STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, October 5, 2014

Juventus yaizamisha As Roma, Tevez moto chini!

https://s.yimg.com/bt/api/res/1.2/etgxU0ykbfbKLMs4UzzcCw--/YXBwaWQ9eW5ld3M7cT04NTt3PTYzMA--/http://l.yimg.com/os/publish-images/sports/2014-10-03/dba924d0-4b36-11e4-9a01-6d10b444caf4_Totti_Juve_0310.jpgCARLOS Tevez amezidi kung'ara nchini Italia baada ya jioni ya leo kuifungia timu yake ya Juventus mabao mawili wakati 'Kibibi cha Turin' kikiwazima As Roma kwa mabao 3-2 kwenye pambano la kusisimua la Seria A, huku timu zote mbili zikicheza pungufu wa mchezaji mmoja mmoja baada ya wachezaji wao kupewa kadi nyekundu kwa nyakati tofauti kutokana na madhambi.
Tevez ambaye amekuwa akichuniwa kuitwa katika timu ya taifa ya Argentina, alifunga mabao yake yote kwa mikwaju ya penati katika dakika ya 27 na 45 wakati bao jingine likiwekwa kimiani na Bonucci dakika nne kabla ya pambano hilo kumalizika.
Mabao ya wageni yalifungwa na Francisco Totti pia kwa mkwaju wa penati dakika ya 32 na Iturbe dakika ya 44.
Kwa ushindi huo Juventus wamezidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 18 tatu zaidi ya wapinzani wao hao waliokuwa wametofautiana mabao ya kufunga na kufungwa kwenue msimamo huo.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo mapema leo mchana Empoli ikiwa nyumbani ilipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Palermo, huku Lazio ikiizamisha Sassuolo kwa mabao 3-2 waliowafuata nyumbani kwao, Parma walikubali kipigo cha magoli 2-1 dhidi ya wageni wao Genoa na Atalanta ikafa ugenini kwa bao 1-0 dhidi ya Sampdoria.
Timu za Udinese na Cesena zilitoshana nguvu kwa kufunga bao 1-1 na hivi sasa kuna mechi mbili zinachezwa ambazo hata hivyo haziwezi kubadilisha msimamo wa nafasi za juu za ligi hiyo.Mtibwa Sugar ushindi 100%, Shomar ampumulia Kavumbagu

WAKATI Mtibwa Sugar ikikwea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuiengua Azam, Ally Shomari, mshambuliaji huyo wa Mtibwa amemuashia taa ya kijani Didier Kavumbagu kwa kufikisha bao la tatu kwenye orodha ya wafungaji bora wa ligi hiyo.
Shomari ndiye aliyeifungia Mtibwa Suigar bao pekee lililoizamisha Mgmabo JKT katika mfululizo wa mechi za ligi kuu katika pambano lililochezwa kwenue uwanja wa Manungu, Turiani Morogoro.
Mtibwa imeweka rekodi ya kushinda mechi zake zote tatu na kufikisha pointi 9 na kukwea kileleni mwa msimamo wakiizidi mabingwa watetezi Azam kwa zaidi ya pointi mbili baada ya timu hiyo jana kulazimishwa suluhu na Prisons-Mbeya.
Shomari alifunga bao hilo dakika ya 10 ya pambano hilo na kufanya afikishe idadi ya mabao matatu akiwa nyuma ya Kavumbagu kwa bao moja.
Didier anaongoza msimamo akiwa na mabao manne, kisha Shomar na kufuatiwa na wachezaji wanne wenye mabao mawili kila mmoja ambao ni Ami Ali wa Mtibwa Sugar, Shaaban Kisiga wa Simba, Rashid Mandawa wa Kagera Sugar na Nassor Kapama wa Polisi Morogoro.

Chelsea waizima Arsenal, Diego Costa hakamatiki

Chelsea striker Diego Costa
Diego Costa akishangilia bao lake dhidi ya Arsenal
KOCHA Arsene Wenger bao hajapata tiza ya kumuzia Jose Mourinho baada ya timu yake ya Arsenal kulala mabao 2-0 mbele ya vijana wa darajani jioni hii katika mfululizo wa Ligi Kuu ya England.
Chelsea ikiwa chini ya Mourinho imekuwa ikiiadhibu Arsenal itakavyo, kitu ambacho kiliendelea leo kwenye uwanja wa Stanford Bridge wakati Chelsea walipopata ushindi huo kupitia mabao ya Eden Hazard aliyefungwa kwa mkwaju wa penati dakika ya 27 kabla ya kinara wa mabao katika ligi Diego Costa kufunga bao la pili katika dakika ya 78 akimalizia kazi nzuri ya Cesc Fabregas na kumfanya kufikisha jumla ya mabao tisa katika ligi hiyo.
Mechi inayoendelea kwa sasa ni kati ya West Ham ambayo ipo nyumbani kuikaribisha QPR na mpaka sasa ikiwa ni dakika chache tangu kuanza wenyeji waoangoza kwa bao 1-0.

Yanga yaendeleza ubabe kwa JKT, yailaza 2-1

http://2.bp.blogspot.com/-vDZhKG3xDnU/VBW5w-uqd4I/AAAAAAABIvw/geeCj2-4uGg/s640/HERM5680.JPGKLABU ya soka ya Yanga wameendelea kuwapa raha mashabiki wao baada ya jioni hii kupata ushindi muhimu wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Ruvu na kuendeleza ubabe kwake kwa maafande hao katika Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga ilipata ushindi huo kwenye uwanja wa Taifa na kuifanya timu hiyo kuchupa hadi nafasi ya tatu ya msimamo ikizipumulia timu za Mtibwa na Azam waliopo mbele yao.
Beki Kelvin Yondani aliianza kuiandika Yanga bao dakika ya 37 kwa mkwaju mkali ulioifanya timu yake kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao hilo.
Kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Niyonzima aliiongezea Yanga bao kipindi cha pili kabla ya Jabir Aziz kuifungia JKT Ruvu bao la kufutria machozi dakika chache kabla ya mapumziko.
Kwa ushindi huo Yanga imefikisha pointi sita wakati JKT wamendelea kusalia kwenye nafasi ya pili toka mkiani kutokana na kuwa na pointi mopja sawa na ndugu zao wa Ruvu Shooting Stars.
Mechi ijayo kwa Yanga itakuwa ni kati yao na watani zao Simba ambao wapo katika hali mbaya kwa kutoka sare katika mechi tatu mfululizo kiasi cha kubatizwa jina la wazee wa sare na watani zao.

Manchester Utd, Spurs zaua England, Di Maria achaa bwana!

Radamel Falcao
Falcao akishangilia bao lake lililokuwa la pili kwa Mashetani Wekundu mapema leo
Angel di Maria celebrates
Di Maria akishangilia bao la kwanza la Man Utd ambalo ni la tatu kwake tangu ajiunge na timu hiyo
Tottenham playmaker Christian Eriksen (left) rifles in a shot to put his side in front against Southampton
Erikson akiifungia Spurs bao dhidi ya Southampton

Radamel Falcao akishangilia bao lake la kwanza tangu ajiunge Old Trafford
Angel Di Maria celebrates scoring Manchester United's first goal against Everton on 27 minutes - it was his third goal in a United shirt
Angel Di Maria akishangilia baada ya kufunga goli la uongozi la Manchester United dhidi ya Everton kunako dakika ya 27 hili likiwa ni goli lake la tatu tangu kujiunga United
Di Maria celebrated by replicating the heart-shaped celebration of his former Real Madrid colleague Gareth Bale
MABAO mawili kutoka kwa wachezaji waliosajiliwa hivi karibuni, Angel di Maria na Radamel Falcao yameisaidia Manchester United kuchupa hadi nafasi ya nne ya msimamo wa Ligi Kuu England baada ya kuilaza timu ya Everton kwa mabao 2-1.
Wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford, Mashetani Wekundu walionyesha dhamira ya ushindi kwa kuandika bao la kwanza lililofungwa na Di Maria dakika ya 27 akimalizia pasi ya Juan Mata.
Bao hilo lililodumu hadi mapumziko kabla ya wageni kuchomoa kupitia kwa Naismith katika dakika ya 55 kama ya nyota wa zamani wa Atletico Madrid na Monaco Falcao kufunga bao la ushindi dakika ya 62 kwa kazi nzuri iliyofanywa na di Maria na kuwapa ushindi muhimu vijana wa Luis Van Gaal.
Katika pambano jingine la ligi hiyo Tottenham Hotspur ikiwa uwanja wa nyumbani wa White Hartlane walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Southampton.
Bao pekee la pambano hilo lilifungwa na Christian Eriksen dakika ya 40 na kuwafanya Spurs kupata ushindi muhimu na pointi tatu zilizowafanya kufikisha jumla ya pointi 11 na kuchupa hadi nafasi ya sita.

