STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, June 12, 2015

Stars kuwafuata Mafarao kindava, Nooij atamba

Watatukoma Jumapili

Stars wakijifua Addis Ababa
TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajiwa kupaa usiku wa leo kutoka Ethiopia kuelekea Misri tayari kwa pambano lao la Jumapili dhidi ya Mafarao.
Stars imeweka kambi ya mazoezi takribani kwa wiki moja jijini Addis Ababa na jana ilifanya mazoezi ya asubuhi kuu kabla ya usiku wa leo kupaa kwenda Cairo na baadaye Alexandria watakapoumana na wenyeji wao.
Kocha mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij amesema, anashukuru maendeleo ya kambi ni mazuri timu yake inafanya mazoezi katika viwanja viwili vizuri vilivyopo Addis Ababa, uwanja wa Taifa na  uwanja wa Benki ya Biashara ya Ethiopia.

Nooij amesema amekuwa akiwafundisha wachezaji wake kucheza mpira wa kasi na pasi za haraka haraka, jambo ambalo wachezaji wameonyesha kufuata vizuri maelekezo yake na kusema wanamuelewa vizuri.

Akiongelea mchezo dhidi ya Misri siku ya jumapili, Nooij amesema timu inakwenda kupambana kusaka matokeo mazuri katika mchezo, nafahamu tunaenda cheza ugenini, nimewaelekeza vijana wangu wanaocheza nafasi ya ushambuliaji kutumia vizuri nafasi tutakazozipata katika mchezo huo.

Aidha kocha Nooij amesema katika mpira hakuna kinachoshindikana, kambi ya wiki moja Addis Ababa imewasaidia wachezaji kukaa pamoja na kushika maelekezo yake vizuri, hivyo anaamini timu yake itafanya vizuri katika mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON.

Katika kikosi cha wachezaji wa 22 waliopo kambini jijini Addis Ababa hakuna mchezaji majeruhi, wachezaji wote wako vizuri kiafya, kifikra na morali ni ya hali ya juu kuelekea kwenye mchezo huo dhidi ya Mafarao.
Taifa Stars inatarajia kuondoka usiku wa leo Ijumaa kuelekea nchini Misri kwa shirika la ndege la Ethiopia majira ya saa 5 usiku na kufika Cairo majira ya saa 8 usiku, kisha kuunganisha safari ya kuelekea jijini Alexandria ambapo timu mchezo huo utakapofanyika.

Mchezo kati ya Misri dhidi ya Tanzania utachezwa katika uwanja wa Borg El Arab kuanzia majira ya saa 1 jioni kwa saaa za huku, sawa na saa 2 kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Waamuzi wa mchezo huo wanatokea nchini Ethiopia ambapo ni Bamlak Tessema Weyesa (mwamuzi wa kati), Kinfe Yilma (mwamuzi msaidizi wa kwanza), na Wolday Hailerague (mwamuzi msaidizi wa pili).

Hawa ndio waliotemwa katika Klabu za Ligi Kuu ya England

Darren Bent

Didier Drogba

Brad Friedel
Abou Diaby
WAKATI klabu za Tanzania zikiendelea kuendesha mambo kizamani kwa kushindwa kuanika hadharani orodha ya wachezaji inayowatema ili kuwapa fursa wachezaji hao kusaka malisho mapya, wenzetu England klabu zao zimeshatoa orodha ya iliyowatema.
Miongoni mwa wachezaji walitangazwa kutemwa na kuanza msako wa kusaka cjaka jipya la kuvuna mihela ni Kiungo wa Arsenal, Abou Diaby Darren Bent wa Aston Villa na Didier Drogba aliyeamua kujiondoa mapema Chelsea.
MICHARAZO imekuwekea orodha kamili ya wachezaji waliotemwa katika klabu za England baada ya kufungwa kwa msimu wa 2014-2015. Jisomee mwenyewe majina hayo;

Arsenal

Abou Diaby, Jack Jebb, Oluwasemilogo Adesewo Ajayi, Austin Lipman, Ryo Miyaichi, Brandon Ormonde-Ottewill, Josh Vickers

Aston Villa
Darren Bent, Graham Burke, Alfie Crooks, Christopher Herd, Craig Hill, Bradley Lewis, Isaac Nehemie, Daniel O’Brien, Enda Stevens, Thomas Strain, Ron Vlaar, Courtney Wildin

