STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, February 13, 2015

VALENTINE DAY NI KITU GANI, JE UISHEREHEKEE?

KESHO baadhi ya watanzania wataingia kwenye mkumbo wa kusherehekea siku iliyobatizwa jina la 'Valentine Day' wakiitaja kama Siku ya Wapendanao.
Kwa hakika kwa Mcha Mungu ni haramu kwake kuiadhimisha sherehe hiyo kutokana na ukweli ni siku ya KIPAGANI na inayokinzana na MAFUNDISHO YA MUNGU MWENYEEZI iwe kwa Ukristo ama kwa Uislam.
Hata hivyo ni vema tuongelee kidogo nini maana ya Valentine kwa asili yake kisha kila mtu kwa IMANI  yake na mapana yake akatambua na kujiamulia kwa nafsi yake ama kukufuru au kumshukuru aliyemuumba.


Maneno hayo aliyoyasema Mtume Muhammad (SAW) hakika yamethibiti kwa sababu imedhihirika Waislamu kuigizia mila, desturi na tabia za makafiri na kuzisherehekea kama mfano siku hii inayoitwa 'Valentine day' (Siku ya Wapendanao).
Na baya zaidi na la kusikitisha sana ni kwamba sherehe hizi zinaenezwa katika njia mbali mbali za mawasiliano kama kutumiana kadi, barua pepe (e-mail), salamu katika simu za mkono. 
Hakika fitna hii humfanya Muislamu aharibu 'Aqiydah (Iymaan) yake kwa kudhani kuwa anafanya jambo la kawaida na hali ni jambo lisilo katika sheria ya dini yetu bali ni shirki kubwa na upotofu wa kufuata wanayoamini makafiri.
Na Mwenyezi Mungu anasema kuwa "Hawatakuwa Radhi Mayahudi na Manaswara kuwaona mpaka mfuate mila zao"
Baadhi ya Waislam na wasio waislam wapo kwenye harakati za kujiandaa na siku hiyo wajifuata mkumbo bila kujua kile wanachokisherehekea ebu tujifunze;
Historia Ya Sherehe Ya Siku Ya ValentineSherehe hii ya wapendanao ni sherehe ya wapagani  wa Kirumi wakati dini yao ya upagani ilikuwa ni dini iliyotapakaa kwa Warumi karne zaidi ya kumi na saba zilizopita.  
Na fikra zao ilikuwa ni kuelezea hisia ya 'mapenzi ya kiroho'
Kulikuwa na visasili (uongo) zilizohusishwa na sherehe hii ya upagani ya Warumi ambao umeendelea kutoka warithi wa Kikiristo. 

Miongoni mwa uongo huo ni kuamini kwao Warumi kuwa Romulus, aliyevumbua Rome, alinyonyeshwa siku moja na mbwa mwitu mwanamke, hivyo akampa nguvu na hikma.
Warumi walikuwa wakisherehekea tukio hili katikati ya Februari kila mwaka kwa kufanya sherehe kubwa. 

Na mojawapo ya tambiko katika sherehe hii ni kuchinja mbwa au mbuzi. 
Vijana wawili wenye nguvu hujipaka damu ya mbwa au ya mbuzi katika miili yao, kisha huiosha damu hiyo kwa maziwa. 
Baada ya hapo, watu hufanya gwaride wakiwa vijana hawa wawili wako mbele wakiongoza gwaride iliyokuwa ikitembea barabarani. 
Vijana hao wawili walikuwa wakichukua vipande vya ngozi ambavyo waliwapigia watu wanaowavuka. Wanawake wa kirumi walikuwa wakipokea mapigo hayo wakiamini kuwa yatawahifadhi na kutibu utasa.
 

Kufungamana kwa Mt. Valentine na Sherehe Hii

Mtakatifu Valentine (Saint Valentine) ni jina waliopewa mashujaa wawili wakongwe waliokufa ambao ni wana wa kanisa la kikiristo. 

