STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, June 15, 2014

Ronaldo awatoa hofu Ureno wakijiandaa kuivaa Ujerumani

Ronaldo alipokuwa akitoka uwanjani kwenye mazoezi
WAKATI nchi yake kesho ikitarajiwa kuwa na kibarua kigumu mbele ya Wajerumani katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia, Mshambuliaji nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo amewatoa hofu mashabiki wa timu yake.
Ronaldo aliviambia vyombo vya habari nchini kwake kuwa majeraha ya goti lake la kushoto yamepona, wakati akifanya mazoezi. 
Zaidi mashabiki wapatao 10,000 walikuwepo kutizama mazoezi hayo ya wazi huko Campinas ambapo kuna wakati mwanamke mmoja alikimbia uwanjani na kujaribu kumfikia Ronaldo na kuzuiwa na walinzi kabla ya kukimbia tena mita 40 na kuwekwa chini na walinzi wengine. 
Ronaldo ambaye alicheza mchezo wa kirafiki ambao Ureno iliitandika Ireland kwa mabao 5-1, alimfuata mwanamke huyo aliwekwa chini ya ulinzi na kuweka saini katika fufala yake kabla ya wachezaji wengine wa Ureno nao kuvua fulana zao na kuwarushia mashabiki hao. 
Ureno itakwaana na Ujerumani katika mchezo wao ufunguzi utakaochezwa kesho Jumatatu na inatarajiwa nyota huyo wa Real Madrid atashuka dimbani kuiongoza nchi yake katika pambano hilo.
Nchi hizo mbili zipo kundi moja na timu za Ghana na Marekani zitakazoumana baadaye usiku wa manane hiyo kesho.

Angeline Jolie atunukiwa tuzo za Malkia Elizabeth

WACHEZA filamu Daniel Day-Lewis na Angelina Jolie, wametukuzwa na Malkia Elizabeth wa Uingereza katika orodha anayotoa kila mwaka kuwatunza watu waliotoa mchango mkubwa kwa jamii.
Daniel Day-Lewis atapewa cheo cha Sir, na Angelina Jolie atapewa cheo cha Dame kwa kampeni yake ya kupambana na uhalifu wa ubakaji wa wanawake katika maeneo ya vita, pamoja na kazi zake nyengine kwa niaba ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi, UNHCR.
Na waandishi wawili wa BBC wamepata nishani ya OBE:
Lyse Doucet, mwandishi mkuu wa BBC katika maswala ya kimataifa, na Tin Htar Swe, mhariri wa Idhaa ya BBC ya lugha ya Burma.
Stephen Sutton, kijana wa miaka 19 aliyekufa karibuni kutokana na saratani, na wakati akiugua aliongoza mchango wa karibu dola milioni 7 kugharimia utafiti dhidi ya ugonjwa huo, ametunzwa MBE, (ambayo alipokea kabla ya kufariki mwezi uliopita.)
Mtunzi wa riwaya, Hilary Mantel, aliyeandika vitabu vilivyopata zawadi ya Booker, 'Wolf Hall' na 'Bring up the Bodies', piya amepewa hadhi ya Dame.
BBC