Burnley
Cameron Howieson, Steven Reid, Ross Wallace

Chelsea
Didier Drogba

Crystal Palace
Foluwashola Ameobi, Michael Chambers, Kyle De Silva, Stephen Dobbie, Owen Garvan, Brede Hangeland, Lewis Price, Peter Ramage, Ghassimu Sow, Jerome Thomas

Everton

Antolin Alcaraz, Sylvain Distin, George Green, Curtis Langton, John Lundstram, Ben McLaughlin

Hull City
Joseph Cracknell, Leon Dawson, Joseph Dudgeon, Maynor Figueroa, Stephen Harper, John Mahon, Jonathan Margetts, Eoghan McCawl, Paul McShane, Mark Oxley, Liam Rosenior, Yannick Sagbo, Sam Topliss

Leicester City

Zoumana Bakayogo, Marcel Barrington, Adam Dawson, Paul Gallagher, Kieran Kennedy, Conrad Logan, Herve Pepe-Ngoma, Louis Rowley, Gary Taylor-Fletcher, Matthew Upson

Liverpool

Steven Gerrard, Glen Johnson, Brad Jones, Jordan Lussey, Marc Pelosi

Manchester City
Adam Drury, John Guidetti, Frank Lampard, Greg Leigh, Dominic Oduro, Micah Richards

Manchester United

Ben Amos, Tom Cleverley, Callum Evans, Ryan McConnell, Thomas Thorpe

Newcastle United

Jak Alnwick, Adam Campbell, Jonas Gutierrez, Remie Streete, Ryan Taylor

Queens Park Rangers

Bruno Andrade, Joey Barton, Richard Dunne, Rio Ferdinand, Jordan Gibbons, Karl Henry, Aaron Lennox, Brian Murphy, Jamie Sendles-White, Shaun Wright-Phillips, Bobby Zamora

Southampton

Artur Boruc, Cody Cropper, Jos Hooiveld, Christopher Johns, Omar Rowe, Jake Sinclair

Stoke City

Oluwatomisin Adeloye, James Alabi, Samuel Coulson, Alexander Grant, Wilson Palacios, Robbie Parry, Nathan Ricketts-Hopkinson, Thomas Sorensen, Adam Thomas, Charlie Ward, Elliot Wheeler, Andrew Wilkinson

Sunderland

Wes Brown, Peter Burke, Andrew Cartright, Joel Dixon, Thomas McNamee, Anthony Reveillere

Swansea City
Thomas Atyeo, David Cornell, Ruaridhri Donnelly, Corey Francis, Giancarlo Gallifuoco, Joseph Jones, Kurtis March, Curtis Obeng, Gareth Owen, Scott Tancock, Alan Tate, Gerhard Tremmel

Tottenham Hotspur
Jordan Archer, Cristian Ceballos, Brad Friedel, Bongani Khumalo, Aaron McEneff, Alexander McQueen, Jonathan Miles

West Bromwich Albion
Wesley Atkinson, Chris Baird, Aaron Birch, Jason Davidson, Bradley Garmston, Alexander Jones, Gareth McAuley, Youssouf Mulumbu, Mani O’Sullivan

West Ham

Kieran Bywater, Carlton Cole, Anderson De Carvalho, Guy Demel, Jussi Jaaskelainen, Sean Maguire, Paul McCallum, Daniel Potts

Chile waanza vema Copa America, Cavani alikoroga

Cavani
WAKATI wenyeji wa michuano ya Kombe la Copa America, Chile wakianza vema michuano hiyo, mshambuliahji wa Kimataifa wa Uruguay na klabu ya Paris Saint-Germain, Edinson Canavi ameomba radhi baada ya kudai kuwa Jamaica ni ngumu kupambana nayo kama zilivyo timu zote za Afrika. 
Nyota huyo wa zamani wa Napoli alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo wao wa kesho Jumamosi dhidi nchi hiyo inayotoka upande wa mataifa ya Caribbean. 
Kauli hiyo ambayo wengi waliichukulia kama ya kibaguzi ilimfanya Cavani kuomba radhi haraka katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akidai alikuwa akifananisha aina ya uchezaji wa Jamaica na baadhi ya timu za Afrika na sio vinginevyo kama watu wanavyotafsiri. 
Nyota huyo aliomba radhi kwa watu wa Jamaica kwa kauli yake hiyo kueleweka vibaya na alikuwa hana nia yeyote mbaya. 
Uruguay ambao ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo wanatarajiwa kutupa karata yao ya kwanza katika michuano hiyo kesho wakichuana na Jamaica.
http://www.panamericanworld.com/sites/default/files/gm1e9970pi201142956718.jpg
Chile