HILI NDILO BANGO LA TFF SIKU YA LEO

http://4.bp.blogspot.com/-uwg-TO-g29w/VDD-48c45qI/AAAAAAAAFcw/mR-gK9auAY0/s1600/tff_LOGO1.jpg
STARS KAMBINI, WACHEZAJI WA NJE WATUATimu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inaingia kambini kesho (Oktoba 6 mwaka huu) kujiwinda kwa mechi ya Kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Benin itakayochezwa Oktoba 12 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inaingia kambini kwenye hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam ikiwa na kikosi cha wachezaji 26 walioitwa na Kocha Mart Nooij kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 11 jioni.

Kwa mujibu wa Kocha Nooij, timu hiyo itakuwa na vipindi (sessions) 11 vya mazoezi kabla ya kucheza na Benin (Squirrels). Stars itafanya mazoezi asubuhi na jioni kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa ambapo baadhi yatafanyika Uwanja wa Taifa, na mengine kwenye uwanja mwingine.


Wachezaji Thomas Ulimwengu na Mbwana Samata wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) pamoja na Mwinyi Kazimoto anayechezea timu ya Al Markhiya ya Qatar wanawasili nchini kesho (Oktoba 6 mwaka huu).

Naye mshambuliaji Juma Liuzio anayechezea timu ya Zesco ya Zambia atawasili nchini keshokutwa (Oktoba 7 mwaka huu) kwa ndege ya Kenya Airways akitokea Ndola.

MAFUNZO YA USAJILI LIGI DARAJA LA PILIShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litaendesha mafunzo ya usajili kwa klabu za Ligi Daraja la Pili (SDL) yatakayofanyika kesho na keshokutwa (Oktoba 6 na 7 mwaka huu) kwenye hosteli ya TFF iliyopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume kuanzia saa 3 asubuhi.

Mafunzo hayo yatahusu usajili wa mtandao ambao ndiyo klabu hizo zitautumia kwa ajili ya Ligi hiyo itakayoanza baadaye mwezi ujao katika makundi manne ya timu sita sita kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

Kesho mafunzo hayo yatakuwa kwa ajili ya maofisa wa usajili wa klabu za Abajalo, Arusha FC, Kiluvya United, Magereza Iringa, Milambo SC, Mji Mkuu (CDA), Mkamba Rangers, Mshikamano, Mvuvumwa FC, Navy, Njombe Mji, Singida United, Transit Camp, Volcano FC na Wenda FC.

Oktoba 7 mwaka huu mafunzo hayo yatahusisha maofisa usajili wa klabu za Bulyanhulu FC, Eleven Stars, JKT Rwamkoma, Kariakoo Lindi, Mbao FC, Mpanda United, Pamba, Town Small Boys na Ujenzi Rukwa.

MABADILIKO YA MECHI ZA FDL KUNDI BShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya mabadiliko kwa baadhi ya mechi za kundi B Ligi Daraja la Kwanza (FDL) baada ya kupokea barua kutoka Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) ikieleza kuwa Uwanja wa CCM Kirumba utatumika kwa shughuli za kidini kuanzia Oktoba 16 hadi 19 mwaka huu.

Kutokana na hali hiyo, mechi namba 17 kati ya Toto Africans na Green Warriors iliyokuwa ichezwe kwenye uwanja huo Oktoba 18 mwaka huu sasa itafanyika Oktoba 20 mwaka huu.

Mabadiliko hayo pia yameathiri mechi namba 19 kati ya Green Warriors na Oljoro JKT ambayo sasa itachezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, Oktoba 23 mwaka huu badala ya Oktoba 21 mwaka huu.

