STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, June 12, 2015

Utani wamtokea puani Mkurugenzi wa Mawasiliano FIFA, atimuliwa

UTANI wakati mwingine mbaya sana! Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Walter De Gregorio ametimuliwa baada ya kutoa kauli ya utani kuhusu shirikisho hilo katika kituo kimoja cha runinga cha huko Uswisi. 
Katika kipindi kimoja maarufu cha mahojiano nchini humo, Gregorio alitania kuwa Rais wa FIFA, Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Mawasiliano wote wanasafiri katika gari moja ambalo linaendeshwa na Polisi. 
Mara baada ya kauli hiyo FIFA ilitoa taarifa baadae kuwa De Gregorio ameamua kujiuzulu wadhifa wake huo, lakini wapekuzi wa mambo wanadai kuwa alitimuliwa na Rais wa FIFA Sepp Blatter. 
Blatter mwenyewe mapema mwezi huu alitangaza kujiuzulu pindi utakapofanyika uchaguzi mpya wa nafasi yake hiyo, ikiwa zimepita siku nne toka ateuliwe kuliongoza shirikisho hilo kea muhula wa tano. Shirikisho hilo lipo katika tuhuma nzito za ufisadi na vitendo vya rushwa vilivyosababisha maafisa wake kadhaa kutiwa mbaroni siku chache kabla ya uchaguzi uliomrejesha Blatter madarakani.

No comments:

Post a Comment