Katika hatua nyingine Kocha wa timu ya taifa ya Chile, Jorge Sampaoli amekiri kuwa pamoja na magumu waliyokuwa nayo katika mchezo wao ufunguzi wa kundi A wa michuano ya Copa America dhidi ya Ecuador lakini anadhani walistahili ushindi wa mabao 2-0 waliopata. 
Mabao ya kipindi cha pili kutoka kwa Arturo Vidal na Eduardo Vargas yaliisaidia Chile kupata ushindi huo muhimu ingawa Sampaoli anadhani bado wanahitaji kuimarika zaidi kama wanataka kushinda taji la michuano hiyo wakiwa kama wenyeji. 
Akihojiwa kocha huyo amesema waliweka mipango yao kama walivyofanya katika mchezo dhidi ya Brazil, ambapo ilikwenda vyema katika kipindi cha kwanza lakini walihangaika kipindi cha pili baada ya kushindwa kufunga. 
Kocha huyo aliendelea kudai kuwa Ecuador waliwapa wakati mgumu kwani nao walikuwa wakishambulia kwa kasi hivyo ni wazi wanapaswa kujiandaa zaidi kwa michezo ijayo ili waweze kufika mbali. 
Chile itakwaana na Mexico Juni 15 katika mchezo wao wa pili wa hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Utani wamtokea puani Mkurugenzi wa Mawasiliano FIFA, atimuliwa

UTANI wakati mwingine mbaya sana! Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Walter De Gregorio ametimuliwa baada ya kutoa kauli ya utani kuhusu shirikisho hilo katika kituo kimoja cha runinga cha huko Uswisi. 
Katika kipindi kimoja maarufu cha mahojiano nchini humo, Gregorio alitania kuwa Rais wa FIFA, Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Mawasiliano wote wanasafiri katika gari moja ambalo linaendeshwa na Polisi. 
Mara baada ya kauli hiyo FIFA ilitoa taarifa baadae kuwa De Gregorio ameamua kujiuzulu wadhifa wake huo, lakini wapekuzi wa mambo wanadai kuwa alitimuliwa na Rais wa FIFA Sepp Blatter. 
Blatter mwenyewe mapema mwezi huu alitangaza kujiuzulu pindi utakapofanyika uchaguzi mpya wa nafasi yake hiyo, ikiwa zimepita siku nne toka ateuliwe kuliongoza shirikisho hilo kea muhula wa tano. Shirikisho hilo lipo katika tuhuma nzito za ufisadi na vitendo vya rushwa vilivyosababisha maafisa wake kadhaa kutiwa mbaroni siku chache kabla ya uchaguzi uliomrejesha Blatter madarakani.

Nani kasema eti Messi na Ronaldo ni mahasimu?!

MSIKIE Leonel Messi anavyosema baada ya kuzuka kwa taarifa kwamba ni hasimu mkubwa na Cristiano Ronaldo. Mshambuliaji huyo nyota wa Barcelona na Argentina, amesisitiza kuwa hana uhasama wowote na nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo. Wawili hao wanahesabiwa kama wachezaji bora kabisa duniani kwasasa wakiwa wameshinda tuzo saba za Ballon d’Or zilizopita kati yao. Ronaldo ambaye ndio alionyakuwa tuzo mbili za mwisho na kuwafanya wadau wa soka kudai kuwa mafanikio ya nyota huyo wa kimataifa wa Ureno ndio yaliyomhamasisha Messi naye kucheza kwa kiwango cha juu msimu huu. 
Hata hivyo, Messi amesisitiza kuwa haathiriki na kitu chochote ambacho Ronaldo anakifanya ndani na nje ya uwanja. 
Messi amesema hakuna wala hakujawahi tokea uhasama wowote kati yao kwani jambo hilo limetengenezwa na vyombo vya habari zaidi kuliko uhalisia na kusisitiza kila mtu anajisikia vema kwa mwenzake.

Liverpool Jeuri! Yaigomea Man City kwa Raheem Sterling

KLABU ya Liverpool jeuri sana! Imeamua kuikataa ofa ya Pauni Milioni 25 iliyotolewa na klabu ya Manchester City inayomtaka mshambuliaji wake Raheem Sterling. Liverpool wanamthaminisha nyota huyo wa Kimataifa wa England ambaye pia anahusisha na tetesi za kutakiwa Arsenal na Real Madrid, kufikia Pauni Milioni 50. Sterling mwenye umri wa miaka 20 alijiunga na Liverpool akitokea Queens Park Rangers mwaka 2010 na yuko chini ya mkataba mpaka mwaka 2017. Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers alisema mwezi uliopita kuwa anamtegemea nyota huyo kubakia Anfield mpaka mkataba wake utakapokwisha baada ua kukataa kusaini mkataba mpya ambao ungemuwezesha kulipwa kitita cha Paundi 100,000 kwa wiki.