Vilevile mechi namba 25 kati ya Burkina Faso na Oljoro JKT imesogezwa mbele kwa siku moja kutoka Oktoba 25 mwaka huu hadi Oktoba 26 mwaka huu. Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

BONIFACE WAMBURA
MKURUGENZI WA MASHINDANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

AC Milan yazinduka Italia, Muntari aibeba Juve, Roma leo

Sulley Muntari
Sulley Muntari
BAADA ya kucheza mechi tatu bila ushindi hatimaye mabingwa wa zamani wa Italia na Ulaya, AC Milan imezinduka kwenye Ligi Kuu ya Italia Seria A baada ya kupata ushindi mujarabu nyumbani kwao dhidi ya Chievo Verona.
AC Milan inayonolewa na mshambuliaji nyota wa zamani wa timu hiyo na Azzurri timu ya taifa ya Italia, Philip Inzaghi 'Pipo' ilipata ushindiwa mabao 2-0 kwenye uwanja wa Giuseppe Meazza, mjini Milano kupitia mabao ya Sulley Muntari aliyefunga dakika ya 55 na Keisuke Honda aliyeongeza la pili kwa mkwaju wa adhabu ndogo dakika ya 78 na kuifanya Milan kufikisha jumla ya pointi 11 na kuchupa hadi nafasi ya nne ya msimamo wa ligi hiyo unaoongozwa na Juventus.
Katika mechi nyingine iliyochezwa jana katika mfululizo wa ligi hiyo timu Hellas Verona ilipata ushindi mwembamba nyumbani wa bao 1-0 dhidi ya Cagliari.
Kipute cha ligi hiyo kitaendelea leo kwa michezo nan, Empoli itaumana na Palermo, Lazio dhidi ya Sassuolo, Parma itaikaribisha Genoa, Sampodoria itaialika Atalanta, wakati Udinese itaumana na Cesena.
Mechi nyingine ni kati ya vinara wa ligi hiyo Juventus na As Roma zenye pointi 15 kila mmoja zitakapochuana mjini Turin nyumbani kwa Juve, wakati Fiorentina itaumana na Inter Milan na Napoli itaikaribisha Torino.

Mtibwa kuongoza ligi leo, Yanga, JKT ni vita Taifa

Mtibwa Sugar wana nafasi kubwa ya kukalia kiti cha uongozi wa Ligi Kuu msimu huu leo
Mgambo JKT watakubali kufanywa ngazi kwa Mtibwa Sugar leo Manungu?
Kikosi cha JKT Ruvu kinachotarajiwa kuvaana na Yanga leo Taifa, watakuwa mdebwedo tena kama msimu uliopita?
http://2.bp.blogspot.com/-vDZhKG3xDnU/VBW5w-uqd4I/AAAAAAABIvw/geeCj2-4uGg/s640/HERM5680.JPG
Yanga watakaokuwa wakijaribu bahati yao kwa JKT Ruvu leo Taifa, watacheka au kununa kama watani zao Simba?
BAADA ya jana timu ya Azam kushindwa kuwakimbia kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kulazimishwa sare ya kutofunga ana Prisons-Mbeya, Mtibwa Sugar leo ina nafasi ya kukalia kiti cha uongozi wa ligi hiyo kama itapata ushindi kwa Mgambo JKT mjini Morogoro.
Mtibwa inaikaribisha Mgambo kwenye uwanja wake wa Manungu, Turiani kati ya mechi mbili zinazopigwa leo kukamilisha raundi ya tatu ya ligi hiyo, pambano jingine likiwa ni kati ya Yanga dhidi ya JKT Ruvu.
Mchezo wa Yanga na JKT Ruvu utapigwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo kila timu itahitaji kupata ushindi ili kujiweka nafasi nzuri katika msimamo kabla ya mechi zao zijazo Oktoba 18 na 19 mwaka huu.
Yanga iliyoifumua Prisons-Mbeya kwa mabao 2-1 katika mechi ya mwisho ipo katika nafasi ya 10 kwa sasa ikiporomoshwa na watani zao Simba ambao jana walilazimishwa sare nyingine ya tatu japo wanalingana pointi tatu kila mmoja, ila uwiano wa mabao unawatenganisha Simba wakiwa juu.
Mtibwa ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi sita baada ya kushinda mechi zake mbili na kuwa timu pekee mpaka sasa iliyoshinda mfululizo baada ya Azam jana kulazimishwa sare na Prisons.
Kama itashinda Mtibwa itaweka rekodi ya kushinda kwa asilimia 100 mechi zake na kukwea kileleni kwa kukusanya pointi 9, japo huenda wakata miwa hao wasipate mteremko kwa Mgambo JKt ambayo inauguza kipigo cha bao 1-0 ilichopewa na Stand United mjini Tanga katika mechi yao iliyopita.
Mtibwa inayonolewa na kocha mzawa na nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Mecky Mexime inajivunia kuwa na wachezaji vijana wenye vipaji vya soka pamoja na kuongezewa nguvu wa makongwe kama Shaaban Nditi, Mussa Mgosi na Vincent Barnabas.
Kwa Yanga itakayokuwa jijini Dar itakuwa na kazi kubwa mbele ya maafande wa JKT Ruvu wanaonolewa na beki wao wa zamani, Fred Felix Minziro kuweza kuendeleza wimbi lao la ushindi.
Baada ya kunyukwa na Mtibwa katika mechi ya kwanza mjini Morogoro, Yanga ilizinduka kwa kuilaza Prisons na leo ingependa kushinda ili kuchupa hadi kwenye Tatu Bora kwani itafikisha pointi sita na kuivuka hata Mbeya City waliopo nafasi ya tatu kwa sasa na pointi zao tano.
Cha kufurahisha Genlson Santana 'Jaja' na Coutinho, pamoja na wakali wote wa Jangwani wapo fiti na kumpa afueni kocha Marcio Maximo kupanga kikosi anachokitaka kusaka ushindi wao wa pili msimu huu.
Hata hivyo vijana wa Minziro ambao wametoka kupokea kipigo toka kwa Kagera Sugar katika mechi iliyopita hawatataka kufanywa ngazi ya kuipandisha Yanga kwenye Tatu Bora kwani wapo nafasi ya pili toka mkiani wakiwa na pointi moja tu.
Kadhalika bado wanakumbuka katika mechi za msimu uliopita walibugizwa jumla ya mabao 9-2 baada ya mechi ya kwanza kufungwa 4-1 na alipokuja kuipokea timu, Minziro alishindiliwa mabao 5-1.
Ngoja tuone mechi hizo mbili za leo zitatoa matokeo gani ambayo yanaweza kupangua msimamo wa sasa ulivyo kama unavyoonekana hapo chini;
MSIMAMO LIGI KUU TANZANIA BARA 2014-2015
                                            P   W   D    L    F    A   GD   Pts
01. Azam                             03  02  01  00  05  01  +4   07
02. Mtibwa Sugar                02  02  00  00  05  01   +4   06
03. Mbeya City                   03  01  02  00  01   00  +1   05
04. Prisons                          03  01  01   01  03   02  +1   04
05.Kagera Sugar                 03  01  01   01  03   02 +1   04
06.Coastal Union                 03  01  01   01  04   04 00  04
07.Stand Utd                       03  01  01   01  03   05  -2   04
08. Ndanda Fc                    03  01  00   02  06   06  00  03
09.Simba                             03  00  03   00  04   04  00  03
10.Yanga                              02  01  00  01   02   02  00  03
11. Mgambo JKT                 02  01  00  01   01    01  00  03
12. Polisi Moro                     03  00  02  01   03   05   -2  02
13.JKT Ruvu                        02  00  01   01   00   02   -2  01
14. Ruvu Shooting                 03  00  01   02  00   04   -4  01

Manchester City yaifumua Aston Villa kwao


Yaya Toure akiwajibika uwanjani kabla ya kuifungia timu yake bao la kuongoza
Kosakosa langoni mwa Aston Villa
Ayaaa! Nimewekosaje
Kitu nyavuni bao la Toure  likiwaliza Villa
Kocha wa Villa haamini macho yake kama wanazamishwa nyumbani
City wakikoswakoswa na wenyeji wao
Aguero akitafuta bao

