STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, April 16, 2013

MO kuiongoa Kamati ya Saidia Stars Ishinde

Mhe Mohammed Dewji
MBUNGE wa Singida Mjini, Mhe Mohammed Dewji ataiongoza Kamati ya Saidia Taifa Stars iliyotangazwa leo na serikali ikiwa na wajumbe 11.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo kamati hiyo itakuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha Stars inajiandaa na kushiriki vyema kwenye michuano ya kimataifa.
Taarifa hiyo ya serikali imewataja wajumbe 11 wa kamati hiyo kuwa ni; Mohammed Dewji (Mbunge) Bi Teddy Mapunda, Dk Ramadhani Dau, Dioniz Malinzi, Asji Shabir, George Kavishe, Mohammed Raza (Mbunge), Leodger Tenga, Joseph Kusaga, Kapt John Komba na Zitto Kabwe (Mbunge).
Taarifa rasmi ya serikali ni kama ifuatavyo:
 
Kama mnavyofahamu, hivi sasa Timu ya Taifa ya mpira wa Miguu kwa Wanaume (Taifa Stars) ipo kwenye michuano ya kufuzu kushiriki Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini Brazil mwaka 2014.
Katika Afrika, Tanzania (Taifa Stars) imepangwa kundi C kati ya makundi 10. Kundi C linajumuisha timu za Ivory Coast, Morocco, Gambia na Tanzania.
Kwa sasa katika kundi C, Taifa Stars inashika nafasi ya pili ikiwa na alama sita (6), nyuma ya Ivory Coast yenye alama saba (7), Morocco ina alama mbili (2) na Gambia ina alama moja(1).
Kwa mara nyingine Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inapenda kuwapongeza Taifa Stars, kwa kazi nzuri ambayo wameishaifanya ikiwemo ushindi wa Bao Tatu kwa Moja dhidi yaMorocco. Watanzania wote na Wadau wa Soka nchini wamefurahishwasanana mafanikio yaliyofikiwa na Taifa Stars na yenye kutupa matumaini  katika kuitayarisha Taifa Stars kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia  kwa mwaka 2014 nchiniBrazil.
Kwa hali ilivyo hivi sasa, Taifa Stars ipo katika nafasi nzuri ya kufuzu. Ili Tanzania tuweze kufuzu, Taifa Stars inatakiwa ishinde mechi zote tatu (3) na kuongoza kundi C na baadae iingie katika Timu kumi (10) bora na kisha zipatikane Timu tano (5) kutoka Afrika ambazo zitakuwa zimefuzu kwenda Brazil katika Fainali za Kombe la Dunia kwa mwaka 2014.  Tunaamini hili linawezekana.
Sasa kwa kuzingatia uzito wa jukumu lililo mbele yetu na kwa Taifa Stars kwa ujumla; Serikali imeunda Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars.
Jukumu la msingi la Kamati tunayoiunda ni kuhakikisha Taifa Stars inawezeshwa na kuandaliwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuunda kikundi cha kuishangilia timu ya Taifa ndani na nje ya nchi. Wajumbe wa Kamati ya Taifa Stars Stars itakayoongozwa na Mhe. Mohamed Dewji ni hawa wafuatao:-
 1. Mhe Mohamed Dewji           -       Mbunge
2. Bi. Teddy Mapunda             -       Montage
3. Dkt. Ramadhani Dau           -       Mkurugenzi Mtendaji NSSF
4. Bw. Dioniz Malinzi               -       Mwenyekiti BMT
5. Bw. Abji Shabir                  -       New Africa Hotel
6. Bw. George Kavishe            -       TBL
7. Mhe. Mohamed Raza           -       Zanzibar
8. Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
9. Bw. Joseph Kusaga             -       Clouds
10. Mhe. Kapt. John Komba    -       Mbunge
11. Mhe. Zitto Kabwe             -       Mbunge
Kamati hii iliyoteuliwa leo, naomba ianze kazi mara moja.  Hadidu za rejea zitakazowaongoza kutekeleza majukumu yao chini ya Kamati hii watazipata kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kamati itashirikisha wadau mbalimbali kadri itakavyoona inafaa.
Serikali inaahidi kutoa ushirikiano utakaohitajika katika kuhakikisha Kamati hii inafanya kazi vizuri ili kuiwezesha Taifa Stars kushinda Mechi zote zilizombele yetu.
Aidha nichukue fursa hii kutoa wito kwa Watanzania wote, kuiunga mkono Taifa Stars na Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars kwa hali namalikatika kuhakikisha timu yetu inafuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia.
Kwa niaba ya Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri Mkuu naomba niwasilishe salaam zao za kuwapongeza Vijana wetu wa Taifa Stars, pamoja na benchi la ufundi likiongozwa na Kocha Mkuu Kim Poulsen. Kwa pamoja wanaomba Taifa Stars iendelee kujipanga kwa mechi zijazo.  Nawahakikishia kuwa Serikali, Watanzania na wadau wa Soka nchini wapo nyuma yao.
Mungu Ibariki Taifa Stars.
Mungu Ibariki Tanzania.
Dkt. Fenella Mukangara (Mb)
WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
16 Aprili, 2013