Wagosi wa Kaya kuteta Juni 22, yafanya kufuru ya usajili

MABINGWA wa zamani wa soka nchini, Coastal Union ya Tanga inatarajiwa kufanya Mkutano Mkuu wa wanachama Juni 22 kwenye ukumbi wa Hotel ya Mkonge, jijini Tanga, huku wakiwasainisha wachezaji kadhaa wapya na wa zamani kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa klabu hiyo, Oscar Assenga mkutano huo utakuwa na ajenda kuu mbili zitakazojadiliwa na mengineyo.
Assenga alisema ajenda ya kwanza itakuwa ni kupokea taarifa na kujadili taarifa za kazi kutoka kamati mbalimbali za utendaji ndani ya klabu hiyo kwa kipindi kilichopita.
Pia alisema kutakuwa na kuthibitisha bajeti kwa mwaka wa fedha unaofuata baada ya mwaka uliopita kumalizika ambapo mkutano huo hautaruhusu wanachama wanaodaiwa madeni kuhudhuria.
“Pia tutafanya marekebisho ya katiba kwani tutaongeza kifungu cha kamati ya maadili ambacho ni muhimu ikiwa ni agizo la TFF," alisema Assenga.
Afisa Habari huyo alitoa wito kwa wanachama wa klabu hiyo waliopo sehemu mbalimbali hapa nchini kuhakikisha wanatimiza haki yao ya msingi kwa kuhudhuria kwenye mkutano huo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya timu hiyo kongwe hapa nchini.
Mkutano huo unafanyika huku klabu hiyo ikiwa imeanza mchakato wa usajili wa wachezaji kwa msimu ujao wa Ligi Kuu ikiwasainisha wachezaji kutoka Mgambio JKT, ASAhanti United na wale iliyoikuwa nao msimu uliopita, licha ya kukimbiwa na aliyekuwa  mfadhili wao, Nassor BinSlum aliyeingia mkataba wa kuidhamini klabu ya Mbeya City kwa miaka mitatu.

Ivo Mapunda atoa darsa Kombe la Dunia

GOLIKIPA wa klabu ya Simba na timu ya taifa 'Taifa Stars', Ivo Mapunda, amesema wachezaji wa soka nchini wanapaswa kuzitumia fainali za kombe la Dunia zilizoanza juzi nchini Brazil kwa ajili ya kujifunza mambo mablimbali ya soka.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mapunda, alisema kuwa pamoja na kuwa Tanzania haishiriki kwenye fainali hizo lakini kuna nafasi kwa wachezaji kujifunza kitu kwenye michuano hiyo mikubwa Duniani.
"Hatupo kwenye fainali..., lakini tumepata fulsa ya kutazama fainali hizi kupitia luninga, tunaweza kama wachezaji kujifunza kitu kutoka kwa wenzetu," alisema Mapunda.
Alisema kuwa hata kwa viongozi wa soka nchini wanapaswa kujipanga na kuhakikisha mikakati thabiti inawekwa ili Tanzania ishiriki kwenye fainali hizo miaka ijayo.
Alisema kuwa Tanzania bado ipo nyuma kisoka ukilinganisha na nchi zinazoshiriki kwenye fainali za Dunia lakini bado ina nafasi ya kufikia kwenye uwezo wa kucheza kombe la Dunia.
"Hata hizo timu zinazoshiriki sasa hivi zilianza chini kabisa kama sisi, ila wenzetu walikuwa na mipango mizuri..., tupo nyuma sana lakini tunaweza," aliongezea kusema Mapunda.
Alisema kuwa kama hakutakuwa na mipango mizuri, Tanzania itaendelea kuwa wafuatiliaji kwenye luninga wa fainali za kombe la Dunia.

Bacary Sagna atua Manchester City kilaini akiikacha Arsenal

KLABU ya Manchester City imetangaza rasmi kumnasa beki Bacary Sagna kwa uhamisho huru kutoka klabu ya Arsenal. 
Beki huyo wa kimataifa wa Ufaransa amejiunga na mabingwa hao wa Ligi Kuu kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya kuthibitisha juzi kuwa hataongeza mkataba na Arsenal. 
Mustakabali wa beki huyo kubakia Arsenal umekuwa mashakani kwa kipindi kirefu baada ya kushindikana kufikiwa kwa makubaliano ya mkataba mpya aliokuwa akiutaka mchezaji huyo. 
Sagna mwenye umri wa miaka 31 ameungana na kiungo wa Porto Fernando ambao meneja wa City Manuel Pellegrini alikuwa akiwahitaji katika kipindi cha usajili wa majira ya kiangazi. 
Kuondoka kwa Sagna kunamuacha kocha Arsene Wenger kutafuta mbadala mpya katika nafasi ya beki wa kulia huku mchezaji wa Atletico Madrid JuanFran na nyota wa Toulouse Serge Aurier wakiwa wachezaji wanaotizamiwa kuziba pengo hilo.

Jahazi la timu ya Babi, UiTM lazama Malaysia

JAHAZI la timu ya UiTM ya Malaysia anayoichezea kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Kassim 'Babi'juzi lilizamishwa baada ya kucharazwa mabao 4-0 na timu ya DRB-Hicom katika mfululizo wa Ligi Kuu ya nchi hiyo.
Kipigo hichio kilichopatikana kwenye uwanja wa ugenini wa Hang Jebat, mjini Melaka imeifanya UiTM ambayo ilianza kuonyesha matumaini kwa kupata ushindi ushindi na sare mfululizo kiasi cha kuchupa toka nafasi za mkiani hadi nafasi ya 8 kusaliwa na pointi zao 20 baada ya mechi 19.
Timu hiyo itashuka dimbani kesho kujaribu bahati yao mbele ya timu kali ya PBAPP katika mfululizo wa ligi hiyo inayoelekea ukingoni kwa sasa.
Babi alisema walizidiwa mchezao na wapinzani wao na wanajipanga kwa mechi ya kesho nyumbani ili kuibuka na ushindi na kusogea nafasi za juu.

Hivi ndivyo Iraq Hudu 'Kimbunga' alivyopumzishwa makaburi ya Kisutu jana

Jeneza lililokuwa na mwili wa marehemu Iraq Hudu 'Mkumwena' wakipeleka mwili kuzika katika makaburi ya Kisutu Dar es salaam kwa ajili ya kumuhifadhi
Baadhi ya waombelezaji wakitia udongo katika kaburi la marehemu Iraq Hudu wakati wa maziko yaliyofanyika leo katika makaburi ya Kisutu Dar es salaam
Baadhi ya waombelezaji na mabondia wakiwa nyumbani kwa marehemu Iraq Hudu kutoka kushoto ni bondia Adwer George, Rashidi Matumla, Rais wa Oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini Yasini Abdallah na Mwenyekiti wa Shiwata Cassim Twalibu 
Mtoto wa Marehemu Iraq Hudu, Daniel Hudu  kushoto akisalimiana mabondia Adrwe George,Rashidi Matumla na Rais wa TPBO Yassin Abdallah
Mtoto wa Marehemu Iraq Hudu, Daniel Hudu  kushoto akisalimiana mabondia Adrwe George,Rashidi Matumla na Rais wa TPBO Yassin Abdallah
Mashekhe wakisoma duwa kabla ya kwenda kuzika
Meneja wa bendi ya msondo ngoma Said Kibiriti akisalimiana na mabondia
Baadhi ya waombelezaji waliojitokeza
Mtangazaji Maulid Baraka Kitenge akizungumza na mabondia mbalimbali wakati wa msiba wa bondia Iraq Hudu
Mtangazaji wa kipindi cha Michezo Maulid Baraka Kitenge akisalimiana na bondia mkongwe ambaye kwa sasa ni kocha wa MKoa wa Tanga katika wilaya ya Muheza Charles Mhillu 'Spinks'
Bondia Marehemu Iraq Hudu 'Kimbunga' kulia enzi za uhai wake katikati ni marehemu bondia Papa Upanga
Bondia Iraq Hudu' Kimbunga kulia akipambana na Stanley Mabesi katika mpambano wao
IRAQ HUDU
WAOMBWELEZAJI WAKIWA WAMEBEBA JENEZA LA MAREHEMU IRAQ HUDU
WAOMBWELEZAJI WAKIWA WAMEBEBA JENEZA LA MAREHEMU IRAQ HUDU
Mmoja wa waombelezaji kulia akimpa pole bondia Chuku Duso katika msiba wa bondia Iraq Hudu
Ibrahimu Kamwe na Said Chaku
wadau mbalimbali wa mchezo wa ngumi
WAOMBWELEZAJI WAKIWA WAMEBEBA JENEZA LA MAREHEMU IRAQ HUDU

