![]() |
| Kamanda Kova |
Akihojiwa muda mfupi na kituo cha TBC1, Kamanda Kova alisema kuwa usambazaji wa taarifa juu ya kundi hilo zimekuzwa sana na kuleta hofu kutokana na uvumi uliosambazwa na kuwataka wananchi wasiwe na hofu.
Kamanda Kova alisema jeshi la Polisi limedhibitiwa tangu walipoanzisha fujo zao na wawili walishatiwa mbaroni na sasa wanaendelea kuwataja wenzao ili kuwasaka walioibua taharuki hiyo.
"Uvumi huu wa kutumiana meseji na kutumia mitandao ya kijamii imeleta taharuki na kukuza jambo kinyume na uhalisia, lakini nataka kuwamabia wakazi wa Dar wasiwe na hofu jeshi la Polisi limewadhibiti na vijana wapo kazini kuhakikisha mambo yanaendelea kuwa shwari,'" alisema Kamanda Kova.
Tangu jioni kulikuwa na taarifa za kuwepo kwa matukio ya uporaji na uvamizi uliokuwa ukidaiwa kufanywa na Panya Road, ingawa DC wa KIinondoni, Jordan Rugimbana alifafanua mapema kabla ya Kamnada Kova kumaliza utata hivi punde. akisisitiza kuwa Dar ni shwari na watu walale kwa amani na utulivu kwa kuwa yeye Kamanda na vijana wake wapo kazini na Panya Road au wahalifu wengine hawawezi kuwazidi ujanja.
.jpg)
PAMBANO la Kombe la Mapinduzi kati ya Yanga na Taifa Jang'ombe limeisha kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 4-0, huku Simon Msuva aliyeifungia mabao matatu akichaguliwa kuwa Man of the Match sambamba na kuondoka na mpira..png)
.png)
.png)
.png)
.png)
.png)
HABARI kutoka Zanzibar kwa sasa kwenye mfululizo wa michuano ya Kombe la Mapinduzi,, Yanga wapo mbele kwa mabao 3-0 dhidi ya Jang'ombe.
KIPIGO cha mabao 5-3, kimeendelea kumuuma Kocha wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho ambapo amenukuliwa akidai anaamini kikosi chake kingeweza kuichapa Tottenham Hotspurs kama wangezawadiwa penati ambayo ingewafanya kuongoza katika mchezo huo.








MMILIKI wa klabu ya Wigan Athletic Dave Whelan amefungiwa kwa wiki sita kujishughulisha na masuala yeyote ya michezo na kutozwa faini ya paundi 50,000 kwa kutoa kauli ya kibaguzi kuwalenga watu wenye asili ya Uyahudi na Wachina. 