Lisome Tamko la Viongozi wa Wanachuo wa KIU

Wanachuo wa KIU Tanzania wakiwa katika maandamano hayo ya hivi karibuni


WANAFUNZI WA KITIVO CHA SAYANSI YA TIBA CHUO KIKUU CHA KIMATAIFA CHA KAMPALA, GONGO LA MBOTO DAR ES SALAAM

Kutokana   na matatizo mbalimbali ya chuo kikuu kishiriki cha Kampala, ambayo yamesababisha kuwa na migomo ya mara kwa mara katika kitivo cha afya. Na yamefikishwa katika ngazi mbalimbali za uongozi wa serikali ikiwemo wizara ya Elimu, wizara ya Afya na Bunge.
   
        MATATIZO:
Chuo chetu kinakabiliwa na matatizo mengi ambayo kwa namna moja au nyingine yanarudisha nyuma maendeleo ya wanafunzi kimasomo, matatizo hayo ni kama ifuatavyo;
1.      Kutokusajiliwa kwa kada zote za afya katika bodi husika za afya nchini ( ambazo zinatolewa chuoni hapa.
Kada ya udaktari, ufamasia na maabara hazina usajili wa bodi husika zinazosimamia taaluma hizo zikiwemo pharmacy council, Tanganyika medical association na medical laboratory council na NACTE (kwa wanafunzi wa diploma na certificate). Kutosajiliwa kwa kada hizo kunapelekea wanafunzi wanaohitimu chuoni hapo kutotambulika hivyo kupelekea kukosa ajira.
2.      Kusimamishwa masomo kwa wanafunzi 5 bila sababu za msingi na kupewa kesi ambazo    hawajasifanya
3.      Kiwango kikubwa cha ada(tuition fee)
Kikao cha tarehe 13/11/2014 kilichofanyika wizara ya elimu kilitoa mapendekezo ya kupunguza ada kwa chuo cha kampala lakini hakuna utekelezaji mpaka sasa. Kwa mfano kwa mwaka wa masomo 2013/2014 wanafunzi wa kada ya ufamasia wa ngazi ya shahada wanalipa tsh 5,400,000/=. Wakati wale wa mwaka wa masomo 2014/2015 wanalipa ada kiasi cha tsh 3,800,000/=. Kwa wanafunzi wa kada ya udaktari ngazi ya shahada mwaka wa masomo 2013/2014 wanalipa tsh 9,900,000/=. Wakati wa mwaka wa masomo 2014/2015 wanalipa kiasi cha tsh 6,700,000/=. Kwa wanafunzi wa stashahada ya udaktari,famasi na maabara wanalipa kiasi cha tsh 1,900,000/=.
4.      Mtaala wa kufundishia(curriculum).
Chuo chetu kinatumia mtaala tofauti na ule wa Tanzania(wa Uganda) ambao unawapa ugumu baraza husika kukisajili chuo chetu. Mtaala huo pia unawapa kazi sana wanafunzi katika kufuatilia na kuyaelewa yale wanayofundishwa kwan umebeba masomo mengi kwa muhula mmoja kwa mfano wanafunzi wa shahada ya ufamasia wanasoma masomo 11 kwa muhula mmoja katika chuo chetu wakati ni tofauti ukilinganisha na vyuo vingine ambavyo kwa muhula mmoja wanasoma masomo 4 hadi 5. Kwa wanafunzi wa stashahada wanasoma hadi masomo 15 kwa muhula mmoja ambayo kwa hali ya kawaida huwezi kuyamudu kwa wakati.
5.      Utaratibu wa supplementary.
Supplementary zinafanyika kila baada ya muhula wa masomo na kwa kila somo mwanafunzi anawajibika kulipia tsh 40,000/= wakati ukilinganisha na vyuo vingine supplementary zinafanyika mwisho wa mwaka wa masomo na mwanafunzi halipii kabisa au kuchanga kiasi kidogo sana kwa ajili ya mitihani hiyo. Pia mwanafunzi anawajibika kurudia muhula endapo atafeli mtihani wake wa supplementary hata kama ni somo moja tu na atalazimika kurudia masomo yote hata yale ambayo alifaulu vizuri.


