STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, February 7, 2015

Ngoma mpya ya AT-Sijazoea isikilize

http://4.bp.blogspot.com/_CNMo2Y_W50s/S-AWAU28FVI/AAAAAAAAA50/65JZzJP3rNM/s1600/DSC_1141.JPG
Msanii AT akiwa jukwaani
 

Everton, Liverpool hakuna mbabe, zashindwa kutambiana

Utemi na kutunishiana kifua ulikuwapo katika pambano hilo
Raheem Sterling akichuana na Aaron Lennon
Nahodha Steven Gerrard akijaribu kufunga mbele ya lango la Everton bila mafanikio
WAPINZANI wa jadi wa Merseyside, Everton na Liverpool zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka suluhu katika pambano kali lililomalizika hivi punde.
Licha ya kushambuliana kwa zamu na kuwepo kwa kosa kosa za hapa na pale katika pambano hilo lililochezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Everton wa Goodison timu hizo zilimaliza dakika 90 zikiwa 0-0 na kugawana pointi moja moja.
Katika pambano hilo Liverpool ilipata pigo mapema baada ya kiungo wak Lucas Leiva kuumia katika dakika ya 15 na nafasi yake kuchukuliwa na Joe Allen, huku Aaron Lennon akishuhudiwa akishuka dimbani kwa mara ya kwanza akiwa na jezi za Everton akitokea Spurs.

Torino yashinda ugenini, Juve, Milan hapatoshi!

http://www1.pictures.zimbio.com/gi/Amauri+Torino+FC+v+Hellas+Verona+FC+Serie+ysKatQlJvdhl.jpgTORINO ikiwa uwanja wa ugenini hivi punde katika Ligi Kuu ya Italia, Serie A, imetoa kipigo kwa wenyeji wao Hellas Verona kwa kuikandika mabao 3-1.
Mabao ya Joseph Martinez katika dakika ya 32 , Fabio Quagliarella kwa mkwaju wa penati dakika ya 50 na bao la dakika 80 kupitia kwa El Kaddouri huku bao la kufutia machozi likifungwa na Luca Toni dakika ya 83.
Muda mchache ujao watetezi Juventus watakuwa uwanja wa nyumbani mjini Turin kuvaana na AC Milan katika pambano la kukata na shoka la ligi hiyo ya Italia.

Cannavaro aomba radhi askari aliyemkumbatia Mkwakwani

http://4.bp.blogspot.com/-pxH2-GRW39I/UxgIPhAR70I/AAAAAAAAKTM/vAosaujzMrY/s1600/CANNA.tif
Nadir Haroub 'Cannavaro'
NAHODHA wa klabu ya Yanga na mfungaji wa bao pekee la Yanga wakati wanaizamisha Coastal Union nyumbani Mkwakwani Tanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amemuomba radhi askari aliyemkimbilia na kumkumbatia dakika chache baada ya kufunga.
Cannavaro alifunga bao hilo katika dakika ya 11, Jumatano iliyopita na kufanya kitendo hicho ambacho kilikuwa gumzo.
Cannavaro alisema alimuomba askari huyo msamaha muda mfupi baada ya mechi hiyo ambapo aliamua kumfuata na kumueleza kuwa hakuwa na nia mbaya.
Cannavaro alisema anamshukuru askari huyo kwa kukubali maombi yake ya msamaha aliyoyatoa kwani hakutarajia hali hiyo kutokea kutokana na furaha aliyoipata baada ya kufunga bao hilo.
“Kiukweli nilifanya kosa kukimbia na kwenda kumkumbatia askari wakati nashangilia bao nililolifunga, nilijikuta ghafla nafanya kitendo kile bila kutarajia, sikukitarajia kabisa wala sikupanga iwe hivyo.