WAOMBELEZAJI WAKITIA UDONGO KWENYE KABURI LA MAREHEMU IRAQ HUDU
WAOMBELEZAJI WAKITIA UDONGO KATIKA KABURI LA IRAQ HUDU
WAOMBELEZAJI WAKITIA UDONGO KATIKA KABURI LA IRAQ HUDU

Ivory Coast yaizima Japan, Balotelli aiua England

Balotelli akiiangamiza England

Andre Pirlo akonyesha ujuzi wake

Kitu


Danile Sturridge akishangilia bao lake aliloifungia England


Kitu jamaniiiGervinho akishangilia bao lake la ushindi na wachezaji wenzake wa Ivory Coast

Yaya Toure akiwatesa wachezaji wa Japan alfajiri ya leo wakati wakiibuka na ushindi wa 2-1

WAWAKILISHI wa Afrika kwenye Kombe la Dunia, Tembo ya Ivory Coast wamewatoa kimasomaso Waafrika baada ya alfajiri ya leo kuifumua Japan mabao 2-1 huku England wakiendelea kuwa wateja kwa Italia kwa kuzabuliwa idadi katika hiyo katika mfululizo wa fainali hizo zinazofanyika nchini Brazil.
Ushindi wa Ivory umewapoza waafrika ambao waliishuhudia timu yao nyingine Cameroon ikianza vibaya kwa kichapo cha bao 1-0 toka kwa Mexico katika mechi ya kundi A.
Mabao ya Wilfried Bony na Gervinho katika kipindi cha pili kimeifanya timu hiyo kutoka nyuma ilipotanuliwa kufungwa na Japasn na kuvuna pointi tatu zao za kwanza katika michuano hiyo ya Dunia ikiwa nyuma ya Colombia inayoongoza kundi C baada ya kuitandika Ugiriki mabao 3-0.
Japan waliwashtua Tembo hao wa Ivory Coast walipojipatia bao la kuongoza katika dakika ya 16 Keisuke Honda na kudumu hadi mapumziko.
Hata hivyo kipindi cha pili Ivory Coast walijipanga na kurejesha bao hilo dakika ya 64 kupitia Bony na dakika mbili baadaye Gervinho alimalizia udhia kwa kufunga bao la ushindi.
Katika mechi nyingine iliyochezwa usiku wa manane, Italia iliendelea kuitesa England kwa kuicharaza mabao 2-1 katika pambano lililokuwa kali na la kusisimua.
Mario Balotelli ndiye aliyekuwa mwiba wa England baada ya kufunga bao la pili na la ushindi dakika tano baada ya kuanza kwa kipindi cha pili na kuzima ndoto za vijana wa Hodgsons kulipa kisasi cha kung'olewa kwenye robo fainali ya Kombe la Ulaya.
Italia walionyesha dalili za kuibuka na ushindi mapema baada ya Claudio Marchiso kufunga bao dakika ya 34 kabla ya Daniel Sturridge kusawazisha dakika tatu baadaye na kuzifanya timu hizo zienda mapumziko zikiwa nguvu sawa ya kufunga bao 1-1.
Ndipo katika kipindi cha pili Mario Balotelli alipodhihirisha kuwa yeye ni mchezaji muhimu katika kikosi cha Azzurri alipofunga bao la pili lililoiweka Italia katika nafasi ya pili katika kundi D nyuma ya Costa Rica iliyoifumua Uruguay kwa mabao 3-1 mapema jana.
Michuano hiyo itaendelea tena siku ya leo kwa michezo ya kundi E ambapo itaumana na  Ecuador kabla ya Ufaransa kushuka dimbani kupepetana na Hondurus na pambano jingine la usiku wa manane litazikutanisha timu za kundi F Argentina dhifi ya Bosnia-Herzegovina.