STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, January 28, 2014

Kivumbi cha nusu fainali CHAN kesho Sauzi

zimbabwe warriors
Zimbabwe itaendeleza maajabu yake mbele ya Libya kesho?


CHAN 2014: Fixtures and Predictions for Rest of African Nations Championship
Nigeria watacheka kama hivi mbele ya Ghana kesho usiku?   
Libya team
Libya wataidhibiti Zimbabwe kesho katika nusu fainali ya kwanza?

Black Stars Ghana
Ghana wana kibarua kigumu mbele ya Nigeria kesho usiku watatokaje?

VUMBI la Nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ligi ya Ndani (CHAN) linatarajiwa kutimka kesho kwenye uwanja wa Free State, Bloemfontaine wakati timu nne zilizofuzu hatua hiyo zitakapopapatuana kuwania kutinga fainali.
Zimbabwe iliyoshangaza wengi kwenye michuano hiyo inayofanyika nchini Afrika Kusini, itashuka dimbani jioni kukwaruzana na Libya ikiwa na kumbukumbu ya kuikwanyua Mali kwenye mechi ya robo fainali bila kutarajiwa.
Mechi nyingine ambayo wengi walitamani kama ingekuwa ndiyo fainali za CHAN 2014 itazikutanisha timu za Nigeria na Ghana ambazo zimekuwa na ushindani katika soka la Afrika kwa miaka kadhaa.
Nigeria iliyopenya kimiujiza kwenye hatua hiyo baada ya kuwa imelala mabao 3-0 dakika 45 za kwanza na kisha kurejesha mabao hayo na kuibuka na ushindi kwenye muda wa nyongeza ndiyo inayopewa nafasi kubwa ya kuwa mabingwa wapya wa michuano hiyo kwa mwaka huu.
Hata hivyo Ghana iliyoitoa DR Congo kwenye hatua ya robo fainali siyo timu ya kubezwa kutokana na rekodi iliyonayo mpaka sasa kwenye michuano hiyo.
Kocha Mkuu wa Nigeria alinukuliwa kuwa walitambua tangu mapema kuwa timu yao ingesonga mbele licha ya kuanza kwa kipigo toka kwa Mali, ambayo imeshang'olewa katika michuano hiyo inayofanyika kwa mara ya tatu sasa.
Mashabiki wa kandanda wana hamu kubwa ya kutaka kuona ni timu zipi zitakumbana katrika pambano la Fainali siku ya  Jumamosi ambapo hatimaye bingwa wa michuano hiyo atafahamika hadharani baada ya kumalizika ama dakika 90 au 120 na ikiwezekana penati.
Bingwa mtetezi wa michuano hiyo Tunisia waliolitwaa fainali za mwaka 2011 haikufanikiwa kupenya katika michuano ya mwaka huu na hivyo taji hilo kuwa halina mwenyewe mpaka sasa.

No comments:

Post a Comment