6.      Uongozi mbovu wa kitivo cha sayansi ya afya(health science).
Uongozi wetu hauna mfumo unaoeleweka wa utoaji matokeo ambapo katika mtihani mmoja mwanafunzi anapokea matokeo yake mara tatu tofauti. Kutokuonekana kabisa kwa matokeo ya baadhi ya wanafunzi hii inachangiwa pia na mfumo wa utoaji matokeo hayo ambapo mpaka leo hii wanafunzi wa chuo wanabandikiwa matokeo ubaoni kama wanafunzi wa shule ya msingi. Pia uongozi hauna mazoea wala utaratibu wa kumsikiliza mwanafunzi.
7.      Uhaba wa miundombinu ya chuo.
Chuo chetu kinakabiliwa na uhaba mkubwa wa vifaa vya ufundishaji na ujifunzaji hasa maabara, vingine ni kama projector na microphone ambapo utakuta darasa la watu zaidi ya 100 halina microphone na kuoelekea baadhi ya wanafunzi kuhudhuria darasani bila kupata chochote kutokana na kutokumsikia kabisa mwalimu. Pia Chuo hakina usafiri wa uhakika kwa ajili ya medical rotation na research mbalimbali.
8.      Ada ya TCU.
Chuo chetu kina utaratibu wa kuwaibia wanafunzi wa stashahada na astashahada kwa kuwalipisha kiasi cha tsh 20,000/= kama ada ya usajili wa TCU wakati TCU wala hawahusiki na wanafunzi hao.huu ni wizi wa dhahiri kwani hizo fedha wanalipa kupitia account ya chuo na sio TCU.
9.      Ukosefu wa uwiano kati ya wafanyakazi wa chuo.
95% ya wafanyakazi wa chuo chetu ni wageni na sio watanzania hivyo kupelekea hata matatizo yetu kutopata suluhu na uangalizi wa karibu kwani wengi wa wafanyakazi hao hawajali hali halisi ya watanzania.
10.  Pesa maalumu kwa ajili ya kada mbalimbali(special faculty requirement).
Kutokana na majibu yaliyotolewa katika kikao kilichofanyika tarehe 04/05/2015 kati ya uongozi wa chuo na bodi ya mikopo ya elimu ya juu(HESLB) imeelezwa kwamba chuo chetu kinakosa fedha hizo kutokana na kukosa usajili wa kudumu.
11.  Masomo ya pre entry(MPP)
Chuo chetu kina utaratibu mbovu wa kuwafundisha masomo ya sekondari wanafunzi wa shahada wanaochaguliwa chuoni hapa na masomo hayo hufundishwa kwa muhula mzima na kupelekea kuongezeka muda wa kuhitimu masomo yao huku wakilipa ada ile ile. Hai hii hupelekea wanafunzi kuwa na muda mfupi wa likizo kwa ajili ya recessive semester ambayo wanafidia muda waliosoma masomo ya sekondari(MPP) badala ya course husika.
12.  Muda wa kuhitimu masomo``
Wanafunzi wa shahada wameongezewa muda wa kukaa chuoni hii ni kutokana na urasimu wa chuo na uwepo wa masomo ya pre entry au MPP ambapo mwanafunzi wa kada ya maabara anatakiwa kusoma kwa miaka 4.5 badala ya miaka 3 na kada za udaktari na ufamasia wameongezewa miezi 6 ambapo madaktari wanasoma miaka 5.5 badala ya miaka 5 na wafamasia wanasoma miaka 4.5 badala ya miaka 4 kitu ambacho ni kinyume kabisa na utaratibu wa elimu ya Tanzania.
13.  BRIDGING COURSE NA UDAHILI WA WANAFUNZI KINYUME NA UTARATIBU.
Kumekua na udahili wa moja kwa moja wa wanafunzi wasio kua na vigezo katika chuo hiki kinyume na utaratibu,wakifundishwa masomo ya bridging course ambayo ni kinyume cha sheria,ambayo pia haipo chuo chochote Tanzania na ilikua ni moja ya sababu zilizo pelekea chuo cha tiba cha IMTU mwaka 2014 kufungiwa.  Je,serikali inakiwajibisha vipi chuo hiki ambacho kinakwenda kinyume na taratibu hizo pamoja na wanafunzi ambao wizara imethibitisha mbele ya waziri kua haitawasajili,chuo kinawafidia vipi wanafunzi hao?
14.  Ukosefu wa prospectus na university calendar,
Chuo hakina prospectus wala university calendar  inayowaongoza wanafunzi na wafanyakazi kwa ujumla na kuwaonyesha ratiba na  matukio ya mwaka mzima.
15.  Kudahiliwa katika chuo cha nje ya nchi wakati tumeomba kama wanafunzi wa ndani ya nchi na tunapata mkopo tukitambulika kama wanafunzi wa ndani ya nchi, hii inatuletea shida ya kutambulika kama wanafunzi wa kigeni na kutakiwa ku verify vyeti vyetu kabla ya kuajiriwa nchini kwetu tofauti na vyuo vingine vilivyopo nchini  ambavyo vipo chini ya TCU.

