IMEFAHAMIKA kuwa klabu ya Manchester United wana mpango wa kumrejesha Gerard Pique Old Trafford akitokea Barcelona.
Mlinzi
huyo aliondoka United mwaka 2008 kwa uhamisho uliogharimu pauni milioni
£5 ambapo amekuwa mchezaji wa kutumainiwa Katalunya tangu wakati huo
ambapo ameisaidia kutwaa mataji manne ya ligi ya Hispania 'La Liga'
mataji mawili ya ligi ya mabingwa Ulaya na mawili ya Copa del Reys.
Hata
hivyo nyota huyo wa kimataifa wa Hispania mpaka sasa ameitumikia timu
yake michezo mitatu tu huku bosi mpya wa Barcelona Luis Enrique
akionekana kupendelea zaidi kumtumia Javier
Mascherano na Jeremy Mathieu katika sehemu ya ulinzi.
Kwa
mujibu wa gazeti moja la nchini Hispania la AS limearifu kuwa
Manchester United inataka kutumia mwanya huo kuweka pendekezo la kutaka
kumsajili Pique kurejea Old Trafford, licha ya kwamba mlinzi huyo mwenye
umri wa miaka 27 akiwa ndio kwanza amesaini mkataba wa nyongeza na
Barca.
Bosi
Louis van Gaal kwasasa analazimika kusaka namna ya kuimarisha eneo la
ulinzi katika kikosi chake mwezi Januari wakati huu ambapo United ikiwa
imekusanya alama tano tu katika michezo mitano tangu kuanza kwa msimu
mpya wa Premier League huku ikiwa tayari imeshatolewa katika kombe la
Capital One na MK Dons.
No comments:
Post a Comment