STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, January 28, 2014

Msiba! MCD hatunaye, kuzikwa leo mjini Moshi

MCD enzi za uhai wake

ALIYEKUWA mwanamuziki mahiri wa bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta'  Soud Mohammed (MCD) amefariki usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya KCMC-Moshi.
Taarifa zilizopenyezwa na mmoja wa wasanii wa Twanga Pepeta usiku wa jana, Haji Ramadhani zinasema kuwa MCD alikuwa amelazwa hopsitalini hapo kwa kusumbuliwa na maradhi ambayo hata hivyo hajawekwa bayana.
Inaelzwa kuwa mwanamuziki huyo aliyewahi kuwa Bingwa kucheza Disko mkoa wa Kilimanjaro kabla ya kujitosa kwenye muziki wa bendi alifariji majira ya saa saa 2:30 usiku.
Enzi za uhai wake MCD aliwahi kuzipigia bendi ya Diamond Sound 'Wana Ikibinda Nkoy', Twanga Pepeta na hivi karibuni alihamia Mashujaa Band kabla ya kurejea Twanga ambapo aliondoka wiki kadhaa kuelekea kwao Kilimanjaro kujiuguza na kukutwa na mauti hayo.
MICHARAZO inatoa pole kwa wanafamilia, ndugu na jamaa za mwanamuziki huyo pamoja na kuwapa pole wana Twanga Pepeta na wadau wa muziki wa ujumla kwa msiba huo.
Mzishi ya msanii huyo yanatarajiwa kufanyika leo mchana mjini Moshi.
Mungu aiweke roho ya marehemu Mahali Pema Peponi. Ameeen

No comments:

Post a Comment