“Baada ya mechi kumalizika nilimfuata nikazungumza naye, pia walikuwepo baadhi ya viongozi wangu na wale wa polisi niliwaomba radhi kwa kitendo hicho nilichokifanya, nikashukuru wakanielewa na kulimaliza tatizo hilo,” alisema Cannavaro. 
Saleh Jembe

Bayern Munich, Dortmund zazinduka Bundesliga

David Alaba scores a free-kick for Bayern Munich's second goal against Stuttgart
David Alaba akishangilia bao lake
BAADA ya kuyumba katika mechi zao mbili zilizopita za Bundesliga, Bayern Munich leo imezinduka wakiwa ugenini baada ya kuicharaza Stuttgart kwa mabao 2-0 na kujiimarisha kileleni, lichja ya wapinzani wao wa karibu Wolfsburg wakipata ushindi wa mabao 3-0 nyumbani dhidi ya Hoffenheim.
Arjen Robbin alifunga bao la kuongoza dakika ya 41 kabla ya David Alaba kuongeza la pili dakika ya 51 na kuwafanya Bayern kufikisha pointi 49 na kujichimbia kileleni.
Wapinzani wao Wolfsburg wanawapumulia Bayern baada ya kupata ushindi mnono nyumbani wa mabao 3-0 dhidi ya Hoffeinheim.
Mabingwa wa zamani wa ligi hiyo Borussia Dortmund walizinduka katika hali mbaya waliyonayo baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 ugeninmi dhidi ya Freiburg, ilhali Mainz 05 ilikubali kipigo cha mabao 2-0 nyumbani dhidi ya Hertha Berlin, na timu za Fc Koln na Paderborn zilishindwa kutambiana baada ya kutoka suluhu na hivi sasa  Hamburger SV ipo mbele kwa mabao 2-0 dhidi ya Hannover 96.

DR Congo watwaa nafasi ya 3 AFCON 2015

http://sport360.com/sites/default/files/styles/x644/public/article/462572530.jpg?itok=zFCD8UsM
DR Congo wakishangilia mechi yao ya robo fainali
TIMU ya soka ya DR Congo imefanikiwa kunyakua nafasi ya tatu ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya kuwanyuka wenyeji Guinea ya Ikweta kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya kumaliza dakika 90 bila kufungana katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Nuevo Estadio de Malabo.
Dakika 90 zilishuhudia timu hizo zikishindwa kufungana bao lolote licha ya kosa kosa za hapa na pale nas katika hatua hiyo ya penati wenyeji walipoteza mikwaju miwili ikiwamo nyota wapo Javier Balboa.
DRC walipata penati nne zilizotumbukizwa kimiani na Cedric Mabwati, Lema Mabidi, Chancel Mbemba na  Cedric Mongongu, huku wapinzani wao wakipata penati mbili kupitia kwa Juvenal na Doualla huku Raul Fabiani akifuata nyayo za Balboa.
Kesho ndiyo kesho kwa wanaume wa shoka Ivory Coast na Ghana zitaumana kwenye pambano la Fainali la michuano hiyo litakalochezwa kwenye uwanja wa Estadio de Bata, ikiwa ni mechi ya kisasi kinachorudisha nyuma kumbukumbu ya fainali kama hizo zilizochezwa mwaka 1992.
Katika pambano hilo Ivory Coast iliweka rekodi kwa kuitandika Ghana mabao 11-10 ya mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika 120 bila kufungana, huku timu hiyo ikicheza fainali hizo mwanzo hadi mwisho bila kuruhusu bao lolote katika muda wa kawaida hadi walipotwaa taji mbele ya Ghana.

Prisons yazidi kutaabika, Kagera Sugar yapumua!

http://3.bp.blogspot.com/-4vuDaX4RByE/VKj4o5VtnLI/AAAAAAAAOTo/RhhJKptdJ1c/s1600/Prisons%2BMbeya.JPG
Prisons-Mbeya wanaoburuza mkia
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/10906246_612237655589282_1427524500915532943_n.jpg
Mbeya City waliong'ang'aniwa na JKT Ruvu leo Chamazi
http://1.bp.blogspot.com/-MOkVqdpaJG0/VLqyQ2mWzOI/AAAAAAAAZG4/b2btW7QpS28/s1600/IMG_5633.JPG
Kagera Sugar angalau sasa wanapumua baada ya kuondoa gundu Kambarage-Shinyanga

KAGERA Sugar ambayo tangu ihame dimba lake la Kaitaba ilikuwa haijaonja ushindi zaidi ya kupokea vip[igo katika uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza na kuamua kukimbilia Kambarage, Shinyanga.
Katika pambano lao la kwanza kwenye uwanja huo mpya Kagera iliondoa gundu kwa kuichakaza Mgambo JKT kwa kuilaza bao 1-0.
Bao pekee la pambano hilo liliwekwa kimiani na Atupele Green dakika ya 50 kwa kichwa akiunganisha krosi pasi ya Daud Jumanne na kuwapa ushindi wa kwanza unaowapeleka hadi kwenye nafasi ya nane wakiizidi Simba wanaokamata nafasi ya 9, huku kipigi cha Mgambo kimewashusha hadi nafasi 12.
Maafande wa Prisons bado wapo mkiani wakiwa na pointi 11 baada ya mechi 13.

