WAKATI nahodha wa Manchester City Vincent Kompany akidai anaamini kuwa uzoefu wa
sasa wa mabingwa hao unaweza kuwasaidia kukwea kileleni katika kiti
walichokalia Chelsea katika msimamo wa Ligi Kuu ya England, leo ni kama vita katika ligi hiyo.
Arsenal watavaana na wapinzani wa jadi wa London ya Kaskazini, Tottenham, wakati Liverpool watawafuata wapinzani wao wa jadi Everton.
City iliyopo katika nafasi ya pili leo itacheza mchezo wake wa
Ligi Kuu ya England dhidi ya Hull City kwenye uwanja wa Etihad ikiwa pointi
tano nyuma ya vinara Chelsea, ambao watakuwa ugenini leo dhidi ya Aston
Villa.
Kikosi hicho cha kocha Manuel Pellegrini kilikuwa pointi moja
nyuma ya Liverpool wakati zimebaki mechi mbili kabla ya kumalizika kwa msimu
uliopita lakini iliweza kutwaa taji la Ligi Kuu.
Na Man City ilikuwa pointi nane nyuma ya Manchester United wakati
zimebaki mechi sita kabla hawajatwaa taji la Ligi Kuu siku ya mwisho ya msimu
wa mwaka 2011/12 wakiwa chini ya kocha wazamani wa timu hiyo Roberto Mancini.
"Hii ndio hali ya kawaida kwetu, “alisema Kompany beki wa kati kutoka Ubelgiji, ambaye alikuwa mchezaji muhimu
wakati timu hiyo ilipotwaa taji hilo mara zote.
"Kuwa pointi tano nyuma Januari au Februari ni jambo kubwa.
"Tunajisikia vizuri kuwa katika nafasi hiyo. Tumekuwa katika
nafasi hiyo mara nyingi."
Huku Man United wakitawala misimu miwili iliyopita, Chelsea waliweza kufanya mambo kama Man City kama wapinzani
wakubwa katika mbio za kuwania taji.
Man United wamekuwa wakipambana tangu kuondoka kwa Alex Ferguson mwaka
2013 na sio ama mbadala wake, David Moyes na Louis van Gaal, aliweza kuiweka
timu hiyo katika mbio za ubingwa.
Ukiacha tambo hizo za Kompany, ligi hiyo leo itakuwa kama vita wakati viwanja kadhaa vitakavyotimua vumbi huku gumzo likiwa mechi za watani wa miji ya London na Liverpool.
Liverpool watakuwa ugenini kuvaana na Everton, kama itakavyokuwa kwa Arsenal watakaowafuata Tottenham Hotspur uwanja wa White Hart Lane.
Ratiba kamili EPL ipo hivi wikiendi hii:
Leo Jumamosi:
Tottenham v Arsenal (Saa
9:45 alasiri)
Man City v Hull City (Saa
12:00 jioni)
Villa v Chelsea (Saa
12:00 jioni)
Swansea v Sunderland
(Saa 12:00 jioni)
QPR v Southampton (Saa 12:00 jioni)
Leicester v Palace (Saa 12:00 jioni)
Everton v Liverpool (Saa
2:30 usiku)
Kesho Jumapili:
Burnley v West Bromwich (Saa 9:00 alasiri)
Newcastle v Stoke City (Saa
11:05).
West Ham v Man United
No comments:
Post a Comment