KLABU ya Liverpool ni
moja ya vilabu kadhaa vinavyotarajiwa kufanyiwa uchunguzi kama wamekiuka
Sheria ya Matumizi ya Fedha-FFP.Kwa mujibu wa sheria za Shirikisho la Soka barani Ulaya-UEFA vilabu vyote barani humo vinapaswa kuweka kikomo cha hasara kutofikia paundi milioni 35.4 kwa misimu miwili.
Kuna adhabu hutolewa kwa wasiotimiza masharti hayo ambapo Manchester City tayari wameshakumbana nayo kwa kutozwa faini na kuwekewa kiwango cha matumizi katika usajili na kupunguziwa idadi ya wachezaji katika kikosi chake Mei mwaka huu.
Lakini pamoja na kupata hasara ya paundi milioni 49.8 katika msimu wa mwaka 2012-2013 na paundi milioni 41 msimu wa mwaka 2011-2012, Liverpool wana uhakika wanaweza kuvuka kikwazo hicho bila adhabu.
Liverpool sambamba na Monaco, Inter Milan na AS Roma ambazo zote hazikushiriki michuano ya Ulaya msimu uliopita tayari zimepeleka taarifa za akaunti zao Bodi ya Udhibiti wa Fedha ya Klabu-CFCB lakini kuna uwezekano wa kuagizwa kupelekea maelezo zaidi kuhusu fedha hizo.
Msimu uliopita vilabu 76 viliingia katika uchunguzi wa FFP lakini vilabu tisa pekee ndio vilipewa adhabu kwa kukiuka sheria hiyo.




NCHI ya Algeria imeamua kujitosa kuwania uenyeji wa Fainali za Afrika, AFCON 2017 baada ya kukosa nafasi ya uandaaji wa fainali za 2019, 2021 na
2023.
MENEJA wa klabu ya
Arsenal, Arsene Wenger amesema anategemea Per Martesacker na Kieran
Gibbs kurejea katika kikosi chake katika mchezo wa Jumamosi
dhidi ya mahasimu wao wa kaskazini mwa London
Tottenham Hotspurs.
CRISTIANO Ronaldo alifunga magoli manne katika ushindi wa Real Madrid wa 5-1 dhidi ya Elche katika Ligi Kuu ya Hispania juzi na kuwa 'hat-trick' yake ya 25 kwa Real Madrid.