WENYEJI
wa fainali za kombe la Mataifa ya Africa, Afcon 2015, Guinea ya Ikweta
wametozwa faini ya dola laki moja kwa mtafaruku wa juzi usiku katika
mechi ya nusu fainali dhidi ya Ghana ‘Black Stars’.
Hata hivyo CAF imesema Guinea ya Ikweta wataucheza mpambano wao wa kusaka Msindi wa Tatu dhidi ya DR Congo mchezo unaochezwa leo.
Mashabiki wa timu mwenyeji walifanya vurugu na kuwarushia chupa za maji wachezaji wa Ghana, Viongozi pamoja na mashabiki.
Polisi
walilazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya mashabiki hao, huku
wachezaji wa Ghana wakitolewa uwanjani chini ya ulinzi mkali.
Vurugu hizo zilisababisha mechi kusimama kwa dakika 35, lakini Ghana walifuzu fainali kutokana na ushindi wa mabao 3-0.
Ghana wanasema katika vurugu zile watu wangeweza kufa, ingawa inaelezwa watu 14 walijeruhiwa akiwa raia wa Mali aliyeumia vibaya.
No comments:
Post a Comment