Coastal Union yangang'aniwa mkwakwani


MABINGWA wa zamani wa Tanzania, Coastal Union ya Tanga jioni ya leo imeng'ang'aniwa nyumbani na JKT Ruvu ya Pwani katika pambano lililochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani-Tanga.
Kwa mujibu wa taarifa ambazo MICHARAZO ilipenyezewa hivi punde kutoka Tanga zinasema kuwa timu hizo zimetoshana nguvu kwa kushindwa kufungana katika pambano lililokuwa kali na lenye ushindani.
Kwa matokeo hayo timu hizo zimegawana pointi moja moja na kuifanya Coastal ifikishe pointi 33 na kulingana pointi na Mtibwa Sugar, lakini uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa yanaifanya ikwee nafasi ya tano huku maafande wa JKT wakifikisha pointi 23 na kuchupa kutoka nafasi ya 12 hadi ya 11.
Kipute cha ligi hiyo kinatarajiwa kuendelea tena kesho kwa mechi tatu katika viwanja vya Mkwakwani Tanga kati ya vinara Yanga na wenyeji wao Mgambo JKT, Mtibwa Sugar itakuwa nyumbani kuumana na JKT Oljoro na Toto African itasafiri hadi Kagera kuwakabili wenyeji wao Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kaitaba.

Tetemeko la Ardhi laleta maafa makubwa Iran

 
TETEMEKO la Ardhi lenye ukubwa wa 7.8 limeupiga mji wa Khash nchini Iran na mpaka sasa inaripotiwa zaidi ya watu 80 wamepoteza uhai wao.
Tetemeko hilo ambalo limezipiga pia nchi za Pakstani, India na Qatar na kusababisha uharibifu na watu kadhaa kujeruhiwa, ambapo kwa habari za sasa zinasema kwa Iran waliofariki ni 81 na zoezi la uokozi linaendelea hali inayobashiriwa huenda idadi ya vifo vikaongezeka.

Wamorocco watakaoikabili Azam kutua kesho

Kikosi cha As FAR Rabat kinachotarajiwa kuja nchini kesho kuvaana na Azam
Azam wakataowakaribisha Wamorocco kwenye uwanja wa Taifa Jumamosi.
Na Boniface Wambura
WAPINZANI wa Azam katika michuano ya Kombe la Shirikisho, AS FAR Rabat ya Morocco wanatarajiwa kutua nchini kesho (Aprili 17 mwaka huu) saa 7 mchana kwa ndege ya Emirates.
Msafara wa timu hiyo wenye watu 28 utafikia hoteli ya Sapphire iliyoko maeneo ya Kariakoo, Dar es Salaam tayari kwa mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya pili itakayochezwa Jumamosi (Aprili 20 mwaka huu) saa 10 kamili jioni Uwanja wa Taifa.
Azam na FAR wataumana katikia pambano la raundi ya pili maarufu kama 16 Bora kuwania nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi za klabu barani Afrika.
Azam iliing'oa BYCII kwa jumla ya mabao 2-1 katika mechi ya raundi ya kwanza awali ikitoa pia Al Nasir Juba ya Sudan Kusini.
Wawakilishi hao pekee wa Tanzania ndiye jicho na roho ya mashabiki wa soka nchini kufuatia wawakilishi wengine wakiwemo Simba na Jamhuri -Pemba kung'olewa mapema kwenye michuano hiyo.
Tayari kikosi cha timu ya Azam ambayo mwishoni mwa wiki waliisimamisha Simba katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kutoka nao sare ya mabao 2-2 imeshaingia kambini kujiandaa na pambano hilo ambalo Azam watahitajika kushinda nyumbani ili kujiweka katika nafasi nzuri kwa mechi ya marudiano ugenini wiki mbili zijazo.
Kwa muda mrefu klabu za kutoka Kaskazini mwa Afrika zimekuwa zikizisumbua timu za Tanzania na Azam wanaoshiriki michuano hiyo ya kimataifa kwa mara ya kwanza wanahitajika kuufuta uteja huo mbele ya Wamorocco hao ambao ni timu ya maafande.

TFF yamlilia Meja Jenerali Makame Rashid


Makamu wa Rais, Dk Gharib Mohammed Bilal akitoa heshima ya mwisho kwa mwili wa Meja Jenerali Makame Rashid ukiwa kwenye jeneza lake.

Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko za kifo cha Mkuu wa zamani wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Makame Rashid kilichotokea juzi (Aprili 14 mwaka huu) kutokana na maradhi jijini Dar es Salaam.

Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kutokana na mchango aliotoa Meja Jenerali Makame Rashid ikiwemo kuwa mlezi wa timu ya Ruvu Stars wakati huo akiwa Kamanda (CO) wa Kikosi cha Ruvu JKT.

Pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mdhamini (Trustee) wa TFF wakati huo ikiitwa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT) na wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya katika miaka ya themanini alikuwa sehemu ya mafanikio kwa timu ya Tukuyu Stars ya Mbeya iliyotwaa ubingwa wa Tanzania Bara mwaka 1987 ikiwa ndiyo kwanza imepanda kucheza Ligi Kuu wakati huo ikiitwa Ligi Daraja la Kwanza.

TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Meja Jenerali Makame Rashid, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Maziko yanatarajiwa kufanyika leo (Aprili 16 mwaka huu) nyumbani kwao mkoani Mtwara. Mungu aiweke roho ya marehemu Sembwana mahali pema peponi. Amina

VPL KUTIMUA VUMBI VIWANJA VITATU KESHO



Na Boniface Wambura
LIGI Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Aprili 17 mwaka huu) kwenye viwanja vitatu huku vinara wa ligi hiyo Yanga wakifukuzia ubingwa huo jijini Tanga.

Yanga inayoongoza ligi ikiwa na pointi 52 itakuwa mgeni wa Mgambo Shooting katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Athuman Lazi kutoka Morogoro kwenye Uwanja wa Mkwakwani. Waamuzi wasaidizi wa mechi hiyo ni Michael Mkongwa wa Iringa na Godfrey Kihwili wa Arusha wakati Kamishna wa mechi hiyo ni Godbless Kimaro kutoka Moshi.

Kagera Sugar na Toto Africans zitaumana kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba katika mechi namba 164 itakayokuwa chini ya mwamuzi Martin Saanya wa Morogoro.

Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro, na wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 4,000 utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mtibwa Sugar yenye pointi 33 na Oljoro JKT yenye pointi 28.

Israel Nkongo kutoka Dar es Salaam ndiye atakayechezesha mechi hiyo akisaidiwa na Hamis Chang’walu (Dar es Salaam) na John Kanyenye (Mbeya). Kamishna wa mechi hiyo ni Ramadhan Mahano kutoka Iringa.

Mamuu ana Tatakoa akiwabeba walemavu

Mamuu (kulia) akiwa na Baby Madaha walioicheza filamu hiyo ya Tatakoa

MWANAHABARI aliyejitosa kwenye fani ya uigizaji na utayarishaji wa filamu nchini, Mariam Mndeme 'Mamuu' amefyatua filamu mpya iitwayo Tatakoa iliyowashirikisha nyota kadhaa nchini.
Mamuu, aliyewahi kuwa mtangazaji wa TBC na kufanya kazi katika magazeti ya Global Publisher, alisema filamu hiyo ni ya pili kwake baada ya awali kuitoa 'Pooja'.
Mwanahabari huyo aliiambia MICHARAZO kuwa, filamu hiyo ya 'Tatakoa' iliyowashirikisha wakali kadhaa ipo hatua ya mwisho kabla ya kuachiwa hadharani.
Mamuu alisema mbali na yeye wakali wengine waliyoicheza filamu hiyo ni pamoja na Baby Madaha, Frola Mvungi, Salma Jabu 'Nisha', Husna Idd 'Sajenti'.  Alice Bagenzi 'Rayuu', Jumanne Kihangale 'Mr Chuz'. Kupa, Zerisha na wengine.
"Baada ya kimya kirefu tangu nilipotoa Pooja, nimekuja na filamu nyingine mpya iitwayo 'Tatakoa' ambapo mimi na Mr Chuz ndiyo wahusika wakuu, huku Baby Madaha akicheza jana 'Jini-Joka'," alisema Mamuu.
Msanii huyo alisema filamu hiyo kazi hiyo mpya ni mwanzo wa kuwapa mashabiki wake burudani ndani ya mwaka huu, akiwa pia mbioni kuratibu kipindi maalum kwa ajili ya walemavu waliokata tamaa waliopo maeneo ya vijijini.
"Nimeona kama mwanajamii napaswa kutoa mchango wangu kwa walemavu kwa kuandaa kipindi hicho kutakachokuwa kikionyesha matatizo ya watu hao na kusaidia kupata misaada itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi," alisema Mamuu.
Mamuu alisema kipidni hicho anachokirekodi kuwasaidia walemavu anapigwa tafu na kigogo mmoja wa serikalini ambaye ji waziri, lakini aliyekataa kumtaja jina kwa sasa na mwingine ni Wema Sepetu

Baby Madaha kupasua anga la kimataifa


NYOTA wa filamu ambaye pia ni mwanamitindo na muimbaji wa muziki wa kizazi kipya nchini, Baby Madaha anatarajiwa kufanya ziara ya maonyesho katika nchi nne tofauti za Afrika.
Ziara hiyo itakayoanza mapema mwezi ujao na itakayochukua muda wa mwezi mzima itamshirikisha msanii huyo na wakali wengine ambao watapangwa katika ratiba hiyo kutoka nchini.
Akizungumza na MICHARAZO, Madaha alisema ziara hiyo itahusisha nchi za DR Congo, Zimbabwe, Angola na Msumbiji na itaratibiwa na 'super market' moja kubwa nchini inayomilikiwa na Jumanne Kishimba.
"Kaka yangu natarajia kufanya ziara ndefu ya kujitangaza kimataifa nje ya nchi ambayo itakuwa ya maonyesho ya muziki na filamu katika nchi nne za Afrika, ziara itakayochukua muda wa zaidi ya wiki tatu," alisema Baby Madaha.
Mkali huyo alisema katika ziara hiyo mratibu mkuu atakuwa muigizaji mwingine nchini Mariam Mndeme 'Mamuu'.
Alisema kwa sasa anaendelea na maonyesho ya ndani ambapo wiki hii anatarajiwa kuwa jijini Mwanza kabla ya kuanza maandalizi ya safari hiyo ambayo amedai itamsaidia kujitangaza na kuitangaza Tanzania kimuziki na filamu nje ya mipaka.
"Kwa sasa naelekea Mwanza kwa ajili ya maonyesho kadhaa kabla ya kujiandaa na safari hiyo," alisema Baby aliyeibuliwa na shindano la Bongo Star Search (BSS) la mwaka 2008.

Golden Bush Veterani yaitafuna Moro Veterani x3

Kikosi cha Golden Bush Veterani

MABAO mawili kutoka kwa Athuman Machuppa na moja la Abuu Ntiro jumamosi yalitosha kuipa ushindi wakali wa soka la maveterani jijini Dar, Golden Bush Veterani kuitambia Morogoro Veterani nyumbani kwao kwa kucharaza mabao 3-1 katika pambano la kirafiki lililochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Kwa mujibu wa msemaji wa klabu hiyo, Onesmo Waziri 'Ticotico' alisema katika pambano lao walionyesha kiwango kikubwa kama kawaida yao na kuwapeleka puta wapinzani wao na kuibuka na ushindi huo wa mabao 3-1, ikiwa wanajiandaa kuvaana na wapinzani wao Wahenga.
Timu hizo mbili 'mahasimu' zilipokutana mara ya mwisho hivi karibuni kwenye uwanja wa Kinesi na Wahenga kulala mabao 2-1, huku wachezaji na aliyekuwa mgeni rasmi Kamanda wa Polisi, Thobias Andengenye wakinyeshewa na mvua iliyonyesha siku hiyo.
Pambano la safari hii kwa wapinzani hao wa jadi linatarajiwa kuchezwa siku ya maadhimisho ya miaka 49 ya Muungano wa Tanzania, ambapo tayari pande hizo mbili zimeshaanza kutambiana kila moja ikitamba kuibuka na ushindi ili kulinda heshima kwa wenzake.

Coastal Union, kuvuna nini leo kwa JKT Ruvu Mkwakwani?


Kikosi cha Coastal Union watakaoikaribisha JKT Ruvu
MICHUANO ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayoelekea ukingoni, inatarajiwa kuendelea leo kwa pambano moja la kukata na shoka kati ya Coastal Union ya Tanga dhidi ya wageni wao maafande wa JKT Ruvu ya Pwani.
Pambano hilo litachezwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Mkwakwani-Tanga, ambapo kila timu itakuwa ikihitaji ushindi ili kufikia malengo tofauti waliyonayo, Coastal ikiwania kuingia kwenye Tatu Bora na JKT kujinasua toka kwenye mstari wa hatari wa kushuka daraja.
Coastal ambayo katika mechi yake ya mwisho ilikumbana na kipigo cha kushtukiza toka kwa wanaoburuza mkia, African Lyon, ina pointi 32 na ushindi katika pambano la leo itawafanya wakwee nafasi moja hadi ya tano na kuiengua Mtibwa Sugar itakayoshuka dimbani kesho.
Hata hivyo maafande wa JKT ambo wamekuwa na msimu mbaya safari hii, wanapigana kuondoka katika janga la kuteremka daraja kutokana na ukweli mpaka sasa ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 22 tu sawa na Toto African, wakizizidi pointi mbili timu zilizozopo mkiani Lyon na Polisi Moro ambazo zina pointi 19 kila moja.
Kwa mazingira ilizonazo timu hizo ni wazi pambano la leo litakuwa gumu na lenye ushindani mkubwa ikizingatiwa kuwa, mashabiki wa Coastal wamekosa furha kitambo na timu yao kiasi cha kupost maoni yenye kukera dhidi ya uongozi na wachezaji wao.
Ligi hito inatarajiwa kuendelea tena kesho kwa michezo kadhaa likiwamo pambano la Yanga dhidi ya JKT Mgambo ambao kupitia kocha wao mkuu, Mohammed Kampira wameapa kuwazuia vinara wa ligi hiyo wasiwafanye daraja la kutwaa ubingwa msimu huu.
Yanga inaoongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 52 na inahitaji pointi sita tu kutawazwa mabingwa wapya baada ya waliokuwa wakilishikilia Simba kutemeshwa mapema wakati ligi ikiwa bado inaendelea kwa vile itawafanya wafikishe pointi 58 ambazo hazitaweza kufikiwa na Azam wanashika nafasi ya pili ambao wakishinda mechi zake nne tatu zilizosalia itafikisha pointi 56 tu.
Mechi zitakazopigwa kesho kwa mujibu wa ratian ya ligi hiyo ni kama ifuatavyo;
Mgambo JKT vs Yanga,
Kagera Sugar v Toto Africans (japo Toto imetishia kutoicheza mechi hiyo ya leo, ikihofia upangaji matokeo)
Mtibwa Sugar v JKT Oljoro

Hatari!

  Fedha za serikali zabebwa bila ulinzi TFF
  Ni mamilioni yatokanayo na makato U/Taifa
 
Viongozi wakuu wa TFF, Rais Leodger Tenga (kulia) na Angetile Osiah (kushoto)
 
WIZARA inayoshughulikia michezo nchini imekuwa ikifanya kitendo hatari cha kutuma maafisa wake kwenda kubeba mamilioni ya fedha zitokanazo na mgawo wake utokanao na makato ya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam bila ya ulinzi wowote ule kama taratibu za usafirisha fedha zinavyoelekeza, imefahamika.
 
Aidha, malipo ya mamilioni hayo ya fedha za serikali kutoka katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) hufanywa kwa fedha taslim na wala siyo kwa njia nyingine salama kama ya hundi, huku anayehusika kuzibeba ni afisa mmoja tu ambaye ni wazi kwamba anahatarisha usalama wake binafsi na pia wa fedha za umma.
 
Uchunguzi uliofanywa kwa siku kadhaa na NIPASHE umebaini kuwa utaratibu huo unaopingana pia kwa kiasi kikubwa na taratibu za malipo ya fedha za umma umekuwa ukifanyika kwa muda mrefu, hata kabla ya kuanza kutumika kwa Uwanja wa Taifa.
 
 
MAMILIONI YANGA v OLJORO
Juzi (Jumapili), mwandishi alishuhudia mmoja wa maafisa wa Wizara ya Michezo akifika katika ofisi za TFF na kubeba kienyeji (bila ya kusindikizwa na askari yeyote mwenye silaha) kiasi cha Sh. 7,552,500 zilizotokana na asilimia 15 ya uwanja katika mapato ya mechi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara kati ya Yanga na Oljoro JKT iliyochezwa Jumamosi na kuingiza Sh. milioni 63.17.
 
Afisa huyo alionekana akitinga kwenye ofisi za TFF zilizopo Karume jijini Dar es Salaam saa 4:38 asubuhi, akiwa peke yake kwenye gari aina ya Suzuki Vitara (namba tunazihifadhi) na kuondoka peke yake pia kwenye gari hilo mishale ya saa 5:22 asubuhi.
 
Kibaya zaidi, afisa huyo aliyekuwa amevaa shati la mikono mifupi lenye rangi nyeupe, kaptula yenye mifuko mingi na viatu vya raba vyenye mchanganyiko wa rangi nyeupe na nyeusi, hakuwa na ulinzi wowote wakati akiingia na kutoka kwenye ofisi ya fedha ya TFF.
 
"Ofisi imefunguliwa leo Jumapili kwa sababu kuna mechi ya Simba dhidi ya Azam. Ni kweli afisa wa wizara amechukua fedha za mgawo wa uwanja. Mtafute afisa habari (Boniface Wambura) au katibu mkuu (Angetile Osiah)... wao wanaweza kuzungumzia kwa kina sababu za uchukuaji fedha kwa mtindo huu wa malipo ya fedha taslim," alisema mmoja wa watu waliokutwa katika maeneo ya ofisi za TFF kwa sharti la kutotajwa jina lake. 
 
MAMILIONI SIMBA v AZAM
Kwa kutambua kuwa juzi kulikuwa na mechi kali ya ligi kati ya Simba na Azam, NIPASHE ilipiga tena kambi jana asubuhi kwenye ofisi za TFF ili kuona kama utaratibu wa kuchukua mamilioni hayo ya serikali kwa malipo taslim utaendelea, na tena bila ya mbebaji kuambatana na askari wa kumlinda.
 
Ilipofika saa 3:11 asubuhi, afisa yule yule aliyejihatarisha Jumapili ndiye aliyetinga tena kwenye ofisi za TFF akiwa peke yake kwenye gari lilelile aina ya Suzuki Vitara.
 
Mwandishi alifuatilia kwa karibu nyendo za afisa huyo. Ni kwamba, baada ya kupaki gari lake, alionekana akisalimiana na maafisa kadhaa wa TFF, akiwamo kocha wa timu ya taifa (Taifa Stars), Mdenmark Kim Poulsen. IIimchukua takriban dakika 26 afisa huyo kukamilisha zoezi hilo maana saa 3:57 asubuhi ndipo alipoingia ndani na kwenda moja kwa moja kwenye chumba cha malipo na kubeba mamilioni yanayokadiriwa kuwa ni Sh.
 7,925,600, kiasi ambacho ni sawa na asilimia 15 ya mgawo wa uwanja kwani mechi hiyo ya Simba dhidi ya Azam iliyochezwa juzi iliingiza Sh. milioni 66.855.
 
Baada ya kubeba fedha hizo, afisa huyo alionekana akifungua mlango wa nyuma wa gari alilokuwa nalo na kuweka begi linalodhaniwa kuwa na fedha hizo kabla ya kuondoka. 
 
Hiyo ilikuwa ni saa 4:03 asubuhi. Mwandishi alijaribu kumfuatilia kwa nyuma. Saa 4:07, afisa huyo aliingia ndani ya Shule ya Sekondari Benjamin William Mkapa iliyopo umbali mfupi kutoka TFF.
 
Saa 4:12, afisa huyo aliondoka kwenye shule hiyo na kurejea tena TFF na kuingia ndani ambapo akiwa na begi lake dogo lenye fedha, bila kuwapo na ulinzi wowote, alikaa kwa dakika 23, baadaye alitoka na kuingia kwenye gari na kuondoka saa 4:35.
 
TFF wanena
Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa TFF, Osiah alikiri kuwa serikali hutuma maafisa wake kubeba fedha hizo kwa malipo taslim kila siku moja baada ya mechi na utaratibu huo umekuwapo kwa muda mrefu.
 
"Ni kweli kwamba hata sisi tunatambua kuwa si vizuri kuwalipa pesa taslimu, tena ni kinyume cha sheria... lakini utaratibu huo umekuwapo kwa miaka mingi na sasa imekuwa kama desturi yetu," alisema Osiah.
 
Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema kuwa hata fedha za klabu zinachukua mgawo wake kwa njia hiyo, licha ya kuwapo kwa taarifa za tukio la kuporwa kwa Sh. milioni 10 za Simba katika eneo la Sinza Makaburini.
 
MICHAEL WAMBURA
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Tanzania (FAT sasa TFF), Michael Wambura alisema jana kuwa utaratibu wa TFF kutoa fedha taslimu badala ya hundi kwa serikali ni kosa, lakini akasema kuwa imezoeleka hivyo na kwamba hata wakati wa uongozi wao (FAT), walikuwa na mfumo huo ambao anaamini kwamba siyo sahihi.
 
"Wakati tukiwa madarakani, tuliwahi kuamua kutumia utaratibu wa hundi lakini ulileta matatizo. Kuna watu hawakutaka kabisa utaratibu huo. Nafikiri kuna haja ya kufanya uchunguzi kujua ni kwanini hawataki utaratibu huo," alisema Wambura.

KAMANDA WA POLISI 
Alipotafutwa na NIPASHE jijini Dar es Salaam kuzungumzia taratibu za usafirishaji wa fedha, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela, alisema ni kosa kwa mtu yeyote kusafirisha kiasi kikubwa cha fedha za umma bila kuwa na ulinzi.
 
"Ni kosa kusafirisha fedha za umma na hata za watu binafsi pasipokuwa na ulinzi wa polisi ama vyombo vingine vya usalama vya serikali au kampuni za ulinzi za watu binafisi zinazotambuliwa kisheria," alisema Kenyela.
 
"Inashangaza kuona TFF na wizara hawatumii utaratibu wa benki (hundi) kulipana. Kulipana fedha taslimu, tena mamilioni ya fedha ni kuhatarisha usalama wa fedha na watu wanaozisafirisha," aliongeza Kenyela.
 
Wakati wa tukio la kudaiwa kuporwa kwa fedha za Simba baada ya mechi yao dhidi ya Black Leopards ya Afrika Kusini iliyochezwa Desemba 29, 2012, aliwahi kuonya kuwa hivi sasa, likitokea tukio lolote la kuporwa fedha huku wahusika wakiwa hawajaomba ulinzi, watakuwa wakianza kwa kuwakamata watu hao
waliobeba fedha hizo kiholela.
 
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, alisema jana kuwa hawezi kulizungumzia suala hilo kwa sababu hakuwa katika mazingira mazuri ya kuzungumza kupitia simu kwa kuwa alikuwa safarini kuelekea jijini Dar es Salaam.
 
Hivi karibuni, watu kadhaa waliuawa katika tukio la uporaji wa Sh. milioni 150 
zilizokuwa zikisafirishwa bila ulinzi wa askari rasmi katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
 
 
CHANZO: NIPASHE

MASHINE ZA UMRI ZAWAUMBUA 'VIJEBA' VYA MICHUANO YA AFRIKA


UDANGANYIFU wa umri wa wachezaji kutoka barani Afrika umekuwa ni jambo la kawaida, lakini teknolojia mpya iliyobuniwa ya kutumia mashine kupima umri sahihi wa wachezaji umeanza kuwaumbua wachezaji 'vijeba' wanaochjachakachua umri ili kujifanya wadogo.
Teknokojia hiyo imewaumbua wachezaji tisa na kuondolewa kwenye michuano ya mataifa  ya Africa chini ya umri wa miaka 17 yanayofanyika nchini Morocco baada kipimo cha kugundua umri kupitia kiganja cha mkono kuonyesha kwamba wana umri mkubwa zaidi kuliko inavyopaswa.
Miongoni mwa wachezaji watatu wanatoka Congo-Brazzaville, Ivory Coast na Nigeria wamefungiwa kabisa kushiriki kwenye mashindano yoyote.
Mashine ya Magnetic Resonance Imaging (MRI) ilitumika kupima viganja vya wachezaji ili kujua ukweli wa umri wao.
Wachezaji ambao wameondolewa kwenye michuano hiyo ni kutoka Congo Cherlevy-Diabala Carim, Hardy Binguila na Bermagin Kangou, kutoka Ivory Coast  ni Dagou Britto, Abdul Diarrassouba na Siriki Dembele, na kutoka Nigeria ni Onyinye Ndidi, Ibrahim Abdullahi and Emmanuel Asadu.
Vikosi vya timu zote tatu vimepunguzwa mpaka kufikia wachezaji 18.
FIFA walianza kufanya utafiti wa umri wa wachezaji kwa kutumia technolojia ya MRI mwaka 2003 lakini wakaanza kuifanyia majaribio machine hiyo kwenye michuano ya U-19 World Cup in Nigeria.
Matokeo ya vipimo kwenye michuano ya kombe la dunia U-17 kuanzia 2003, 2005 na 2007 yalionyesha kwamba asilimia 35 ya wachezaji walikuwa wamezidisha umri unaoruhusiwa.
Wadau wa soka wanatamani kipimo hicho kianze kutumika pia hapa nchini ili kubaini baadhi ya wachezaji 'vibabu' lakini wakijitambulisha wakiwa na umri mdogo, jambo ambalo hata wenyewe wanajishangaa wanavyoongopa.
Credit to shaffihdauda.com

'Magaidi' walipua mabom na kuua watatu, zaidi ya 140 wajeruhiwa Boston Marathon



Baadhi ya picha za tukio hilo ambalo limesababisha kifo cha mtoto mwenye umri wa miaka 8 miongoni mwa waliofariki

Boston Marathon bombing kills 3, injures over 140

BOSTON (AP) — Two bombs exploded in the crowded streets near the finish line of the Boston Marathon on Monday, killing at least three people and injuring more than 140 in a bloody scene of shattered glass and severed limbs that raised alarms that terrorists might have struck again in the U.S.
A White House official speaking on condition of anonymity because the investigation was still unfolding said the attack was being treated as an act of terrorism.
President Barack Obama vowed that those responsible will "feel the full weight of justice."
As many as two unexploded bombs were also found near the end of the 26.2-mile course as part of what appeared to be a well-coordinated attack, but they were safely disarmed, according to a senior U.S. intelligence official, who also spoke on condition of anonymity because of the continuing investigation.
The fiery twin blasts took place about 10 seconds and about 100 yards apart, knocking spectators and at least one runner off their feet, shattering windows and sending dense plumes of smoke rising over the street and through the fluttering national flags lining the route. Blood stained the pavement, and huge shards were missing from window panes as high as three stories.
"They just started bringing people in with no limbs," said runner Tim Davey of Richmond, Va. He said he and his wife, Lisa, tried to shield their children's eyes from the gruesome scene inside a medical tent that had been set up to care for fatigued runners, but "they saw a lot."

"They just kept filling up with more and more casualties," Lisa Davey said. "Most everybody was conscious. They were very dazed." As the FBI took charge of the investigation, authorities shed no light on a motive or who may have carried out the bombings, and police said they had no suspects in custody. Officials in Washington said there was no immediate claim of responsibility.
WBZ-TV reported late Monday that law enforcement officers were searching an apartment in the Boston suburb of Revere. Massachusetts State Police confirmed that a search warrant related to the investigation into the explosions was served Monday night in Revere but provided no further details.
Some investigators were seen leaving the Revere house early Tuesday carrying brown paper bags, plastic trash bags and a duffel bag.
Police said three people were killed. An 8-year-old boy was among the dead, according to a person who talked to a friend of the family and spoke on condition of anonymity. The person said the boy's mother and sister were also injured as they waited for his father to finish the race.
Hospitals reported at least 144 people injured, at least 17 of them critically. The victims' injuries included broken bones, shrapnel wounds and ruptured eardrums.
At Massachusetts General Hospital, Alasdair Conn, chief of emergency services, said: "This is something I've never seen in my 25 years here ... this amount of carnage in the civilian population. This is what we expect from war."
Some 23,000 runners took part in the race, one of the world's oldest and most prestigious marathons.
One of Boston's biggest annual events, the race winds up near Copley Square, not far from the landmark Prudential Center and the Boston Public Library. It is held on Patriots Day, which commemorates the first battles of the American Revolution, at Concord and Lexington in 1775.
Boston Police Commissioner Edward Davis asked people to stay indoors or go back to their hotel rooms and avoid crowds as bomb squads methodically checked parcels and bags left along the race route. He said investigators didn't know whether the bombs were hidden in mailboxes or trash cans.
He said authorities had received "no specific intelligence that anything was going to happen" at the race.
The Federal Aviation Administration barred low-flying aircraft within 3.5 miles of the site.
"We still don't know who did this or why," Obama said at the White House, adding, "Make no mistake: We will get to the bottom of this."

With scant official information to guide them, members of Congress said there was little or no doubt it was an act of terrorism. "We just don't know whether it's foreign or domestic," said Rep. Michael McCaul, R-Texas, chairman of the House Committee on Homeland Security.
A few miles away from the finish line and around the same time, a fire broke out at the John F. Kennedy Library. The police commissioner said that it may have been caused by an incendiary device but that it was not clear whether it was related to the bombings.
The first explosion occurred on the north side of Boylston Street, just before the finish line, and some people initially thought it was a celebratory cannon blast.
When the second bomb went off, spectators' cheers turned to screams. As sirens blared, emergency workers and National Guardsmen who had been assigned to the race for crowd control began climbing over and tearing down temporary fences to get to the blast site.
The bombings occurred about four hours into the race and two hours after the men's winner crossed the finish line. By that point, more than 17,000 of the athletes had finished the marathon, but thousands more were still running.
The attack may have been timed for maximum carnage: The four-hour mark is typically a crowded time near the finish line because of the slow-but-steady recreational runners completing the race and because of all the friends and relatives clustered around to cheer them on.
Runners in the medical tent for treatment of dehydration or other race-related ills were pushed out to make room for victims of the bombing.
A woman who was a few feet from the second bomb, Brighid Wall, 35, of Duxbury, said that when it exploded, runners and spectators froze, unsure of what to do. Her husband threw their children to the ground, lay on top of them and another man lay on top of them and said, "Don't get up, don't get up."
After a minute or so without another explosion, Wall said, she and her family headed to a Starbucks and out the back door through an alley. Around them, the windows of the bars and restaurants were blown out.
She said she saw six to eight people bleeding profusely, including one man who was kneeling, dazed, with blood trickling down his head. Another person was on the ground covered in blood and not moving.
"My ears are zinging. Their ears are zinging," Wall said. "It was so forceful. It knocked us to the ground."
Competitors and race volunteers were crying as they fled the chaos. Authorities went onto the course to carry away the injured, while race stragglers were rerouted away from the smoking site.
Roupen Bastajian, a state trooper from Smithfield, R.I., had just finished the race when he heard the blasts.
"I started running toward the blast. And there were people all over the floor," he said. "We started grabbing tourniquets and started tying legs. A lot of people amputated. ... At least 25 to 30 people have at least one leg missing, or an ankle missing, or two legs missing."
The race honored the victims of the Newtown, Conn., shooting with a special mile marker in Monday's race.
Boston Athletic Association president Joanne Flaminio previously said there was "special significance" to the fact that the race is 26.2 miles long and 26 people died at Sandy Hook Elementary School.
___
Associated Press writers Jay Lindsay, Steve LeBlanc, Bridget Murphy, Rodrique Ngowi and Meghan Barr in Boston; Julie Pace, Lara Jakes and Eileen Sullivan in Washington; and Marilynn Marchione in Milwaukee contributed to this report.