 MAJIBU YA WAZIRI WA ELIMU MUHESHIMIWA SHUKURU KAWAMBWA
Baada ya wanafunzi wa kitivo cha sayansi ya tiba katika chuo kikuu kishiriki cha Kampala kukumbwa na matatizo mbalilmbali ambayo yameshindwa kutatuliwa katika ngazi mbalilmbali mpaka pale yalipofikishwa katika bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania na kuundwa kamati ili kuweza kushugulikiwa  matatizo hayo .
 kamati ilipewa muda wa wiki moja kuweza kukamilishwa kwa kazi hiyo tarehe 4 mwezi huu wa sita  leo  hii ni wiki moja imepita na kamati hii haijafika.
Lakini cha kushangaza tulipata ugeni jana tarehe 10/06/2015 Mh Shukuru Kawambwa waziri wa elimu nchini ambapo alipanga kuonana na uongozi wa chuo pamoja na serikali ya wanafunzi bila kuwaona wanafunzi wenye matatizo husika, ambapo baada ya wanafunzi hao kugundua walimuomba waweze kuongea nae kuhusu matatizo hayo ambayo yameshindwa kupatiwa ufumbuzi kwa miaka mingi sasa  na muda huo wanafunzi wote wa kitivo cha sayansi ya afya chuoni hapa tulisimamishwa masomo kwa siku zisizojulikana kuanzia tarehe 8/06/2015.Na muheshimiwa waziri alipanga kujibu matatizo ya chuo hicho yasiyopungua 15 kwa muda wa dakika 30 akiwa anadai kwamba anawai ndege kwa ajili ya safari ya saa 12 jioni.
N.B: kuja kwa waziri hakujatatua tatizo lolote bali kumeongeza matatizo kwa sababu tarehe 1/06/2015 alikiri mbele ya bunge kuwa matatizo ya chuo kikuu cha kampala hayawezi kutatuliwa na serikali yake.
       MAJIBU YA WAZIRI KUHUSU MATATIZO HAYO.
1;KUHUSU USAJILI
Waziri alikili wazi kwamba chuo kimesajiliwa kama chuo cha nje na Tume ya vyuo vikuu Tanzania(T.C.U) Na kudai kwamba vyuo kama hivyo nchini vipo ambapo alipata kutolea mfano wa vyuo kama vile Jommo Kenyata university,Aga khan university bila kujali kwamba vyuo hivyo havipo katika orodha ya vyuo vinavyotambulika na Tume ya vyuo vikuu nchini Tanzania(T.C.U) .
     Hoja za Wanafunzi katika hili jibu ni kama ifuatavyo.
Sisi kama Watanzania halali wa nchi yetu tunashangazwa na majibu hayo maana sisi tumeomba kama wanafunzi wa ndani katika vyuo vitano tulivyopaswa kuomba na kupangiwa masomo hayo na Tume ya vyuo vikuu Tanzania katika chuo hiki cha Kampala international university  ambacho hakifuati kanuni na taratibu za nchi yetu ya Tanzania.
        Lakini hoja iliyokuwa kubwa zaidi hiki kama ni chuo kilichopata usajili kama chuo cha nje ni kwa nini basi wanafunzi tunapata mikopo ya serikali kama vyuo vya ndani wakati hii ni kinyume maana mikopo hutolewa kwa wanafunzi wa ndani tuu na isiwe scholarship kama ilivyo kwa wale wanaosoma nje za nchi.Ambapo hata hivyo vyuo alivyotolea mfano mheshimiwa waziri havitambuliki na tume ya vyuo vikuu nchini (T.C.U) pamoja na bodi ya mikopo ya Elimu ya juu nchini(H.E.S.L.B)
           Hata hivyo elimu inayotolewa katika chuo hiki cha kimataifa hakiendani na vyuo vingine vya kimataifa na hata vya ndani na sisi wanafunzi wa chuo hiki imepelekea kudharaulika na kuwa na uwasiwasi na soko la ajira hapo baadae endapo tutamaliza salama katika chuo hiki ambacho wanafunzi wadai haki tena kwa njia ya amani hunyanyaswa kwa kusimamishwa masomo ,kupelekwa lumande na kusingiziwa kesi mbalimbali ili waweze kukwamishwa katika masomo yao.
     2; MITAALA YA CHUO HIKI.
Majibu ya waziri huyo mwenye dhamana ya elimu nchini yameonesha wazi kwamba mitaala hiyo imepitishwa na jopo wataalam  maprofesor wengi kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam(U.D.S.M) na kupitishwa na tume ya vyuo vikuu nchini(T.C.U)
  Na mheshimiwa waziri alipata kuongeza wazi kwa kusema kwamba bodi za afya yaani ile ya famasia,mahabara na udaktari haziusiki na mambo ya mitaala bali ni T.C.U peke yake ndio inahusika.
     Hoja za wanafunzi kuhusu jibu hili
Sote tunajua wazi kwamba chuo kikuu cha Dar es salaam hakina kozi za afya sasa bado tunakosa  imani na waziri maana haiwezekani mitaala hii kutungwa na watu wenye fani tofauti na zile za afya hata wawe maprofesor gani maana hii kazi inabeba maisha ya watu hivyo basi tunaomba bodi husika kupitisha mtaala huu.
Pia tukirejea barua kutoka baraza la famasia iliyotumwa katika chuo hiki yenye Kumbukumbu namba  AB/300/312/02/20,ya tarehe 14/04/2015 inaeleza moja ya matatizo ambayo yanafanya chuo hiki kutosajiliwa ni pamoja na mtaala unaotumika ambao ni kinyume na mtaala wa Tanzania  ulioanzishwa kwa mujibu wa sheria  ya famasia Cap 311 na pia chuo hiki kilikumbushwa na TCU suala hili kwa barua yenye kumbukumbu namba TCU/A.40/1/VOL.II/14 ya tarehe 16/12/2014 na hata tarehe 4/6/2015 mbele ya bunge waziri wa afya alisema wazi kwamba hawawezi kumsajili mwanafunzi yeyote kama mtaala wa chuo chake haujapitishwa na bodi husika na taaluma inayotolewa na chuo husika iwe inakubalika.
     