Inasemekena kwamba walikuwa ni wawili au mmoja tu. 
Huyo mmoja alikufa Rome kutokana na mateso ya kiongozi wa Kigothi aliyeitwa Claudius. 
Kanisa la Saint Valentine lilijengwa kwa ajili ya kudumisha kumbukumbu yake.
Warumi walipoingia ukristo, wakaendelea kusherehekea sikukuu ya wapendanao (valentine day) lakini wakabadilisha kutoka fikra ya upagani ya 'mapenzi ya kiroho' (spiritual love) na kuleta fikra nyingine iliyojulikana kama ni 'mapenzi ya mashujaa' yaliyowakilishwa na Saint Valentine ambaye aliuliwa kwa ajili ya kutetea mapenzi na amani. 

Vile vile ikajulikana ni sikukuu ya wapenzi, na Saint Valentine alifanywa kuwa ni mlezi wa mapenzi ya mtakatifu.
Miongoni mwa imani yao inayoambatana na sherehe hii ni kwamba majina ya wasichana waliofika umri wa kuolewa yaliandikwa katika vikaratasi vidogo vilivyokunjwa mviringo kisha vikawekwa katika chombo juu ya meza. 

Kisha wavulana waliotaka kuoa waliitwa na kila mmoja huchagua karatasi moja ikiwa na jina la msichana. Kisha hujiambatanisha naye huyo msichana aliyempata kutokana na kura hiyo aliyochagua kwa muda wa mwaka ili wajuane vizuri kisha tena hufunga ndoa, au kama hawakuelewana hurudia tena kufanya kura inapofika siku hiyo mwaka unaofatia.  
Vile vile imesemekana kwamba chanzo cha sikukuu hii, ni kwamba warumi walipokuwa wakristo baada ya ukristo kutapakaa, Mfalme wa Kirumi Claudius II alitoa hukumu katika karne ya tatu kwamba askari wasioe kwa sababu kuoa kwao kutawashughulisha na vita walivyokuwa wakipigana. 

Hukumu hiyo ilipingwa na Saint Valentine ambaye alianzisha kuozesha maaskari kwa siri. 
Alipokuja kujua mfalme, alimfunga jela na akamhukumu kuuliwa. 
Huko jela akapendana na mtoto wa mkuu wa jela, lakini ikawa ni siri kwani kutokana na sheria ya ukristo, mapadri na makasisi wameharamishwa kuoa au kupenda.
Hata hivyo alipewa heshima yake na wakristo kwa sababu ya kushikilia na kujikita imara katika ukristo wakati mfalme alipotaka kumsamehe kwa sharti aache ukristo na kuabudu miungu ya Kirumi ili awe msiri wake na awe mkwe wake. 

Lakini Saint Valentine alikataa ahadi hiyo na akapendelea ukristo, kwa hiyo akauliwa siku ya tarehe 14 Februari 270 CE. 
Ndio ikaitwa siku hii kwa jina la huyo mtakatifu (Valentine).

Papa (Pope) naye akaifanya siku hiyo ya kufa Saint Valentine tarehe 14 Februari 270 CE kuwa ni sikukuu ya mapenzi. 

Na ni nani alikuwa Papa huyo? Ni Askofu mkuu wa kanisa la 'universal church', ambaye ni mrithi wa mtakatifu Peter.
Ndugu Waislamu tazameni vipi huyo askofu anavyohusika katika kuadhimisha sikukuu hii ambayo ni uzushi katika dini yao ya Kikiristo. 


Hii itukumbushe kauli ya Allaah
"Wamewafanya makuhani wao na wamonaki wao kuwa ni marabi badala ya Mwenyezi Mungu"At-Tawbah: 31

Matendo Yanayotakiwa Kujiepusha Katika Sikukuu Hii  
1- Kuonyeshana bashasha na furaha kama ilivyo katika sikukuu zao nyingine.
2-Kupeana mawaridi mekundu (Red Roses) ambayo ni alama ya kuelezea mapenzi, 'mapenzi ya kiroho' ya wapagani au 'mapenzi' ya Wakristo. Hivyo inajulikana kuwa ni 'Sikukuu Ya Wapendanao'.
3-Kupelekeana kadi. Na kadi nyingine zina picha za 'mungu wa mapenzi wa kirumi' ambaye ana mbawa mbili, akiwa amekamata upinde na mshale. Huyu ndio mungu wa mapenzi wa wapagani warumi. Shirk iliyoje hii ndugu Waislamu?
4-Kubadilishana maneno ya mapenzi na matamanio katika kadi wanazopelekeana, yakiwa katika mfumo wa kimashairi, tenzi na sentensi fupi fupi. 

Kadi nyingine zina picha za kimzaha na maneno ya kuchekesha, na mara nyingi zina maneno ya kusema 'Kuwa Valentine wangu'. 

Hii inaashiria maana ya kikiristo ya sikukuu hii baada ya kuwa asili yake ni kutokana na fikra za upagani.
5-Katika nchi nyingi za kimagharibi, hufanyika sherehe siku hiyo ambayo kunakuweko kuchanganyika wanaume na wanawake, kuimba, na kucheza dansi. Na wengi wanapelekeana zawadi kama mawaridi, maboksi ya chokoleti kwa wake zao, marafiki na wanaowapenda.
Kutokana na maelezo yote hayo ya chanzo cha sikukuu hii, tunaona kwamba siku hiyo haina uhusiano wowote katika Uislamu, bali yana uhusiano na washirikina mapagani, hata wakristo katika dini yao nao pia ni uzushi, sasa itakuwaje sisi Waislamu tuwaigize kusherehekea?
Basi ndugu Waislamu tutambue kuwa jambo hili ni ovu mno, haimpasi Muislamu kuharibu 'Aqiydah (iymaan) yake kwani kuna hatari kubwa kushiriki katika sherehe hii nayo ni kuingia katika kumshirikisha Allaah na kama tunavyojua kuwa Allaah Hamsamehe mtu anayefanya shirki pindi akifariki bila ya kutubu kama ilivyo katika aya ifuatayo:
"Hakika Mwenyezi Mungu Hasamehe kushirikishwa, na Husamehe yaliyo duni ya hilo kwa Amtakaye. Na anayemshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa" (An-Nisaa: 48).
Hivyo ni kuharamishwa na Pepo na kupata makazi ya moto, tunajikinga na Allaah kwa hayo.
"Kwani anayemshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu Atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na waliodhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru"-Al-Maaidah: 72.
Tunamuomba Allaah  Atuepushe na kila aina ya shirk na Atuonyeshe yaliyo ya haki tuyafuate, na yaliyo ya batili tujiepushe nayo na Atuajaalie ni miongoni mwa wale wanaosikiliza kauli (nyingi) wakafuata zile zilizo njema.  Aamiyn

Special Al Hidaya

Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin
Friday, 13 February 2015 VALENTINE NI NINI? Leo nimeona niongelee kidogo nini maana ya Valentine kwa asili yake kisha kila mtu kwa Imani yake na mapana yake akatambua kuwa anapokuwa sehemu ya Valentine Day anakuwa ana adhimisha nini na kwa sababu gani wengi tunasheherekea kama sio kuadhimisha Valetine Pasipo kujua asili yake. Valentine’s Day kama Sikukuu Ya Kipagani: Valentine’s Day si siku ya Sikuu ya Kikristo, hata kama jina lake asili yake inatokana na Ukristo haiwezi kuhalalisha sasa Valentine kuwa Siku Ya Kikristo. Tukiangalia suala sikukuu hii kwa jicho la tatu, hatuoni uhusiano mkubwa kati ya watu wa Mungu na Malove dove yaani mapenzi. Kuna mambo mengi yanaweza ibua mjadala na kutokuelewana miongoni mwa jamii ya wakristo na wasomi juu ya chimbuko ya Siku ya wapendanao al maarufu Valentine’s Day. Hatutaweza kamwe kuwa na uwezo wa kuwa na jibu muafaka kuhusu uhalali wa kusheherekea valentine kwa namna moja ama nyingine kutokana na tofauti za kitamaduni na kidini ili mwisho wa siku tujenga upya hadithi kamili na madhubuti, lakini uhusiano kipagani hadi sasa na nguvu zaidi kuliko wale wa Kikristo kwa namna yoyote ile. Februari 14 & Juno Fructifier au Juno Februata (February 14th & Juno Fructifier or Juno Februata) Enzi hizo Warumi walikuwa wakisheherekea kwa kupumzika kabisa kama sikukuu ya muungano ama sikukuu zozote za hapa bongo kila Februari 14 kama siku ya kutoa heshima kwa Juno Fructifier. Huyu Juno Fructifier alikuwa nani?huyu alikuwa Malkia wa miungu ya Kirumi ambaye alikuwa Mungu mke kama mmoja wapo wa miungu ya ndoa kama ndo zilikuwa zinasua sua basi tarehe 14 February ndo ilikuwa kama siku ya kufanya matambiko. Enzi hizoilikuwa Katika sherehe moja, wanawake walikuwa wakiwasilisha majina yao na kuweka kwenye kisanduku na baadae wanaume wangepita mbele ya kisanduku hicho na kila mmoja kujitwalia jina moja. Kilichokuwa kinatokea katika sherehe kila aliyejiokotea jina hulitaja na kujitwalia huyo mwanamke kuwa mwanandoa kwa muda wote wa sikukuu wakati mwingine ilikuwa ni mwanandoa wako kwa mwaka mzima mpaka Valentine nyingine akaweke jina pale kwenye kibox. Mila hii ilitumika kukuza Jamii ya Kirumi kwa maana ya uzazi na maisha mengine kwa ujumla, kasheshe kama ulibeba ile ya mwaka mzima then Valentine imefika kisha unataka kubadilisha halafu uliyembeba mwaka jana mjamzito tehe tehe imekula kwako. St Valentine, Padri Wa Kikristo (St. Valentine, Christian Priest) Kulingana na hadithi za zamani, Mfalme wa Kirumi mwenye jina Claudius II ilipiga marufuku juu ya ndoa kwa sababu enzi hizo vijana wengi walikuwa wakiojitwalia wake mapema ili kukimbia jeshi maana amri ilikuwa mtu ambaye hana mke hana familia ndo alikuwa anapaswa kuingia jeshini maana hana cha kupoteza yuko mwenyewe tuy tehe tehe. Sasa kuna Padri mmoja wa Kikristo aitwaye Valentinus yeye ndo alikuwa kazi yake kufungisha hizo harusi kisirisiri maana inaonekana walikiuwa wakimpoza na mwisho wa siku huyu padri akahukumiwa kunyongwa. Wakati akisubiri kunyongwa, Wapenzi Vijana (Couples) walimtembelea na kumwandikia kitu kama barua kama sio waraka kuwa ni namna gani ndo ni tamu kuliko Vita ya kwanza vya dunia na vya pili. Valentine Mwingine. Valentinus mwingine alikuwa Padri nae alifungwa jela kwa ajili ya kusaidia Wakristo. Wakati akiwa bado yuko jela huyu kuhani aka fall in love na binti mlinzi wa gereza na wakati karibu anakwenda kunyongwa akaandika ujumbe “From Your Valentine” . Habari zake zikahifadhiwa na kuripotiwa Papa Julius I na baadae alijenga nakshi nakshi juu ya kaburi lake. Wakristo Wajibinafsishia Valentine’s Day: Katika mwaka wa 469 wa kutawala kwake Gelasius alitangaza Februari 14 siku takatifu kwa heshima ya Valentinus tajwa hapo juu badala ya kuwa siku ya kipagani ya mungu Lupercus wa Kirumi. Hapa ndo Wakristo wa enzi hizo wakachakachua sikukuu hiyo na kuruhusu kuchukua baadhi ya maadhimisho ya siku ya mapendo na ngono ambapo awali mambo hayo yalikuwa katika mazingira ya upagani. Si ajabu kwenye Valentine hii ukaona Guest House zimejaa, madukani watu wananunua condom hawajui kuwa kuadhimisha huko hawajaanza wao ila ni zile imani za kipagani. Maadhimisho ya kipagani yalikuwa lazima yaitimishwe kwa tendo la ngono ili kuonesha kilele cha upendo. Na njia rahisi iliyokuwa ikitumika katika kusheherekea siku hii ni ile ya kuweka majina kwenye kibox kisha kilaini unajibebea huku “mungu” Shahidi akisimamia zoezi zima. Kwa maana ya kwamba hakuna mtu atakaye okota jina bahati mbaya kuna roho inayomuongoza mtu kuchagua jina fulani. Valentine Day Yageuka kuwa Siku Ya Wapendanao. Kama ambavyo tumeitazama siku ya Valentine wala haikuwa siku ya wapendanao ilikuwa sikukuu ya Kipagani, ila baadae ikachakachuliwa hapo ikawa ya Kikristo lakini ni kama upagani ndani yake. Ilipokuwa Wakati wa Uamsho kwente Karne ya 14 ambapo tamaduni zikaanza kupewa tena shamrashamra za Kitaifa, ndipo Valentine ikapewa shavu la kuwa siku ya wapendanao. Ndipo katika kipindi hiki watu wakaachana na makatazo ya kidini wakati huo na yale mafundisho ya msingi katika dini yakapewa kisogo na watu wakageukia matamanio yao.Nyaraka na nyimbo mbali mbali za kuhusu mapenzi, ngono na kujamiiana vikaenea katika kizazi hicho kama ilivyo sasa kila nyimbo ni mapenzi hata picha za mabango ya barabarani ni mapenzi kwenda mbele. Valentine na Kibiashara Zaidi. We utaona tu valentine hii ubepari unavyoshika hatamu yake katika kutumia ili tu “Wapenzi” Wakolezee eti Valentine Day. Kuna watu watanunua nguo mpya nyekundu ili mradi tu watupie kitu chekundu, mijihela mingine itapelekwa kununulia zawadi za wapenzi, hapo sijahesabu maua yatakayonunuliwa siku ya valentine, hapo sijaongelea chakula cha usiku cha wapenzi, hapo sijaongelea wale watakao amua kwenda kulala. Kama kuna siku nzuri ya biashara basi Valentine inakaribiana na Christimas. Mtazamo Wangu na Valentine Za Kibongo. Nakubaliana na wale ambao siku hiyo watatumia kuwapongeza ndugu zao wazazi wao na wapenzi wao. Swali la kujiuliza hapa “tuna adhimisha” ama “tunasheherekea” Valentine?kama tuna adhimisha siku hii, lazima ujue unachoadhimisha, kipi kati yapo juu unachoadhimisha?kama unasheherekea unashehereka nini?otherwise tunakuwa busy na sikukuu tusiyoijua. Ukitaka lawama valentine we usinunue zawadi, usimtoe mtu dinner, jikaushe kama jumanne zingine tu za kawaida. Kwa Mtazamo wangu mdogo nimebaini “Valentine Day” Wanawake ndo wako excited nayo kuliko Wanaume. Kwanini?Kwa wale wanaume wasio waaminifu siku hiyo wengi hu opt kupumzika nyumbani ili kuondoa lawama. How?Unajua wanaume wengi ndio wanao cheat sasa anapotaka kwenda outing anajua msala unaweza kutokea. Ila kwa wale wanao tazamia kusheherekea ama kuadhimisha siku hii kwa namna yoyote ile basi nina wasiwasi wa baadhi ya watu kukimbiwa kidizaini siku hii, na wengi pasipo kujua kuwa kuna roho nyuma yake watajikuta wakiadhimisha kwa ngono kama ishara ya upendo kumbe ni ile ibada ya kipagani tuliyoisoma hapo juu. Abiria chunga mzigo wako kwenye Valentine. Swali la Kujiuliza Kuna madhara yoyote ya Mkristo kusheherekea Sikukuu Ya Valentine? SPECIAL THANKS TO SAM SASALI. Posted by Sophia Mbeyu at 00:36 Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to FacebookShare to Pinterest No comments: Post a Comment Links to this post Create a Link Older Post Home Translate Powered by Translate PLACE YOUR ADS HERE PLACE YOUR ADS HERE TANGAZO: UNAHITAJI VIATU WASILIANA NASI HAPA TANGAZO: UNAHITAJI VIATU WASILIANA NASI HAPA UNAHITAJI BOFYA PICHA HII KUONA PICHA ZAIDI About Me My Photo Sophia Mbeyu View my complete profile Blog Archive Popular Posts MATOKEO YA DARASA LA SABA MWAKA 2014 YAMETOKA, INGIA HUMU KUONA DK. CHARLES E. MSOND E AKITANGAZA MATOKEO YA DARASA LA SABA MAPEMA HII LEO OFISINI KWAKE,MSONDA AMESEMA MATOKEO YA MWAKA HUU UFAURU WAKE ... MITINDO YA VITENGE KWA WANAWAKE NA WANAUME... KAMA INAVYYONYESHA PICHA! VAZI LAKITENGE LAWEZA KUTUMIWA KAMA VAZI LA OFISI AMA CASUAL SIO LAZIMA KITENGE KIWE N... MITINDO YA VITENGE KWA WOTE,.... WADAU WA VITENGE KILA WIKI KUNA POST YA VITENGE FUATILIA POST ZA NYUMA KUPATA MITINDO MBALIMBALI ZAIDI... MITINDO YA VITENGE KWA AKINA DADA NA WATOTO.. MITINDO YA VITENGE Mitindo ya Vitenge inaweza kushonwa katika dizain mbalimbali, hii inaonyesha mitindo kwa vijana ni katika kuonyesha kuwa kitenge si lazima ... MITINDO BOMBA YA VITENGE! Huhitaji nguo za majina kupendeza, kitu cha kitenge tosha kabisa kukutoa bomba! MITINDO MBALIMBALI YA VITENGE, VIATU NA HANDBAG ZA KITENGE.... MITINDO YA VITENGE KWA AKINA DADA NA WATOTO! MITINDO YA VITENGE KATIKA MATUKIO TOFAUTI... MITINDO YA VITENGE Labels African day 2008 may AMUUA BABA YAKE KUMUOKOA SHANGAZI YAKE ALIYEKUWA ANABAKWA- NACHINGWEA ARIEL SHARON AFARIKI ASEMA YADHOOFISHA UCHUMI AFRIKA aswira Kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar:Rais wa Comoro Awasili Zanzibar Kuhudhuria Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 50 ya Mapinduzi BAADA YA BASI KUGONGA NA KUUA WATATU BABA NA MWANA JAY-Z NA MWANAE BLUE IVY.. Biza mupulu artist Biza mupulu Botswana BREAKING NEWS: FIFA YAHAMISHA MUDA WA KOMBE LA DUNIA MWAKA 2022 HUKO QATAR HABARI ZA KIMATAIFA/ WAUMINI WAUAWA MSIKITINI NCHINI NIGERIA HABARI ZA UMBEYA/. WAKATI WEMA AKITUMA VIDEO YA DIAMOND AKIWA KITANDANI HAKUNA KAMA MWANAMKE HAPO NAPO SASA IGP ATANGAZA MABADILIKO MAKUBWA JESHI LA POLISI. IJUMAA NJEMA WADAU WA SOPHIEMBEYU BLOG.... IMETANGAZWA RASMI KESHO NI SIKU YA MAPUMZIKO KUSHEHEREKEA MAPINDUZI: Kundi la FM Academia KUTWAA TUZO YA MWANASOKA BORA WA AFRIKA NJE YA AFRIKA Machael Jackson kuaga dunia MADAWA YA KULEVYA YAINGIZWA SUPERMARKET KATIKA MAKASHA YA NDIZI MAGAZETI YA LEO IJUMAA 10 JANUARY 2014 Magonjwa ya mlipuko yanukia jijini Dar MAN UNITED YAZINDUKA Mariam bongo MAWAZIRI WAPYA WATANO WATAJWA TANZANIA MITINDO YA NYWELE MITINDO YA VITENGE MKAPA AIPONDA MISAADA KUTOKA NJE MSIKIE JOKATE AKIONGELEA MUZIKI NA FILAMU....... Mwekezaji abomoa nyumba za wananchi wa Mkuyuni-Morogoro ili kupisha ujenzi wa Majosho.11 jan mgogoro Nondoz wa Bongo waliokamilisha kisomo chao Data India. Pablo Machine Familia dar Pablo Machine na watoto Pablo Machine na wakenya kwenye festival Pablo Machine Sabiti PENNY NAE ANENA "HAITATOKEA KAMWE NIKAMDHARAU DIAMOND PICHA ZA WATUHUMIWA WALIOKAMATWA WAKISAFIRISHA SILAHA ZA KIVITA KATAVI PICTURE OF THE DAY..KWA RAHA ZAO Rais wa Zanzibar Dr Ali Shein Aendelea Kutunuku Nishani Rihanna out in Barbados RWANDA YAKANUSHA UVUMI KUHUSU KIFO CHA KAGAME SABABU YA KIFO CHA MPENDWA WETU ZAINAB BUZOHERA TASWIRA MBALI MBALI KATIKA SHEREHE YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI ZANZIBAR LEO 12/01/2014 UNAKANDAMIZA ... VAZI LA LEO Wa Bongo WAFANYABIASHARA WA DAR WAGOMEA MASHINE ZA KODI ZA TRA WAFUNGA MADUKA LEO Wakali bongo hawo WANANCHI WALITEKETEZA BASI KWA MOTO WAZIRI KIGODA : MFUMO MASHINE EFDs NI MBOVU WEEKEND NJEMA WADAU WA SOPHIEMBEYU BLOG....NAWAPENDAAA MINGIIII. WEMA NI MAMA KIJACHO? SOMA ALICHOANDIKA HAPO Wizara ya maliasili na utalii imewasimamisha kazi watumishi wake 22 wa idara ya wanyama pori YAICHAPA 2-0 SWANSEA CITY Yatima Dar walilia madarasa yakujisomea PLACE YOUR ADS HERE PLACE YOUR ADS HERE powered by Slideshow Sikiliza clouds radio SIKILIZA KWANZA JAMII RADIO Followers Google+ Followers Total visitors Total Pageviews Sparkline 1515131 CLOCK & CALENDAR buy research paper custom essay writing answering service care February 2015 S M T W T F S 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 Free Counter Counter Free PLACE YOUR ADS HERE PLACE YOUR ADS HERE WEBSITES & BLOGS MICHUZI JIACHIE BONGOBLOGS TanzMED Wavuti Allyshams Myummah76 Francis Godwin Globalpublishers Full Shangwe Ladyjaydee Swahili TV TMF Haki Ngowi Mimi na Tanzania Mo Blog Chadema Blog CCM Blog January Makamba Zitto kabwe Habari Leo Daily News Mwananchi Mtanzania Tanzania Daima Raia Mwema Majira Mwanaspoti The Citizen Daraja Letu IPP Media Bashir Nkoromo BBC Swahili Sauti ya Amerika Jamii Forums BLOG DEVELOPMENT BLOG DEVELOPMENT AUDIO BAR SIKILIZA BRAND NEW TRACK HAPA!! VIDEO BAR UNATAKA KUPUNGUA UZITO!! CLICK THIS IMAGE Contact Form Name

No comments:

Post a Comment