MSIMAMO LIGI KUU TANZANIA BARA:
                            P   W    D    L    F   A   GD  Pts
01. Azam             12  06   04   02  17  10  07   22
02. Yanga            12  06   04   02  13   07  06  22
03. Polisi Moro     14  04   07   03  12   11  01  19
04. JKT Ruvu       14  05   04   05  14   14  00  19
05. Ruvu Sh'ting  14  05   04   05  10   11   -1  19
06. Mtibwa Sugar 11  04   06   01  13   07  06  18
07. Coastal Union 14  04   06   04  11   10  01  18
08.
Kagera Sugar 14  04   06   04  11   11  00  18 
09. Simba            13  03   08   02  13   11  02  17
10. Mbeya City     13  04   04   05  09   11  -2   16
11.
Ndanda Fc      14  04  03   07  13    18  -5  15
12. Mgambo JKT   12  04  02  06   06    11  -5  14
13. Stand Utd       14  02  06   06   09   17  -8  12
14. Prisons           13  01  08   04   10   12  -2   11
Wafungaji:

7- Didier Kavumbagu(Azam)
6- Samuel Kamuntu (JKT Ruvu), Rashida Mandawa (Kagera Sugar)
5- Ame Ali (Mtibwa), Danny Mrwanda (Yanga)
4-
Rama Salim (Coastal),  Simon Msuva (Yanga),  Emmanuel Okwi (Simba),Nassor Kapama (Ndanda)
3- Ally Shomari (Mtibwa),  Jacob Massawe (Ndanda), Kipre tchetche (Azam)

Real Madrid na Ronaldo wao wazamishwa 4-0

Saul Niguez doubles Atletico's lead with a superb overhead kick just four minuted after the first goal 
Saul Niguez akifunga bao la pili la Atletico kwa tiktak
Mario Mandzukic akifunga bao la nne la Atletico Madrid
Cristiano Ronaldo looks dejected after Real Madrid concede two goals inside the opening 20 minutes of the game 
Kachokaaa! Ronaldo akiwa hoi timu yake ikitunguliwa ugenini
Former Bayern Munich midfielder Toni Kroos controls the ball while his old team-mate Mario Mandzukic closes him down 
Licha ya juhudi Real Madrid haikufua dafu kwa wapinzani wao wa jadi
MABINGWA wa Ulaya, Real Madrid licha ya kuwa na nahodha wake Cristiano Ronaldo wamepokea kipigo cha aibu cha mabao 4-0 toka kwa wapinzani wao wa jadi, Atletico Madrid katika pambano la La Liga lililochezwa kwenye uwanja wa Vincente Calderon.
Atletico ambao ndiyo watetezi la La Liga walianza kuwaadabisha wapinzani wao kwa kuandika bao la kwanza katika dakika ya 14 kupitia kwa Tiago kabla ya Saul Niguez kuongeza la pili dakika nne baadaye.
Mabao mengine yaliyendeleza ubabe wa Atletico Madrid dhidi ya wapinzani wao yalifungwa na Antoine Griezmann kwa shuti kali dakika ya 67kabla ya Mario Mandzukic kumalizia udhia kwa kufunga kwa kichwa dakika ya 89.Ligi hiyo itaendelea tena kwa michezo mingine mitatu ambapo hivi punde Villarreal ikiwa nyumbani imepata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Granada.


