muhimu kwa Young Africans kupata ushindi ili iweze kuendelea kukaa kileleni.
Kocha msaidizi wa Young Africans Charles Mkwasa amesema vijana wake wote fit kwa sasa baada ya kupata muda mzuri wa kupumzika kufuatia safari ndefu kutoka nchini Uturuki mwishoni mwa wiki kisha kubadirisha hali ya hewa, na kwa sasa anasema vijana wako vizuri.
Akiongelea mchezo wa kesho Mkwasa amesema anajua Coastal Union wana timu nzuri ambayo imekua ikitoa upinzani mkali kwa timu nyingi za Ligi Kuu lakini anaamini katika mchezo wa kesho jinsi walivyowaandaa vijana wake watafanya vizuri na kuwapa furaha washabiki, wapenzi na wanachama wake.
Hali ya kikosi ni nzuri hata mara baada ya mazoezi ya leo hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja, hivyo wachezaji wote 20 waliokuja jijini Tanga wapo tayari kwa mchezo huo wa kesho na kazi inabakia kwa benchi la ufundi kuchagua wamtumie nani katika mchezo huo.
Mechi itaaanza majira ya 10 kamili kwa saa za Afrika Mashariki .
Viingilio vya mchezo:
Jukwaa Kuu Tshs 15,000/=
Mzunguko Tshs 5,000/=
Young Africans

Kivumbi cha nusu fainali CHAN kesho Sauzi

zimbabwe warriors
Zimbabwe itaendeleza maajabu yake mbele ya Libya kesho?


CHAN 2014: Fixtures and Predictions for Rest of African Nations Championship
Nigeria watacheka kama hivi mbele ya Ghana kesho usiku?   
Libya team
Libya wataidhibiti Zimbabwe kesho katika nusu fainali ya kwanza?

Black Stars Ghana
Ghana wana kibarua kigumu mbele ya Nigeria kesho usiku watatokaje?

VUMBI la Nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi ya Ndani (CHAN) linatarajiwa kutimka kesho kwenye uwanja wa Free State, Bloemfontaine wakati timu nne zilizofuzu hatua hiyo zitakapopapatuana kuwania kutinga fainali.
Zimbabwe iliyoshangaza wengi kwenye michuano hiyo inayofanyika nchini Afrika Kusini, itashuka dimbani jioni kukwaruzana na Libya ikiwa na kumbukumbu ya kuikwanyua Mali kwenye mechi ya robo fainali bila kutarajiwa.
Mechi nyingine ambayo wengi walitamani kama ingekuwa ndiyo fainali za CHAN 2014 itazikutanisha timu za Nigeria na Ghana ambazo zimekuwa na ushindani katika soka la Afrika kwa miaka kadhaa.
Nigeria iliyopenya kimiujiza kwenye hatua hiyo baada ya kuwa imelala mabao 3-0 dakika 45 za kwanza na kisha kurejesha mabao hayo na kuibuka na ushindi kwenye muda wa nyongeza ndiyo inayopewa nafasi kubwa ya kuwa mabingwa wapya wa michuano hiyo kwa mwaka huu.
Hata hivyo Ghana iliyoitoa DR Congo kwenye hatua ya robo fainali siyo timu ya kubezwa kutokana na rekodi iliyonayo mpaka sasa kwenye michuano hiyo.
Kocha Mkuu wa Nigeria alinukuliwa kuwa walitambua tangu mapema kuwa timu yao ingesonga mbele licha ya kuanza kwa kipigo toka kwa Mali, ambayo imeshang'olewa katika michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya tatu sasa.
Mashabiki wa kandanda wana hamu kubwa ya kutaka kuona ni timu zipi zitakumbana katrika pambano la Fainali siku ya  Jumamosi ambapo hatimaye bingwa wa michuano hiyo atafahamika hadharani baada ya kumalizika ama dakika 90 au 120 na ikiwezekana penati.
Bingwa mtetezi wa michuano hiyo Tunisia waliolitwaa fainali za mwaka 2011 haikufanikiwa kupenya katika michuano ya mwaka huu na hivyo taji hilo kuwa halina mwenyewe mpaka sasa.

