STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, January 28, 2014

Mourinho aomba radhi kwa kumuuza Mata kwa Mashetani

Mourinho akiwa na Mata enzi wakiwa pamoja Chelsea
MENEJA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho ameomba msamaha kwa uamuzi wake wa kumuuza Juan Mata Manchester United na kuweka wazi kuwa "ulikuwa uamuzi mgumu" kumuacha kiungo huyo raia wa Hispania kujiunga na mahasimu wao hao wa Old Trafford.
Mata, 25, ameweka rekodi United ya uhamisho baada ya kujiunga nayo kwa paundi milioni 37 akitokea Chelsea, ambako alikuwa hana raha tangu kocha huyo wa kireno kutua Stanford Bridge..
Mourinho aliiambia BBC Radio 5  kuwa angelipenda kuendelea kuwa na Mata katika kikosi chake.
"Kuna uamuzi ambao kocha anatakiwa kuchukua, lakini kwangu mimi ulikuwa uamuzi mgumu. Ningependa kuwa naye katika kikosi changu," alisema Mourinho.
"Mata ni mfungaji mzuri, lakini kuwa na mchezaji katika hali kama hii ni ngumu. Alistahili hilo kwa Chelsea kumfungulia mlango [akapate nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza].
"Ninapenda watu kuwa na furaha. Naomba msamaha sikuweza kumfanya kuwa na furaha katika kikosi hiki - Nimeumia sana katika hilo, lakini ninajenga timu yangu kwa kumchezesha Oscar kama namba 10."
Pia Mourinho alisema pindi Mata atakaporejea Stamford Bridge akiwa na United atamhakikishia mapokezi mema kutoka kwa mashabiki wa Chelsea.
"Ni wa kipekee sana. Nadhani ni 'mchezaji ambaye atabaki kuwa rohoni mwa mashabiki' na pia katika kizazi hiki," aliongeza Mreno huyo.
"Nimekuwa naye kwa kipindi cha miezi sita tu na nilimpenda sana. Sasa chukulia kwa watu ambao wamekuwa naye kwa miaka mitatu. Atabaki kuwa katika historia ya klabu - ametwaa makombe muhimu na watu wanampenda.
"Siku moja atakuja hapa akiwa na jezi ya Manchester United na watu watamuonyesha upendo huo." 

No comments:

Post a Comment