Arsenal yafa kwa Spurs, Man City yabanwa Itihad

Tottenham striker Harry Kane
Harry Kane aliyewaangamiza Arsenal leo
Harry Kane scores his first goal against Arsenal
Harry Kane akifunga bao la pili na la ushindi la  Spurs
Chelsea
Hazard na wachezaji wenzake wakishangilia bao la kwanza la Chelsea
Aston Villa
Jores Okore wa Aston Villa akishangilia bao la kufutia machozi la timu yake
James Milner scores Man City's equaliser against Hull
James Milner akiisawazishia Manchester CIty waliokuwa wakielekea kuzama nyumbani mbele ya Hull City leo
WAKATI Arsenal wakiduwazwa ugenini kwa kucharazwa mabao 2-1 na wapinzani wao wa jadi wa London ya Kaskazini, Tottenham Hotspur, mabingwa watetezi Manchester City imeng'ang'aniwa nyumbani  na Hull City na kutpoka sare ya 1-1, huku Chelsea ikizidi kujichimbia kileleni kwa kuilaza Asron Villa mabao 2-1.
Arsenal ikienda kwenye uwanja wa White Hart Lane wakiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Aston Villa walitangulia kupata bao dakika ya 11 kupitia Mesut Ozil bao lililodumu hadi wakati wa mapumziko.
Wenyeji walirejea kipindi cha pili na hasira na kufanikiwa kuyarejesha mabao hayo kupitia kwa kinda linalotisha kwa sasa England, Harry Kane aliyefunga katika dakika ya 56 na 86 na kuipa ushindi muhimu Vijogoo vya London na kufikisha pointu 43 na kuingia kwenye Nne Bora wakiishusha Arsenal.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo Mabingwa watetezi walilazimishwa sare ya 1-1 na Hull City, huku Chelsea wakishinda mabao 2-1 ugenini dhidi ya timu isiyofunga mabao ya Aston Villa,.
Mechi nyingine Southampton ikiwa ugenini ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya QPR,  Swansea City ililazimishwa sare ya 1-1 na Sunderland, huku Leicester City ilikubali kipigo cha bao 1-0 nyumbani dhidi ya Crystal Palace.
Hivi sasa Everton na wapinzani wao wa jadi wa Merseyside, Liverpool zinajiandaa kupepetana kwenye uwanja wa Goodson Park.

Mnyama ashindwa kutamba Tanga, Azam yarudi kileleni

* Kagera Sugar yaondoa gundu Shinyanga, Ndanda bado sana nyumbani

http://4.bp.blogspot.com/-HlzYMgUqY6E/VLYmO19_SFI/AAAAAAAAw04/Tum0BDfocyc/s1600/simba-mapinduzi_2015.jpg
Simba iliyong'ang'aniwa Tanga
http://api.ning.com/files/cPakA0chAEyfyqjZRP3k2djpZ9GyxNW23W69D7FY4fYhsuNz2vmH6gr7yEITcci18IdnTvIgOej4xydmYu8LtJiXW0uQDhCL/16.jpg
Kagera Sugar waliooindoa 'gundu' kwa kushinda uwanja wa Shinyanga
http://3.bp.blogspot.com/-PppuzbfEWwc/VL6E1nJsTMI/AAAAAAAAA_M/9P9teC7mt0Y/s1600/10847549_808297752551709_8272495318791573431_o-790072.jpg
Azam waliorejea kileleni kwa muda baada ya sare ya 2-2 mjini Morogoro
MDUDU wa sare ametawala katika viwanja vitano wakati wa michezo ya  Ligi Kuu Tanzania Bara zilizochezwa jioni ya leo, 'Mnyama', Simba alishindwa kufurukuta Tanga na Azam wakang'anganiwa Morogoro.
Simba ikicheza na Coastal Union kwenye uwanja wa Mkwakwani walitoka suluhu, wakati Azam walitoshana nguvu na Polisi Moro kwa kutoka sare ya mabao 2-2.
Magoli katika pambano la mjini Morogoro, mabingwa watetezi walipata mabao yake kupitia kwa mapacha Kipre Tchetche  dakika 10 na Kipre Balou dakika 66 kwa frikiki.
Polisi walipata mabao yake kupitia Edward Christopher katika dakika ya 25 na Selemen Kassim Selembe' dakika ya 69.
Katika uwanja wa Chamazi, JKT Ruvu na Mbeya City walitoka sare ya bao 1-1, matokeo yaliyofana na yale ya mjini Mtwara kati ya Ndanda Fc dhidi ya wageni wao Stand United.
Wenyeji walishtushwa kwa bao la dakika ya 9 la wageni lililofungwa na Jibelele Abasilim kabla ya kuja kusawazisha katika dakika ya 53 kupitia kwa Nassor Kapama.
Mjini Mbeya, wenyeji Prisons ilishindwa kutamba Kwenye uwanja wa Sokoine, baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Ruvu Shooting.
Ruvu walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 17 kupitia kwa Yahya Tumbo kwa tiktak kabla ya wenyeji kusawazisha dakika ya 36 kupitia kwa  Jacob Kalipalate na kuzifanya timu hizo zigawane pointi moja moja.
Kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga, Kagera Sugar waliondoa gundi baada ya kuicharaza Mgambo JKT bao 1-0. Bao hilo liliwekwa kimiani na Atupele Green.
Ushindi huo umeifanya Kagera kufikisha pointi 18 na kuzidi kuifanya ligi hiyo kuwa ngumu kutokana na klabu kufungana au kutofautiana kwa pointi chache, Azam wakirejea kileleni wakiiengua Yanga.
Licha ya timu zote kuwa na pointi 22 Azam wanaongoza kwa uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa, huku Mtibwa wakiporomoka kutoka  nafasi ya tatu hadi ya sita.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa pambano moja tu kwenye uwanja wa Taifa, Yanga ikivaana na Mtibwa Sugar katika mechi ya kisasi kwani Mtibwa waliitoa nishai Yanga kwenye uwanja wa Morogoro kwa kuifunga mabao 2-0 katika mechi ya ufunguzi wa ligi ya msimu huu uwanja wa Jamhuri.