Matatizo haya tumeweza kuyapitisha katika ngazi mbalimbali za kiserikali ikiwemo Tume ya vyuo vikuu nchini,bodi husika,kwa mkuu wa wilaya ya ilala na huko kote hatukupata ufumbuzi wa matatizo haya mpaka sasa tupo ngazi ya bunge.
          Hivyo basi sisi wanafunzi wote wa kitivo cha sayansi ya tiba katika chuo cha kimataifa kampala tunakiri wazi kwamba hatuna imani na majibu ya waziri wa elimu mh.Shukuru Kawambwa


HOJA ZA WANAFUNZI WOTE KWA UJUMLA WA KITIVO CHA SAYANSI NA TIBA
1.Uhalali wa hotuba wanazotoa hawa viongozi zinazopingana kama zile zinazotolewa na waziri wa elimu pamoja na waziri wa afya mwenye dhamana husika.
2.Kuto kuwepo kwa kwa uthibitisho sahihi wa juu ya usajili wa kozi husika katika  bodi zake.
3.Matumizi ya nguvu katika kutatua  mambo ya wazi kabisa ambayo ni muhimu kama vile matumizi ya mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kwa siku ya tarehe 8/06/2015
4.Bodi ya mikopo inatoaje mikopo katika chuo kilichosajiliwa kama chuo cha nje
5. Kwanini serikali inaruhusu chuo cha kimataifa Kampala (K.I.U) kisisimamiwe na  BODI ZA UFAMASIA ,MAHABARA ,na UDAKTARI zenye lengo la kusimamia ubora wa taaluma  ikiwa pamoja na kusimamia mitaala na kudhibiti  viwango vya waalimu wenye sifa  kufundisha  kozi za afya nchini kuliko ilivyo hivi sasa  ambapo mitaala haitambuliki na bodi hizo husika.
       
 
SISI KAMA  WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA KAMPALA TUNALAANI  VIKALI MATENDO                                      YAFUATAYO  TULIYOFANYIWA KATIKA VIPINDI HIVI VYA MGOMO MPAKA SASA

1.Wanafunzi kufukuzwa chuo kila wanapodai haki zao ambapo siku ya tarehe 30/04/2015 jumla ya wanafunzi kumi na sita ambao baadhi yao walikuwa wana kamati ya kufuatilia matatizo haya walisimamishwa masomo .na tarehe 2/06/2015 jumla ya wanafunzi watano walisimamishwa masomo kwa madai hayohayo na wanafunzi wapatao takribani 19 walipata kulala mahabusu kwa makosa yasiyoeleweka.
    
