STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, September 25, 2014

Arsene Wenger apumua Arsenal wakijiandaa kuivaa Spurs

http://4.bp.blogspot.com/-xR7WWLG8rfg/UXvRcY5R4uI/AAAAAAAACCs/RYm0E5WSDtc/s1600/guar.jpgMENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema anategemea Per Martesacker na Kieran Gibbs kurejea katika kikosi chake katika mchezo wa Jumamosi dhidi ya mahasimu wao wa kaskazini mwa London Tottenham Hotspurs. 
Majeraha madogo madogo yalipelekea Martersacker na Gibbs kukosa mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya Southampton na kupelekea Wenger kuwatumia mabeki wasio wazoefu akiwemo Hector Bellerin na Isaac Hayden. 
Kukosekana kwa Nacho Monreal kunamaanisha Calum Chambers ndio mchezaji pekee katika safu ya ulinzi mwenye uzoefu aliyechezeshwa na Wenger lakini kinda huyo amecheza katika mechi saba pekee za Arsenal toka alipojiunga akitokea Southampton. 
Katika mchezo huo Arsenal walitandikwa nyumbani mabao 2-1 na Southampton lakini Wenger ana uhakika kuwa mabeki wake wazoefu Matersacker na Gibbs watakuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi. 
Safu ya ulinzi ya Arsenal ilizidi kupungua baada ya taarifa za Jumatatu kuwa beki wa kimataifa wa Ufaransa Mathieu Debuchy atakosekana dimbani kwa miezi mitatu kufuatia kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu wake wa kushoto.

No comments:

Post a Comment