TANZAIA: MUINGIZAJI WA KAOLE AFARIKI DUNIA

http://4.bp.blogspot.com/-XS6FexPcfp0/VKFEEGMHDKI/AAAAAAAAt5E/Ie3iQQZBKBM/s1600/KaoneSanaa-cut-533.jpg
Baadhi ya wasanii waliowahi kuigiza na Mama Mashaka wakiwa na Januari Makamba. Wasanii hawa wamelifufua kundi kwa jina jipya la Kaone Sanaa Group
MSANII wa maigizo aliyewahi kuwika na kundi la Kaole Sanaa Group, Mwajuma Abdallah ‘Mama Mashaka’ amefariki dunia.
Mama Mashaka amefariki usiku wa kuamkia leo majira ya saa tano za usiku katika Hospitali ya Amana iliyopo Ilala, jijini, Dar.Kwa habari zaidi tutaendelea kukujuza hapa.
GPL

BALAA TUPU LEO LIGI KUU YA ENGLAND

http://www.independent.co.uk/incoming/article9756138.ece/alternates/w620/Liverpool%20v%20Everton,%20Arsenal%20v%20Tottenham:%20The%20major%20talking%20points%20this%20weekend%20in%20the%20Premier%20League.jpghttp://news.bbcimg.co.uk/media/images/80827000/jpg/_80827370_newsplit.jpgWAKATI nahodha wa Manchester City Vincent Kompany akidai anaamini kuwa uzoefu wa sasa wa mabingwa hao unaweza kuwasaidia kukwea kileleni katika kiti walichokalia Chelsea katika msimamo wa Ligi Kuu ya England, leo ni kama vita katika ligi hiyo.
Arsenal watavaana na wapinzani wa jadi wa London ya Kaskazini, Tottenham, wakati Liverpool watawafuata wapinzani wao wa jadi Everton.
City iliyopo katika nafasi ya pili leo itacheza mchezo wake wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Hull City kwenye uwanja wa Etihad ikiwa pointi tano nyuma ya vinara Chelsea, ambao watakuwa ugenini leo dhidi ya Aston Villa.
Kikosi hicho cha kocha Manuel Pellegrini kilikuwa pointi moja nyuma ya Liverpool wakati zimebaki mechi mbili kabla ya kumalizika kwa msimu uliopita lakini iliweza kutwaa taji la Ligi Kuu.
Na Man City ilikuwa pointi nane nyuma ya Manchester United wakati zimebaki mechi sita kabla hawajatwaa taji la Ligi Kuu siku ya mwisho ya msimu wa mwaka 2011/12 wakiwa chini ya kocha wazamani wa timu hiyo Roberto Mancini.
"Hii ndio hali ya kawaida kwetu, alisema Kompany beki wa kati kutoka Ubelgiji, ambaye alikuwa mchezaji muhimu wakati timu hiyo ilipotwaa taji hilo mara zote.
"Kuwa pointi tano nyuma Januari au Februari ni jambo kubwa.
"Tunajisikia vizuri kuwa katika nafasi hiyo. Tumekuwa katika nafasi hiyo mara nyingi."
Huku Man United wakitawala misimu miwili iliyopita, Chelsea waliweza kufanya mambo kama Man City kama wapinzani wakubwa katika mbio za kuwania taji.
Man United wamekuwa wakipambana tangu kuondoka kwa Alex Ferguson mwaka 2013 na sio ama mbadala wake, David Moyes na Louis van Gaal, aliweza kuiweka timu hiyo katika mbio za ubingwa.
Ukiacha tambo hizo za Kompany, ligi hiyo leo itakuwa kama vita wakati viwanja kadhaa vitakavyotimua vumbi huku gumzo likiwa mechi za watani wa miji ya London na Liverpool.
Liverpool watakuwa ugenini kuvaana na Everton, kama itakavyokuwa kwa Arsenal watakaowafuata Tottenham Hotspur uwanja wa White Hart Lane.
Ratiba kamili EPL ipo hivi wikiendi hii:
Leo Jumamosi:
Tottenham     v    Arsenal   (Saa 9:45 alasiri)
Man City  v    Hull City (Saa 12:00 jioni)
Villa     v    Chelsea   (Saa 12:00 jioni)
Swansea  v    Sunderland  (Saa 12:00 jioni)
QPR  v    Southampton (Saa 12:00 jioni)
Leicester     v    Palace (Saa 12:00 jioni)
Everton   v    Liverpool (Saa 2:30 usiku)
Kesho Jumapili:
Burnley   v    West Bromwich (Saa 9:00 alasiri) 
Newcastle v   Stoke City (Saa 11:05).
West Ham  v   Man United