 2.polisi kutumia nguvu kutawanya wanafunzi ambao wamekaa na hawafanyi vurugu zozote na waliotii amri za kipolisi kwa kukaa chini hii tumeona siku ya tarehe 8/06/2015 ambapo polisi waliwamwagia wanafunzi maji ya kuwasha na kupiga mabomu na kuleta uvunjifu wa amani ambapo walisababisha wanafunzi wengi waliumia na wengine bado wapo katika matibabu mpaka sasa,masomo kusitishwa kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizo karibu na chuo kutokana na ulipukaji wa mabomu ya machozi vilevile kuathirika kwa wagonjwa katika kituo cha afya cha gongo la mboto kilicho jirani na chuo.

3.Viongozi mbalimbali wa kiserikali kuacha matatizo haya mpaka yanafikia hali hii kwamba wanafunzi wanahitimu taaluma yao na kushindwa kuajiliwa.

4.Tunalaani vikali uongozi wa chuo hiki kwa kushindwa kufuatilia  haya mapaka yanafika hatua hii.

                                                           
                MATATIZO AMBAYO HAYAJAFANYIWA UFUMBUZI HADI SASA

                                                                                        
                               
1.      Mitaala(curriculum) haijarekebishwa ili ifanane na vyuo vingine. Ref. TCU reg no. 40 ibara A uk. 17, reg no. 47 uk. 20 na reg no. 62 uk. 25
2.      Kukosekana kwa kalenda inayomuongoza mwanafunzi kwa mwaka mzima na kumuonesha utaratibu na ratiba za chuo mpaka sasa.
3.      Waalimu wengi wao kuto kuwa na sifa ya kufundisha kozi husika. Ref TCU reg no. 14 ibara ya 4.
4.      Kukosekana kwa uwiano sawa kati ya wafanyakazi wazawa na wageni hasa kwa ngazi za juu. Refer TCU Reg no. 14 ibara ya 3.
5.      Masomo ya pre entry ama MPP hayajatolewa  kabisa hasa ikizingatiwa masomo haya huchukua semester mzima na kuchelewesha wanafunzi kuendelea na kozi zao husika.
6.      Muda wa kuhitimu masomo uwe sawa na vyuo vingine kama utaratibu wa elimu ya nchi unavyotambua.
7.      Kusajiliwa kwa kada za sayansi ya afya na tiba katika bodi husika(full registration).
8.      Uongozi wetu haujabadilishwa akiwemo dean of faculty of health and applied science.
9.      Ada haujashuka  kama utaratibu wa TCU na wizara ya elimu ulivyoelekeza.
10.  Wanafunzi  wote waliosimamishwa  hawajarudishwa  maana walipewa kesi nyingi za kusingiziwa  na  zisizoeleweka



     MSIMAMO WA WANAFUNZI:
Kutokana na matatizo tajwa hapo juu ambayo yamekuwa na mizozo mikubwa sana hapa chuoni sisi kama umoja wa wanafunzi wa kada za afya tuna misimamo ifuatayo.
·         Bado tunaiomba serikali ituhamishe sehemu hii maana si salama kwetu sisi wanafunzi na haina uhakika wa kozi zake hali inayofanya wanafunzi weng huacha masomo.
·         Hatupo tayari kurudi katika majengo ya kampala international university mpaka matatizo yetu yapatiwe ufumbuzi(Tuhamishwe) ili chuo hiki kimalize matatizo hayo tajwa  maana ni mwaka mzima umekwisha bila sisi kusoma masomo yaliyopo kwenye kozi za afya


MASWALI YA MSINGI KWA WIZARA HUSIKA
1.      Kwanini wizara ya elimu idahili wanafunzi kuja kusoma kampala int. university bila kuwasiliana na wizara ya afya na bodi husika?.
2.      Kwanini chuo kinachukua wanafunzi wasiokuwa na vigezo kwa direct entry?
3.      Nini hatima ya waathirika wa matatizo haya ambao wamemaliza chuo na wamekosa ajira na kwa wale wanaoendelea?
4.      Ni hatua zipi za kisheria zinachukuliwa juu ya chuo hiki ikiwa chuo cha IMTU kilikuwa na matatizo machache kuliko haya lakini kilifungiwa?
              NB:Tamko hili limetolewa na Mwenyekiti  Mteule wa Wanafunzi, David Payovela na Katibu wake Jackson Raymond.