Kitimtim cha Ligi Kuu Bara kutimka kesho

Mbeya City watakaikabili Ruvu Shooting
'Vijana wa Oman' Coastal Union watakaoivaa Yanga kesho Mkwakwani
Yanga watakaokuwa wageni wa Wagosi wa Kaya
Azama watakaokuwa nyumbani Chamazi dhidi ya Mgambo

Ruvu Shooting wataweza kuizuilia Mbeya City Mabatini kesho?
Na Boniface Wambura LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,  itaendelea kesho kwa Coastal Union kuikaribisha Yanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga. Kiingilio katika mechi hiyo ni sh. 5,000 na sh. 15,000. Nayo Ruvu Shooting na Mbeya City zitapambana kwenye Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani kwa viingilio vya sh. 10,000 na sh. 5,000. Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Kagera Sugar na Mtibwa Sugar. Viingilio ni sh. 5,000 na sh. 3,000.
Azam itaumana na Rhino Rangers katika Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Mbagala. Viingilio ni sh. 10,000 na sh. 3,000.
Yanga SC ambao ndio mabingwa watetezi, wanaongoza Ligi Kuu kwa pointi zao, 31 wakifuatiwa na Azam Mbeya City zenye 30 kila moja baada ya timu zote kucheza mechi 14.

Wachezaji wasiopimwa Afya kuzuiwa kucheza Ligi Kuu



Na Boniface Wambura SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limesema kwamba kuanzia Machi 1, mwaka huu mchezaji ambaye hatakuwa amefanyiwa vipimo vya afya hataruhusiwa kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.   Taarifa ya TFF leo imesema kwamba, watatoa kwa madaktari wa klabu za Ligi Kuu fomu maalumu za vipimo kwa wachezaji na kila mchezaji atatakiwa kufanyiwa vipimo vyote kama ambavyo fomu imeelekeza. “Hakuna mchezaji atakayeruhusiwa kuendelea kucheza VPL au kuchezea timu za Taifa kama atakuwa hajafanya vipimo hivyo. Machi 1 mwaka huu ndiyo utakuwa mwisho wa kurejesha fomu za vipimo vya wachezaji,”imesema taarifa hiyo ya TFF chini ya rais wake Jamal Emil Malinzi. Aidha, Madakatri wote wa timu za Ligi Kuu kupitia klabu zao wanatakiwa kuwasilisha vyeti pamoja na wasifu wao (CV) TFF kufikia Februari 8 mwaka huu. TFF imesema wasifu na vyeti hivyo vinatakiwa ili kuwezesha Kamati ya Tiba ya TFF kuandaa mafunzo kwa wataalamu hao wa tiba kwa wachezaji.

Abdi Kassim aiokoa UiTM isilale Malaysia, atupia bao


KIUNGO wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Kassim 'Babi' aliisaidia timu yake ya UiTM ya Malaysia kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Johor baada ya kuifungia bao katika mechi ya Ligi Kuu ya nchi hiyo.
Akizungumza kutoka Malaysia kuwa pambano hilo lililokuwa la pili kwa timu yake katika ligi kuu ya Malaysia lilichezwa kwenye uwanja wa Mini UiTM , uliopo mji wa Shah Alam.
"Nashukuru tumeshuka tena dimbani na kufanikiwa kupata sare ya bao 1-1, bao la timu yetu ya UiTM nikiwa nimelifunga mimi, kwa kweli nasijikia furaha sana," alisema Babi.
Babi alisema pambano hilo lilikuwa kali na wapinzani wa Johor walionyesha walitaka kusawazisha makosa baada ya kuanza ligi hiyo Ijumaa iliyopita kwa kulazwa mabao 3-1 nyumbani kwao na  PDRM, lakini walifanikiwa kuwadhibiti na kuambulia pointi hiyo moja.
Kabla ya mechi hiyo, Babi aliishuhudia timu yake ikinyukwa mabao 3-2 katika mechi ya Kombe la FA dhidi ya PBDKT T-Team kabla ya kuanza vyema pambano la ligi kwa kuilaza Kuala Lumpur SPA kwa bao 1-0.
Kiungo huyo wa zamani wa timu za Mtibwa Sugar, Yanga, Azam, KMKM na DT Long ya Vietnam alisema timu yao inatarajiwa kushuka tena dimbani Ijumaa ijayo ya (Februari 7) kwa kuumana na kuumana na DRB-Hicom uwanja wa nyumbani kabla ya Februari 10 kuwafuata PBAPP na kucheza nao kwenye uwanja wa Bandaraya mjini Penang.