Zidane kumrithi Ancelotti Real Madrid

http://i.cbc.ca/1.2649728.1400694761!/cpImage/httpImage/image.jpg_gen/derivatives/16x9_620/zinedine-zidane.jpg
Zidane kushoto akiwa na Ancelotti
 MADRID, Hispania
GWIJI wa zamani wa Ufaransa, Zinedine Zidane ananolewa ili aje kuwa kocha wa baadaye wa klabu ya Real Madrid, alisema Carlo Ancelotti.
Zidane, ambaye kwa sasa ndiye anakinoa kikosi cha akiba cha Real Madrid cha Castilla, "ana viwango vyote " vinavyohitajika kushika usukani wa klabu, alisema Ancelotti alipozungumza na waandishi wa habari.
"Nafurahia kazi ya Zidane, anafanya vizuri sana, " alisema Ancelotti katika mahojiano hayo.
Baada ya mwanzo mgumu wa msimu, Castilla wako kileleni mwa ligi daraja la tatu ya Hispania.
"Anafanya vizuri sana katika mwaka wake wa kwanza wa kuifundisha timu hiyo. Ameichukua Castilla hadi katika nafasi ya kwanza na anatakiwa kuendeleza kazi hiyo nzuri.
"Kwangu ni wazi kuwa ana vigezo vyote vya kuwa kocha wa kuifundisha timu kubwa. Na ikiwemo Real Madrid," alisema kocha huyo Muitalia, aliyemteua gwiji huyo Mfaransa msimu uliopita.
Baada ya kushuhudia Castilla ikipoteza mechi zake tano kati ya sita za mwanzo, Zidane alibadili mambo na pamoja na ugeni wake katika kuifundisha timu hiyo, sasa amepoteza mchezo mmoja tu katika miezi minne iliyopita.
Timu hiyo inaweza kuongeza tofauti ya pointi endapo Jumapili kesho itashinda itakapocheza dhidi ya Athletic Bilbao.

MKWAKWANI PATACHIMBIKA NI COASTAL, SIMBA!

