Zidane kushoto akiwa na Ancelotti |
MADRID, Hispania
GWIJI wa zamani wa Ufaransa, Zinedine Zidane ananolewa ili aje kuwa kocha wa baadaye wa klabu ya Real Madrid,
alisema Carlo Ancelotti.
Zidane, ambaye kwa sasa ndiye anakinoa kikosi cha akiba cha Real
Madrid cha Castilla, "ana viwango vyote " vinavyohitajika kushika
usukani wa klabu, alisema Ancelotti alipozungumza na waandishi wa habari.
"Nafurahia kazi ya Zidane, anafanya vizuri sana, " alisema
Ancelotti katika mahojiano hayo.
Baada ya mwanzo mgumu wa msimu, Castilla wako kileleni mwa ligi
daraja la tatu ya Hispania.
"Anafanya vizuri sana katika mwaka wake wa kwanza wa
kuifundisha timu hiyo. Ameichukua Castilla hadi katika nafasi ya kwanza na
anatakiwa kuendeleza kazi hiyo nzuri.
"Kwangu ni wazi kuwa ana vigezo vyote vya kuwa kocha wa
kuifundisha timu kubwa. Na ikiwemo Real Madrid," alisema kocha huyo
Muitalia, aliyemteua gwiji huyo Mfaransa msimu uliopita.
Baada ya kushuhudia Castilla ikipoteza mechi zake tano kati ya
sita za mwanzo, Zidane alibadili mambo na pamoja na ugeni wake katika
kuifundisha timu hiyo, sasa amepoteza mchezo mmoja tu katika miezi minne
iliyopita.
Timu hiyo inaweza kuongeza tofauti ya pointi endapo Jumapili kesho
itashinda itakapocheza dhidi ya Athletic Bilbao.
No comments:
Post a Comment