Mashine isiyochoka ikielekezwa cha kufanya uwanjani kuisaidia City
Sub ikifanyika kwa Villa
Lampard akianza mambo yake uwanjaniKun Aguero akishangilia bao la pili la Manchester City
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya England wamepata ushindi muhimu ugenini baada ya kuifumua Aston Villa mabao 2-0 na kujisogeza kwenye msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na Chelsea.
Magoli ya dakika 10 za mwisho za kipindi cha pili yalitosha kuwafanya watetezi hao kufikisha jumla ya pointi 14 na kukwea hadi nafasi ya pili wakiishusha Villa waliokuwa wakishika nafasi hiyo kabla ya kipigo hicho cha Manchester City.
Mabao ya washindi katika mchezo huo yaliwekwa kimiani na kiungo na Mwanasoka Bora wa Afrika, Yaya Toure dakika ya 82 kabla ya Sergio 'kun' Aguero kuongeza la pili dakika mbili kabla ya pambano hilo kumalizika.
Vikosi vilikuwa hivi:
Aston Villa: Guzan 8, Hutton 5, Senderos 6.5, Baker 7, Cissokho 6.5, Cleverley 5.5, Westwood 5, Delph 7, Richardson 7 (Grealish 71), Weimann 6 (Benteke 61, 6.5), N'Zogbia 6.5 (Bacuna 71) 
Man City: Hart 6, Zabaleta 6.5, Kompany 6.5, Mangala 7, Kolarov 7, Milner 6.5, Fernandinho 5.5 (Lampard 56, 6.5), Toure 7, Silva 7 (Navas 84), Dzeko 6 (Fernando 64, 6), Aguero 7.5

Simba bado gonjwa, Azam yabanwa, Ndanda yafa Tanga

Mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe akitafuta mbinu za kumtyoka mchezaji wa Stand Utd

Yalaaa! Ndivyo Emmanuel Okwi akilalama baada ya kuchezewa vibaya na mchezaji wa Stand

Shaaban Kisiga akifumua shuti mbele ya mchezaji wa Stand

Elias Maguli akiwa chini sambamba na beki wa Stand United katika mechi yao iliyoisha kwa sare ya 1-1
 
Mashabiki wa Coastal wakiangalia mpira
Manahodha wa Ndanda Fc na Coastal wakisalimianaKocha wa timu ya Coastal Union, Yusuf Chippo akihojiwa na wanahabari
Mashabiki wa timu ya Ndanda wakishindwa kuhamini macho yao ya kinachotokea baada ya kubugizwa bao 2.1 na Coastal katika uwanja wa Mkwakwani
Shabiki wa Ndanda aliyejitambulisha kwa jina la Kadio Rashidi akiwa amejichora mgongoni kuisapoti timu yao ambayo hata hivyo ililala Mkwakwani kwa mabao 2-1.

Raia wa kigeni kutoka mataifa mbalimbali wakifatilia mpambano wa Ndanda na Coastal uliokuwa ukipigwa katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.


Raia wa kigeni kutoka mataifa mbalimbali wakifatilia mpambano wa Ndanda na Coastal uliokuwa ukipigwa katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.
****
WAKATI mabingwa watetezi wakibanwa mjini Mbeya baada ya kulazimishwa suluhu na maafande wa Prisons, huku Ndanda Fc ikizamishwa uwanja wa Mkwakwani na Coastal Union kwa kufungwa mabao 2-1, hali bado si shwari kwa Simba baada ya kulazimishwa sare ya tatu mfululizo katika Ligi Kuu Tanzania Bara.
Simba ilishindwa kufurukuta mbele ya wageni wa ligi hiyo, Stand United ya Shinyanga na kutoka nao sare ya bao 1-1 ikiwa ni sare ya tatu tangu ligi ya msimu huu ianze na kuleta hali ya taharuki kwa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kongwe.
Simba ndiyo waliyokuwa wa kwanza kupata bao kama ilivyo katika mechi zao mbili za awali dhidi ya Coastal Union na Polisi Moro baada ya kiungo Shaaban Kisiga kudhihirisha kuwa 'utu uzima' dawa kwa 'kukusanya kijiji' kabla ya kufunga bao tamu lililoifanya Simba iwe mbele.
Hata hivyo dakika za mwishoni kuelekea mapumziko wageni Stand walichomoa bao hilo na kufanya timu ziende kupumzika zikiwa nguvu sawa, hali iliyoendelea hata katika kipindi cha pili na hadi mwisho wa pambano hilo na kuiacha Simba ikikusanya pointi tatu katika mechi tatu.
Katika mechi nyingine mjini Mlandizi, Ruvu Shooting ikiwa nyumbani iliambulia pointi yake ya kwanza baada ya kulazimishwa suluhu na Mbeya City katika pambano lililochezwa uwanja wa Mabatini, Mlandizi, huku Azam wakilazimishwa sare kama hiyo mjini Mbeya na maafande wa Prisons katika uwanja wa Sokoine.
Kwenye uwanja wa Mkwakwani, Coastal Union ilizinduka katika ligi hiyo kutoka kwenye kipigo kwa kuizamisha Ndanda Fc ya Mtwara kwa mabao 2-1. Mabao ya washindi katika mechi hiyo yalifungwa na Joseph Mahundi sekunde chache baada ya pambano kuanza na jingine kupitia Hussein Sued dakika ya 26 kabla ya Ndanda kuchomoa bao moja katika kipindi cha pili kupitia Nassor Kapama.
Maafande wa Polisi Moro wakiwa uwanja wao wa nyumbani wa Jamhuri Morogoro waliambulia pointi moja baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya wageni wao Kagera Sugar. Wenyeji walianza kufunga bao kupitia Nicolaus Kabipe kabla ya Kagera Sugar kuchomoa 'jioni' kupitia Rashidi Mandawa.