Simba
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/coastal-union1.jpg
Coastal Union
http://www.azamfc.co.tz/sites/default/files/imagecache/slides/AZAM%20FC.JPG
Azam Fc watakaoivaa Polisi Moro na mbinu za Kikongo
http://kabumbu.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/polisi-moro-KIKOSI.jpg
Maafande wa Polisi Moro watahimili vishindo vya Azam uwanja wa Jamhuri?
PATACHIMBIKA Mkwakwani! Ndivyo unavyoweza kusema wakati 'Mnyama' Simba watakaposhuka dimbani kuvaana na 'ndugu' zao, Coastal Union katika pambano la Ligi Kuu Tanzania Bara.
Aidha mabingwa watetezi Azam watakuwa uwanja wa Jamhuri, Morogoro kuwafundisha Polisi Moro mbinu mpya za Kikongo watakapoumana kwenye mfululizo wa ligi hiyo.
Coastal Union iliyofumuliwa na Yanga bao 1-0 katikati ya wiki watakuwa na kazi ngumu ya kuwasimamisha Simba iliyozinduka tangu walipolambwa mabao 2-1 na Mbeya City.
Simba iliitandika JKT Ruvu mabao 2-0 katika pambano la kusisimua wiki iliyopita na hivo watavaana na Coastal wakiwa na ari na nguvu kubwa.
Ikiwategemea nyota wake wa KIganda, Emmanuel Okwi, Dan na nduguye Simon Sserunkuma itashuka dimba la Mkwakwani wakiwa na nia ya kuongeza pointi tatu ili wasogea maeneo ya juu baada ya kushindwa kuonja kwa muda mrefu tangu ligi ilipoanza Septemba 20 mwaka jana.
Mechi nyingine ya kutupiwa macho ni ile ya Azam dhidi ya Polisi itakayochezwa uwanja wa Jamhuri, ambapo Polisi wakiwa wanachekelea kuizima Mbeya City katika mechi hiyo iliyopita itataka kuwazima Azam wanatokea DR Congo walipoenda kushiriki michuano maalum.
Meneja wa Azam, Jemedari Said amesema kikosi chao kipo tayari kwa vita mbele ya Polisi, huku habari ambazo MICHARAZO inayo ni kwamba klabu hiyo imevamia tawi la Simba la Mpira Pesa la Magomeni Mikumi na kuwanunua mashabiki kuwapeleka Morogoro kwa ajili ya kuwapa sapoti katika mchezo huo.
Azam watakuwa wakihitaji ushindi ili kurejea kileleni angalau kwa muda baada ya Yanga watakaocheza kesho dhidi ya Mtibwa Sugar, kuwaengua katikatgi ya wiki baada ya kuwalaza Coastal.
Mabingwa watetezi hao wana pointi 21, moja pungufu na ilizonazo Yanga wenye 22 na waliokaa kileleni, huku Polisi wakiwa nafasi ya Nne wakiwa na pointi 18 sawa na ilizonazo JKT Ruvu, Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar.
Mechi nyingine za ligi hiyo leo ni pambano la kukata na Mundu kati ya Ndanda Fc dhidi ya Stand United katika mechi ya kisasi itakayochezwa uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, huku Mgambo JKT baada ya 'likizo' ndefu itashuka dimba la Kambarage Shinyanga kuvaana na 'wenyeji' wao Kagera Sugar waliohamia katika uwanja huo toka CCM Kirumba.
Maafande wa Prisons wakuwa uwanja wa nyumbani wa Sokoine, Mbeya kuwaalika Ruvu Shooting katika mchezo mwingine wa kisasi baada ya Prisons kuwatoa nishai wapinzani wao kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Mabatini katika mechi ya ufunguzi wa duru la kwanza.
Baada ya kupokea kichapo toka kwa Simba, maafande wengine wa JKT Ruvu watakuwa uwanja wa nyumbani wa Chamazi kuwakaribisha wababe wa Simba, Mbeya City katika mechi kali ya kusisimua inayowakutanisha makocha wenye rekodi nzuri Fred Minziro na Juma Mwambusi.

Wenyeji Guinea ya Ikweta watozwa faini


256137B200000578-2941812-image-a-28_1423209530874
WENYEJI wa fainali za kombe la Mataifa ya Africa, Afcon 2015, Guinea ya Ikweta wametozwa faini ya dola laki moja kwa mtafaruku wa juzi usiku katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Ghana ‘Black Stars’.
Hata hivyo CAF imesema Guinea ya Ikweta wataucheza mpambano wao wa kusaka Msindi wa Tatu dhidi ya DR Congo mchezo unaochezwa leo.
Plastic bottles and other debris litter the running track at the Malabo Stadium following the crowd disturbances
Mashabiki wa timu mwenyeji walifanya vurugu na kuwarushia chupa za maji wachezaji wa Ghana, Viongozi pamoja na mashabiki.
Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya mashabiki hao, huku wachezaji wa Ghana wakitolewa uwanjani chini ya ulinzi mkali.
Vurugu hizo zilisababisha mechi kusimama kwa dakika 35, lakini Ghana walifuzu fainali kutokana na ushindi wa mabao 3-0.
Ghana wanasema katika vurugu zile watu wangeweza kufa, ingawa inaelezwa watu 14 walijeruhiwa akiwa raia wa Mali aliyeumia vibaya.

