STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, January 28, 2014

Yanga tayari kuitia adabu Coastal kwao


Yanga

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young Africans kesho itashuka dimbani kupambana na wenyeji Coastal Union katika muendelezo wa michezo ya VPL, mchezo utakaopigwa katika daimba la Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Young Africans ambayo imeshawasili jijini Tanga tangu jana leo imefanya mazoezi mepesi asubuhi majira ya saa 2 katika uwanja wa mkwakwani kujiandaa na mchezo huo wa kesho ambao ni muhimu kwa Young Africans kupata ushindi ili iweze kuendelea kukaa kileleni.
Kocha msaidizi wa Young Africans Charles Mkwasa amesema vijana wake wote fit kwa sasa baada ya kupata muda mzuri wa kupumzika kufuatia safari ndefu kutoka nchini Uturuki mwishoni mwa wiki kisha kubadirisha hali ya hewa, na kwa sasa anasema vijana wako vizuri.
Akiongelea mchezo wa kesho Mkwasa amesema anajua Coastal Union wana timu nzuri ambayo imekua ikitoa upinzani mkali kwa timu nyingi za Ligi Kuu lakini anaamini katika mchezo wa kesho jinsi walivyowaandaa vijana wake watafanya vizuri na kuwapa furaha washabiki, wapenzi na wanachama wake.
Hali ya kikosi ni nzuri hata mara baada ya mazoezi ya leo hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja, hivyo wachezaji wote 20 waliokuja jijini Tanga wapo tayari kwa mchezo huo wa kesho na kazi inabakia kwa benchi la ufundi kuchagua wamtumie nani katika mchezo huo.
Mechi itaaanza majira ya 10 kamili kwa saa za Afrika Mashariki .
Viingilio vya mchezo:
Jukwaa Kuu Tshs 15,000/=
Mzunguko Tshs 5,000/=
Young Africans

No comments:

Post a Comment