DR Congo wakishangilia mechi yao ya robo fainali |
Dakika 90 zilishuhudia timu hizo zikishindwa kufungana bao lolote licha ya kosa kosa za hapa na pale nas katika hatua hiyo ya penati wenyeji walipoteza mikwaju miwili ikiwamo nyota wapo Javier Balboa.
DRC walipata penati nne zilizotumbukizwa kimiani na Cedric Mabwati, Lema Mabidi, Chancel Mbemba na Cedric Mongongu, huku wapinzani wao wakipata penati mbili kupitia kwa Juvenal na Doualla huku Raul Fabiani akifuata nyayo za Balboa.
Kesho ndiyo kesho kwa wanaume wa shoka Ivory Coast na Ghana zitaumana kwenye pambano la Fainali la michuano hiyo litakalochezwa kwenye uwanja wa Estadio de Bata, ikiwa ni mechi ya kisasi kinachorudisha nyuma kumbukumbu ya fainali kama hizo zilizochezwa mwaka 1992.
Katika pambano hilo Ivory Coast iliweka rekodi kwa kuitandika Ghana mabao 11-10 ya mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika 120 bila kufungana, huku timu hiyo ikicheza fainali hizo mwanzo hadi mwisho bila kuruhusu bao lolote katika muda wa kawaida hadi walipotwaa taji mbele ya Ghana.
No comments:
Post a Comment