Msiba! MCD hatunaye, kuzikwa leo mjini Moshi

MCD enzi za uhai wake

ALIYEKUWA mwanamuziki mahiri wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta'  Soud Mohammed (MCD) amefariki usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya KCMC-Moshi.
Taarifa zilizopenyezwa na mmoja wa wasanii wa Twanga Pepeta usiku wa jana, Haji Ramadhani zinasema kuwa MCD alikuwa amelazwa hopsitalini hapo kwa kusumbuliwa na maradhi ambayo hata hivyo hajawekwa bayana.
Inaelzwa kuwa mwanamuziki huyo aliyewahi kuwa Bingwa kucheza Disko mkoa wa Kilimanjaro kabla ya kujitosa kwenye muziki wa bendi alifariji majira ya saa saa 2:30 usiku.
Enzi za uhai wake MCD aliwahi kuzipigia bendi ya Diamond Sound 'Wana Ikibinda Nkoy', Twanga Pepeta na hivi karibuni alihamia Mashujaa Band kabla ya kurejea Twanga ambapo aliondoka wiki kadhaa kuelekea kwao Kilimanjaro kujiuguza na kukutwa na mauti hayo.
MICHARAZO inatoa pole kwa wanafamilia, ndugu na jamaa za mwanamuziki huyo pamoja na kuwapa pole wana Twanga Pepeta na wadau wa muziki wa ujumla kwa msiba huo.
Mzishi ya msanii huyo yanatarajiwa kufanyika leo mchana mjini Moshi.
Mungu aiweke roho ya marehemu Mahali Pema Peponi. Ameeen

Mourinho aomba radhi kwa kumuuza Mata kwa Mashetani

Mourinho akiwa na Mata enzi wakiwa pamoja Chelsea
MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho ameomba msamaha kwa uamuzi wake wa kumuuza Juan Mata Manchester United na kuweka wazi kuwa "ulikuwa uamuzi mgumu" kumuacha kiungo huyo raia wa Hispania kujiunga na mahasimu wao hao wa Old Trafford.
Mata, 25, ameweka rekodi United ya uhamisho baada ya kujiunga nayo kwa paundi milioni 37 akitokea Chelsea, ambako alikuwa hana raha tangu kocha huyo wa kireno kutua Stanford Bridge..
Mourinho aliiambia BBC Radio 5  kuwa angelipenda kuendelea kuwa na Mata katika kikosi chake.
"Kuna uamuzi ambao kocha anatakiwa kuchukua, lakini kwangu mimi ulikuwa uamuzi mgumu. Ningependa kuwa naye katika kikosi changu," alisema Mourinho.
"Mata ni mfungaji mzuri, lakini kuwa na mchezaji katika hali kama hii ni ngumu. Alistahili hilo kwa Chelsea kumfungulia mlango [akapate nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza].
"Ninapenda watu kuwa na furaha. Naomba msamaha sikuweza kumfanya kuwa na furaha katika kikosi hiki - Nimeumia sana katika hilo, lakini ninajenga timu yangu kwa kumchezesha Oscar kama namba 10."
Pia Mourinho alisema pindi Mata atakaporejea Stamford Bridge akiwa na United atamhakikishia mapokezi mema kutoka kwa mashabiki wa Chelsea.
"Ni wa kipekee sana. Nadhani ni 'mchezaji ambaye atabaki kuwa rohoni mwa mashabiki' na pia katika kizazi hiki," aliongeza Mreno huyo.
"Nimekuwa naye kwa kipindi cha miezi sita tu na nilimpenda sana. Sasa chukulia kwa watu ambao wamekuwa naye kwa miaka mitatu. Atabaki kuwa katika historia ya klabu - ametwaa makombe muhimu na watu wanampenda.
"Siku moja atakuja hapa akiwa na jezi ya Manchester United na watu watamuonyesha upendo huo."