Liverpool yazinduka England, Sunderland yaua

Jordan Henderson (kulia) akishangilia bao lake la pili baada ya kufanya 2-1 dhidi ya West Brom AlbionTIMU ya Liverpool imezinduka kwenye Ligi Kuu ya England baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 nyumbani dhidi ya West Bromwich Albion.
Mabao ya washindi yalifungwa na Adam Lallana na Jordan Henderson, wakati lile la wageni lilifungwa kwa mkwaju wa penati na  Saido
Berahino. 
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Hull City ikiwa nyumbani iliitambia Crystal Palace kwa mabao 2-0, huku Leicester City ikibanwa kwao kwa kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Burnley.
Nayo Sunderland ikiwa nyumbani iliiua Stoke City kwa kuizamishwa kwa mabao 2-1 na Swansea City kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Newcastle United.

Hatari! Jenereta laua baba, mama na watoto

Mwili wa mama, na wa mmoja wa watoto unaonekana kwa mbali nyuma yakeMume, mke na watoto wao watatu wamefariki dunia baada ya kupumua hewa iliyojaa gesi ya “carbon monoxide” iliyokuwa ikitolewa na generator waliloliwasha ndani ya nyumba yao .
Katika dhahama hiyo iliyotokea Lagos, Nigeria, miili ya wahanga wote watano iligunduliwa na majirani zao. Majirani wameripoti kuwa baba wa familia hiyo alinunua generator siku mbili kabla ya kukutwa na umauti, na kuliweka chumbani kwake akihofia kuwa litaibwa akiliweka nje.

Siku iliyofuatia, majirani waligundua kuwa wanafamilia hao wote walikuwa kimya, na ndani ya nyumba yao siku nzima, hivyo mmoja wao akaamua kuangalia kujua kinachoendelea. Jirani huyo aliona miili ya marehemu, na kuwataarifu wenzake. Walipoingia ndani ya nyumba, walistushwa na janga walilokutana nalo.
Katika moshi unaotolewa na majenereta, kama wa mkaa, magari, pikipiki, na mashine nyingi, kuna gesi ya “carbon monoxide (CO)” ambayo, ni sumu inayokusababisha kuchoka, kupoteza fahamu, na hatimaye kufariki taratibu bila onyo, maumivu, wala kujijua. Utadhani unapata usingizi na kujilaza, kumbe ndio mauti yanakukuta. Uthithubutu kupika kwa kutumia mkaa ndani ya nyumba bila kufungua madirisha, au kuwasha jenereta ndani ya nyumba, au kuwasha gari katika “garage” wakati madilisha na milango imefungwa; maana hiyo ni sawa na kucheza na kifo. Gesi ya carbon monoxide ni tofauti na carbon dioxide (CO2) inayopumuliwa na wanyama, ambayo si sumu na inatumiwa na mimea katika photosynthesis.
Miili ya watoto watatu wa familia hiyo.