STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Tuesday, April 16, 2013

Baby Madaha kupasua anga la kimataifa


NYOTA wa filamu ambaye pia ni mwanamitindo na muimbaji wa muziki wa kizazi kipya nchini, Baby Madaha anatarajiwa kufanya ziara ya maonyesho katika nchi nne tofauti za Afrika.
Ziara hiyo itakayoanza mapema mwezi ujao na itakayochukua muda wa mwezi mzima itamshirikisha msanii huyo na wakali wengine ambao watapangwa katika ratiba hiyo kutoka nchini.
Akizungumza na MICHARAZO, Madaha alisema ziara hiyo itahusisha nchi za DR Congo, Zimbabwe, Angola na Msumbiji na itaratibiwa na 'super market' moja kubwa nchini inayomilikiwa na Jumanne Kishimba.
"Kaka yangu natarajia kufanya ziara ndefu ya kujitangaza kimataifa nje ya nchi ambayo itakuwa ya maonyesho ya muziki na filamu katika nchi nne za Afrika, ziara itakayochukua muda wa zaidi ya wiki tatu," alisema Baby Madaha.
Mkali huyo alisema katika ziara hiyo mratibu mkuu atakuwa muigizaji mwingine nchini Mariam Mndeme 'Mamuu'.
Alisema kwa sasa anaendelea na maonyesho ya ndani ambapo wiki hii anatarajiwa kuwa jijini Mwanza kabla ya kuanza maandalizi ya safari hiyo ambayo amedai itamsaidia kujitangaza na kuitangaza Tanzania kimuziki na filamu nje ya mipaka.
"Kwa sasa naelekea Mwanza kwa ajili ya maonyesho kadhaa kabla ya kujiandaa na safari hiyo," alisema Baby aliyeibuliwa na shindano la Bongo Star Search (BSS) la mwaka 2008.

No comments:

Post a Comment