STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, June 12, 2015

Chile waanza vema Copa America, Cavani alikoroga

Cavani
WAKATI wenyeji wa michuano ya Kombe la Copa America, Chile wakianza vema michuano hiyo, mshambuliahji wa Kimataifa wa Uruguay na klabu ya Paris Saint-Germain, Edinson Canavi ameomba radhi baada ya kudai kuwa Jamaica ni ngumu kupambana nayo kama zilivyo timu zote za Afrika. 
Nyota huyo wa zamani wa Napoli alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanahabari kuelekea mchezo wao wa kesho Jumamosi dhidi nchi hiyo inayotoka upande wa mataifa ya Caribbean. 
Kauli hiyo ambayo wengi waliichukulia kama ya kibaguzi ilimfanya Cavani kuomba radhi haraka katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akidai alikuwa akifananisha aina ya uchezaji wa Jamaica na baadhi ya timu za Afrika na sio vinginevyo kama watu wanavyotafsiri. 
Nyota huyo aliomba radhi kwa watu wa Jamaica kwa kauli yake hiyo kueleweka vibaya na alikuwa hana nia yeyote mbaya. 
Uruguay ambao ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo wanatarajiwa kutupa karata yao ya kwanza katika michuano hiyo kesho wakichuana na Jamaica.
http://www.panamericanworld.com/sites/default/files/gm1e9970pi201142956718.jpg
Chile

Katika hatua nyingine Kocha wa timu ya taifa ya Chile, Jorge Sampaoli amekiri kuwa pamoja na magumu waliyokuwa nayo katika mchezo wao ufunguzi wa kundi A wa michuano ya Copa America dhidi ya Ecuador lakini anadhani walistahili ushindi wa mabao 2-0 waliopata. 
Mabao ya kipindi cha pili kutoka kwa Arturo Vidal na Eduardo Vargas yaliisaidia Chile kupata ushindi huo muhimu ingawa Sampaoli anadhani bado wanahitaji kuimarika zaidi kama wanataka kushinda taji la michuano hiyo wakiwa kama wenyeji. 
Akihojiwa kocha huyo amesema waliweka mipango yao kama walivyofanya katika mchezo dhidi ya Brazil, ambapo ilikwenda vyema katika kipindi cha kwanza lakini walihangaika kipindi cha pili baada ya kushindwa kufunga. 
Kocha huyo aliendelea kudai kuwa Ecuador waliwapa wakati mgumu kwani nao walikuwa wakishambulia kwa kasi hivyo ni wazi wanapaswa kujiandaa zaidi kwa michezo ijayo ili waweze kufika mbali. 
Chile itakwaana na Mexico Juni 15 katika mchezo wao wa pili wa hatua ya makundi ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment