STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, January 2, 2015

Lampard awakera Wamarekani kuamua kubaki Manchester City

http://assets.nydailynews.com/polopoly_fs/1.1947373!/img/httpImage/image.jpg_gen/derivatives/article_970/lampard22s-1-web.jpg
Add caption

KITENDO cha kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya England, Frank Lampard ya kuongeza muda wa kuendelea kuichezea Manchester City kwa mkopo hadi mwisho wa msimu "umewachefua" mashabiki wa timu yake mama ya New York City FC inayoshiriki ligi kuu ya Marekani.
Lampard awali alijiunga na Man City kwa mkopo wa miezi sita akitokea New York City FC baada ya kuondoka Chelsea mwisho wa msimu uliopita.
Lakini dili lake na klabu hiyo ya England, ambayo kwa sasa ni ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England, limeongezwa hadi Mei au Juni, jambo linalomaanisha kwamba kiungo huyo mwenye umri wa miaka 36 atakosa miezi mitatu ya kwanza ya msimu mpya wa ligi ya MLS.
"Tunapenda kupinga hadharani... maamuzi ya Frank Lampard kuongeza muda wake wa kucheza kwa mkopo Manchester City hadi mwisho wa msimu wa Ligi kuu ya England," umoja wa mashabiki wa New York City wajiitao 'Third Rail' ulisema katika taarifa yao.
"Mashabiki wengi, wakiwamo wanachama, wameamua kuisapoti timu,kununua tiketi za msimu, na kununua bidhaa za timu zikiwamo jezi kutokana na imani kwamba Frank Lampard ataichezea New York City Football Club, siyo Manchester City."
"Mashabiki wengi kati ya hao wamekerwa na maamuzi hayo, na tunasapoti hatua zozote watakazochukua katika kupinga maamuzi haya.
"Tunapinga mitazamo ya aina yoyote kwamba sisi NYCFC ni watoto wa Manchester City FC, bila ya kujali chanzo, na tumefadhaishwa na jumuiya ya City Football Group kuweka mtazamo huo."
New York City inamilikiwa kwa pamoja na klabu za Manchester City na timu ya baseball ya New York Yankees na itatumia Uwanja wa Yankee kama uwanja wake wa nyumbani wakati msimu wa 2015 wa ligi ya MLS utakapoanza Machi.
Lampard (36) ameifungia Man City magoli sita na tarehe ya kujiunga kwake New York City itategemea mechi ya mwisho ya Man City.
Ligi Kuu ya England itamalizika mwisho Mei 24, wakati mechi ya fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya itachezwa Juni 6. Manchester City itawavaa Barcelona katika mechi ya 16-Bora ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment