STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, September 17, 2012

Cheka kucheza mara ya mwisho na Nyilawila, kisa...!

Francis Cheka (kulia) alipokuwa 'akimsulubu' Karama Nyilawila katika pambano lao lililofanyika mapema mwaka huu na mjini Morogoro na Cheka kuibuka mshindi wa pointi dhidi ya mpinzani wake.

BONDIA nyota wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka 'SMG' amesema huenda pambano lake dhidi ya Karama Nyilawila 'Captain' ndilo likawa la mwisho kwake kupigana na mabondia wa Tanzania.
Cheka anatarajiwa kuzipigana na Nyilawila katika pambano la kuwania ubingwa wa UBO litakalofanyika Septemba 29 kwenye ukumbi wa PTA, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mara ya tatu kwa mabondia hao kukutana.
Katika michezo yao ya awali, wawili hao walitoka sare mechi moja na nyingine iliyochezwa mapema mwaka huu, Cheka aliibuka kidedea kwa kumpiga mpinzani wake kwenye uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Cheka alisema anaamini pambano hilo alilodai ana hakika ya kuibuka na ushindi mbele ya Nyilawila, huenda likawa la mwisho kwake kuzipiga na mabondia wa Tanzania.
Alisema, awali alishasema asingecheza tena nchini kwa kukosa mpinzani wa kweli kufuatia kuwachakaza karibu mabondia wote wakali akiwemo Rashid Matumla, Mada Maugo, Japhet Kaseba na hata Nyilawila mwenyewe.
"Iwapo nitaendeleza mkong'oto kwa Nyilawila, japo nina hakika kwa hilo kutokana na ubora nilionao na uwezo mkubwa katika ngumi, sitacheza tena na mabondia wa nchini, nitaelekeza nguvu zangu kwa mabondia wa nje ili kujenga zaidi jina," alisema.
Alisema kwa sasa anaendelea vema na maandalizi yake dhidi ya pambano hilo lililoandaliwa na Robert Ekerege na litakalosindikizwa na michezo kadhaa ya utangulizi na kutamba ataendelea kuwapa raha mashabiki wake.
"Naendelea vema kujifua chini ya kocha wangu Abdallah Saleh 'Komando', sitawangusha mashabiki wangu kwa namna nitakavyomchapa Nyilawila," alisema.
Pambano hilo la uzani wa Super Middle raundi 12, litaamuliwa na mwamuzi wa kimataifa wa Malawi Jerome Waluza na litasindikizwa na michezo ya utangulizi ambapo Juma Kihiyo dhidi ya Ibrahim Maokola, Seba Temba wa Morogoro dhidi ya Stam Kesi.
Michezo mingine ni kati ya Sadik Momba dhidi ya Amos Mwamakula, huku Anthon Mathias wa Morogoro atacheza na Shaban Kilumbelumbe na Deo Samwel akipambana na Hassan Kidebe.
          
Mwisho

No comments:

Post a Comment