STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, September 25, 2014

Aisha Bui awaandalia mashabiki wake 'Asante' kumpokea

Aisha Bui katika pozi tofauti
NYOTA wa filamu nchini, Aisha Fat'hi  a.k.a Aisha Bui, yupo kwenye maandalizi ya kufyatua kazi mpya baada ya filamu yake ya 'Mshale wa Kifo' kufanya vyema sokoni.
Akizungumza na MICHARAZO, Aisha alisema anashukuru namna mashabiki walivyoipokea filamu yake hiyo ya kwanza kuitengeneza mwenyewe kupitia kampuni ya Bad Girl Entertainment na katika kuonyesha shukrani zake anajiandaa kuwatengenezea filamu nyingine kali zaidi.
Aisha alisema ingawa ni mapema kwa sasa kutaja jina la filamu hiyo, lakini alisema itawashirikisha wasanii kadhaa nyota kama alivyofanya katika 'Mshale wa Kifo' aliowashirikisha kina Mzee Chillo, Gabo na wengine.
"Nipo katika maandalizi ya kutengeneza filamu nyingine mpya, hii kama 'Mshale wa Kifo' itashirikisha pia wakali mbalimbali wa filamu nchini, lengo ni kuwapa burudani mashabiki wangu walioniunga mkono kupitia kazi yangu ya kwanza kuizalisha mwenyewe," alisema Aisha.
Kabla ya kutengeneza filamu yake mwenyewe, alishafanya vema katika filamu za wenzake zikiwamo za 'Saturday Morning', 'The Second Wife', 'Better Days', 'Not Without My Son', 'Continous Love', 'Revenge of Love', 'Mirathi', 'Pain of Love' na 'Crazy Love'.

No comments:

Post a Comment