STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, September 17, 2012

MKURANGA wapata viongozi wapya wa soka

CHAMA cha Soka Wilaya ya Mkuranga, MDFA, kimefanikiwa kupata viongozi wake wapya baada ya chama hicho kufanya uchaguzi wake mkuu jana Jumapili.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Soka Mkoa wa Pwani, COREFA, iliyosimamia uchaguzi huo wa Mkuranga, Masau Bwire, uchaguzi huo wa MDFA ulifanyika wilayani humo juzi Jumapili, ambapo Sudi Baisi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa chama hicho.
Bwire, alisema Baisi alipata jumla ya kura 41 kati ya wajumbe 46 kutoka klabu 19 walioshiriki kinyang'anyiro cha uchaguzi huo ambao baadhi ya nafasi zilikosa wagombea wenye sifa za kuziwania.
Mwenyekiti huyo alisem, aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu ni Issa Kivyele aliyezoa kura 42, huku John Malata alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa COREFA na Mwakilishi wa Klabu nafasi hiyo ilitetewa vema na Rashid Selungwi.
Bwire, alisema nafasi nyingine katika uchaguzi huo hazikuwa na wagombea na hivyo chama hicho kitalazimika kuitisha uchaguzi mdogo kwa ajili ya kuziba mapengo hayo.
MDFA kimekuwa chama cha pili kufanya uchaguzi wake mkuu baada ya awali Chama cha soka Kisarawe, KIDAFA kuchaguana wiki mbili zilizopita, huku vyama vingine viwili vya Rufiji na Mafia vyenyewe zikitarajiwa kufanya Septemba 29 sambamba na kile cha Soka la wanawake mkoa wa Pwani, TWFA.
Chama cha soka Bagamoyo chenyewe kitaitisha uchaguzi wake Oktoba 8, siku chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa COREFA utakaofanyika Oktoba 14 wilayani Mafia.

Mwisho

No comments:

Post a Comment