Nyosso, Morris wafungiwa kisa 'uhuni' uwanjaniSHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limefungua makucha yake na kumuadhibu beki ngangari wa Mbeya City, Juma Nyosso kwa kitendo cha kumshika mshambuliaji wa timu yake ya zamani, Simba Elias Maguri.
TFF imemfungia Nyosso adhabu ya mechi nane na klabu yake imesema itakata rufaa kwa mabai ni ya kionevu na yenye kuviza maendeleo ya soka hata kama ni kweli beki wao alifanya kitndo hicho kinavyotafrisiwa kuwa ni 'udhalilishaji'.
Nyosso anatuhumiwa kumfanya 'ubasha' Maguri timu zao zilipokutana January 28 na Simba kulala mabao 2-1.
Mbali na Nyosso pia TFF imemfungia mechi tatu beki mahiri wa Azam, Aggrey Morris kwa madaiu ya kumpiga kiwiko kilichomfanya mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi kuzimia uwanjani.
Morris anadaiwa kufanya tukio hilo wakati timu hizo zilipokutana kwenye uwanja wa Taifa Januari 25 na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Beki mwingine George Assey anayedaiwa kumpiga kabali Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe yeye amewekwa kiporo kwa kushindwa kuhudhuria kikao cha kamati ya Nidhamu iliyotoa adhabu hizo.
Assey anayeichezea Ruvu Shooting alionekana akimniga na kumtoa damu Tambwe katikia mechi yao kwenye uwanja wa Taifa iliyoisha kwa sare isiyo na magoli.

Ancelotti awakosa Rodriguez, Ronaldo Madrid Derby

http://www1.pictures.zimbio.com/gi/James+Rodriguez+Club+Atletico+de+Madrid+v+xwEg2Ahj4GDl.jpg
Ameikosa Derby ya Madrid baada ya kuumia mguu
http://www.realmadridfootballblog.com/wp-content/uploads/2013/05/1530-cristiano-ronaldo-real-madrid.jpg
Ronaldo karudi
KOCHA klabu ya ya Real Madrid, Carlo Ancelotti amethibitisha kuwa James Rodriguez na Sergio Ramos watakosa mchezo wa La Liga dhidi ya mahasimu wao jiji Atletico Madrid leo Jumamosi, lakini cha kufurahisha ni kwamba nyota wake Cristiano Ronaldo atakuwepo katika mchezo huo.
Ronaldo alikosa mechi iliyopita kutokana na adhabu iliyotokana na kadi nyekundu na leoi atarejea kwenye mechi hiyo ya watani wa jadi wa jiji la Madrid litakalochezwa kwenye uwanja wa Estadio Vincente Calderon nyumbani kwa mabingwa watetezi wa La Liga, Atletico Madrid.
Ancelotti atawakosa wachezaji wake wawili Rodriguez na Ramos baada ya wawili hao walipata majeruhi katika mchezo wa majuzi wakiiitandika Sevilla kwa mabao 2-1, ambapo Ramos alipata majeruhi ya msuli wa paja huku Rodriguez akielezwa kuvunjika mguu wa  kulia baada ya kufunga bao la kuongoza.
Ancelotti sasa anakabiliwa na uhaba wa mabeki kutokana na beki wake wa kati Pepe naye kuwa nje kutokana na majeruhi ya mbavu.
Hata hivyo, Ancelotti ana matumaini chipukizi Raphael Varane na Nacho wataweza kumudu changamoto za Atletico iliyo chini Diego Simeone.
Akihojiwa Ancelotti amesema pamoja na kuwakosa mabeki wake kutegemea lakini bado ana imani na waliopo akiwemo Nacho na Varane kwamba wataweza kuhimilia mikikimikiki ya wapinzano wao hao.

NGOMA MPYA YA DAYNA NYANGE-PEPEA

http://3.bp.blogspot.com/-lOrzPztIzT4/UiMopms7pYI/AAAAAAAAAaA/QLGZzSAV3Wk/s640/dayna.JPG
Dayna Nyange katika pozi
BONYEZA HAPA KUUSIKILIZA WIMBO MPYA WA DAYNA NYANGE 
 Dayna Nyange - Pepea @Hulkshare: