STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, September 25, 2014

Simba yapata pigo, Ivo, Kiongera kuikosa Yanga Okt 12

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj8__24SqlWkKjcX7F8kwlm9XNcJcmuX00g5LSeJnhkhyvDdgaA_LOv5ObDUcs7DcWxwbUMiMiTANgKbV434hiewe8cAlv0KlOHhyuP0g6sM4YhdkxIkgyI8l30SjnEcyw_ja49lQ9HlEI/s1600/ivo.jpg 
WIKI mbili kabla ya kuvaana na watani zao, Yanga klabu ya Simba imepata pigo baada ya kipa wake namba moja, Ivo Mapunda kuvunjika kidole na hivyo kuwa nje ya dimba kwa wiki nane.
Kwa mujibu wa taarifa za klabu hiyo Ivo amevunjika kidole mazoezini Zanzibar jana asubuhi na anatakiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki nane.
Kuumia huko kunamfanya asiweze kusimama langoni wakati  wa pambano la watani wa jadi la Simba na Yanga la Oktoba 12.
Daktari wa Simba SC Yassin Gembe amenukuliwa akisema Ivo aliumia wakati anachupia mpira katika mazoezi ya asubuhi na kwa bahati mbaya mpira ukamgonga kwenye kidole kidogo cha mwisho mkono wa kulia.
Gembe amesema Ivo alitoka mazoezini baada ya tukio hilo na baadaye akapelekwa hospitali ya Mnazi Mmoja kisiwani humo ambako baada ya vipimo ikagundulika amevunjika sana.
"Si kuvunjika kwa mzaha, amevunjika sana na anatakiwa kupumzika kwa wiki nane, baada ya hapo aanze taratibu… ina maana makadirio ya kurudi tena uwanjani ni hadi baada ya miezi mitatu" – Gembe.
Kuumia kwa Ivo kunatoa nafasi kwa makipa chipukizi Hussein Sharrif  ‘Cassilas’ na Peter Manyika kujibidiisha ili kuziba pengo lake ambapo sasa Ivo anafanya idadi ya wachezaji majeruhi ambao ni tegemeo Simba kufikia wanne baada ya Paul Kiongera anayetakiwa kuwa nje wiki sita, Haroun Chanongo na Issa Rashid ‘Baba Ubaya’.

No comments:

Post a Comment