Balotelli akiiangamiza England |
Andre Pirlo akonyesha ujuzi wake |
Kitu |
Danile Sturridge akishangilia bao lake aliloifungia England |
Kitu jamaniii |
Gervinho akishangilia bao lake la ushindi na wachezaji wenzake wa Ivory Coast |
Yaya Toure akiwatesa wachezaji wa Japan alfajiri ya leo wakati wakiibuka na ushindi wa 2-1 |
WAWAKILISHI wa Afrika kwenye Kombe la Dunia, Tembo ya Ivory Coast wamewatoa kimasomaso Waafrika baada ya alfajiri ya leo kuifumua Japan mabao 2-1 huku England wakiendelea kuwa wateja kwa Italia kwa kuzabuliwa idadi katika hiyo katika mfululizo wa fainali hizo zinazofanyika nchini Brazil.
Ushindi wa Ivory umewapoza waafrika ambao waliishuhudia timu yao nyingine Cameroon ikianza vibaya kwa kichapo cha bao 1-0 toka kwa Mexico katika mechi ya kundi A.
Mabao ya Wilfried Bony na Gervinho katika kipindi cha pili kimeifanya timu hiyo kutoka nyuma ilipotanuliwa kufungwa na Japasn na kuvuna pointi tatu zao za kwanza katika michuano hiyo ya Dunia ikiwa nyuma ya Colombia inayoongoza kundi C baada ya kuitandika Ugiriki mabao 3-0.
Japan waliwashtua Tembo hao wa Ivory Coast walipojipatia bao la kuongoza katika dakika ya 16 Keisuke Honda na kudumu hadi mapumziko.
Hata hivyo kipindi cha pili Ivory Coast walijipanga na kurejesha bao hilo dakika ya 64 kupitia Bony na dakika mbili baadaye Gervinho alimalizia udhia kwa kufunga bao la ushindi.
Katika mechi nyingine iliyochezwa usiku wa manane, Italia iliendelea kuitesa England kwa kuicharaza mabao 2-1 katika pambano lililokuwa kali na la kusisimua.
Mario Balotelli ndiye aliyekuwa mwiba wa England baada ya kufunga bao la pili na la ushindi dakika tano baada ya kuanza kwa kipindi cha pili na kuzima ndoto za vijana wa Hodgsons kulipa kisasi cha kung'olewa kwenye robo fainali ya Kombe la Ulaya.
Italia walionyesha dalili za kuibuka na ushindi mapema baada ya Claudio Marchiso kufunga bao dakika ya 34 kabla ya Daniel Sturridge kusawazisha dakika tatu baadaye na kuzifanya timu hizo zienda mapumziko zikiwa nguvu sawa ya kufunga bao 1-1.
Ndipo katika kipindi cha pili Mario Balotelli alipodhihirisha kuwa yeye ni mchezaji muhimu katika kikosi cha Azzurri alipofunga bao la pili lililoiweka Italia katika nafasi ya pili katika kundi D nyuma ya Costa Rica iliyoifumua Uruguay kwa mabao 3-1 mapema jana.
Michuano hiyo itaendelea tena siku ya leo kwa michezo ya kundi E ambapo itaumana na Ecuador kabla ya Ufaransa kushuka dimbani kupepetana na Hondurus na pambano jingine la usiku wa manane litazikutanisha timu za kundi F Argentina dhifi ya Bosnia-Herzegovina.
No comments:
Post a Comment