STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, February 7, 2015

MKWAKWANI PATACHIMBIKA NI COASTAL, SIMBA!

Simba
http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/coastal-union1.jpg
Coastal Union
http://www.azamfc.co.tz/sites/default/files/imagecache/slides/AZAM%20FC.JPG
Azam Fc watakaoivaa Polisi Moro na mbinu za Kikongo
http://kabumbu.co.tz/wp-content/uploads/2015/01/polisi-moro-KIKOSI.jpg
Maafande wa Polisi Moro watahimili vishindo vya Azam uwanja wa Jamhuri?
PATACHIMBIKA Mkwakwani! Ndivyo unavyoweza kusema wakati 'Mnyama' Simba watakaposhuka dimbani kuvaana na 'ndugu' zao, Coastal Union katika pambano la Ligi Kuu Tanzania Bara.
Aidha mabingwa watetezi Azam watakuwa uwanja wa Jamhuri, Morogoro kuwafundisha Polisi Moro mbinu mpya za Kikongo watakapoumana kwenye mfululizo wa ligi hiyo.
Coastal Union iliyofumuliwa na Yanga bao 1-0 katikati ya wiki watakuwa na kazi ngumu ya kuwasimamisha Simba iliyozinduka tangu walipolambwa mabao 2-1 na Mbeya City.
Simba iliitandika JKT Ruvu mabao 2-0 katika pambano la kusisimua wiki iliyopita na hivo watavaana na Coastal wakiwa na ari na nguvu kubwa.
Ikiwategemea nyota wake wa KIganda, Emmanuel Okwi, Dan na nduguye Simon Sserunkuma itashuka dimba la Mkwakwani wakiwa na nia ya kuongeza pointi tatu ili wasogea maeneo ya juu baada ya kushindwa kuonja kwa muda mrefu tangu ligi ilipoanza Septemba 20 mwaka jana.
Mechi nyingine ya kutupiwa macho ni ile ya Azam dhidi ya Polisi itakayochezwa uwanja wa Jamhuri, ambapo Polisi wakiwa wanachekelea kuizima Mbeya City katika mechi hiyo iliyopita itataka kuwazima Azam wanatokea DR Congo walipoenda kushiriki michuano maalum.
Meneja wa Azam, Jemedari Said amesema kikosi chao kipo tayari kwa vita mbele ya Polisi, huku habari ambazo MICHARAZO inayo ni kwamba klabu hiyo imevamia tawi la Simba la Mpira Pesa la Magomeni Mikumi na kuwanunua mashabiki kuwapeleka Morogoro kwa ajili ya kuwapa sapoti katika mchezo huo.
Azam watakuwa wakihitaji ushindi ili kurejea kileleni angalau kwa muda baada ya Yanga watakaocheza kesho dhidi ya Mtibwa Sugar, kuwaengua katikatgi ya wiki baada ya kuwalaza Coastal.
Mabingwa watetezi hao wana pointi 21, moja pungufu na ilizonazo Yanga wenye 22 na waliokaa kileleni, huku Polisi wakiwa nafasi ya Nne wakiwa na pointi 18 sawa na ilizonazo JKT Ruvu, Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar.
Mechi nyingine za ligi hiyo leo ni pambano la kukata na Mundu kati ya Ndanda Fc dhidi ya Stand United katika mechi ya kisasi itakayochezwa uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, huku Mgambo JKT baada ya 'likizo' ndefu itashuka dimba la Kambarage Shinyanga kuvaana na 'wenyeji' wao Kagera Sugar waliohamia katika uwanja huo toka CCM Kirumba.
Maafande wa Prisons wakuwa uwanja wa nyumbani wa Sokoine, Mbeya kuwaalika Ruvu Shooting katika mchezo mwingine wa kisasi baada ya Prisons kuwatoa nishai wapinzani wao kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Mabatini katika mechi ya ufunguzi wa duru la kwanza.
Baada ya kupokea kichapo toka kwa Simba, maafande wengine wa JKT Ruvu watakuwa uwanja wa nyumbani wa Chamazi kuwakaribisha wababe wa Simba, Mbeya City katika mechi kali ya kusisimua inayowakutanisha makocha wenye rekodi nzuri Fred Minziro na Juma Mwambusi.

No comments:

Post a Comment