STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, October 5, 2014

Juventus yaizamisha As Roma, Tevez moto chini!

https://s.yimg.com/bt/api/res/1.2/etgxU0ykbfbKLMs4UzzcCw--/YXBwaWQ9eW5ld3M7cT04NTt3PTYzMA--/http://l.yimg.com/os/publish-images/sports/2014-10-03/dba924d0-4b36-11e4-9a01-6d10b444caf4_Totti_Juve_0310.jpgCARLOS Tevez amezidi kung'ara nchini Italia baada ya jioni ya leo kuifungia timu yake ya Juventus mabao mawili wakati 'Kibibi cha Turin' kikiwazima As Roma kwa mabao 3-2 kwenye pambano la kusisimua la Seria A, huku timu zote mbili zikicheza pungufu wa mchezaji mmoja mmoja baada ya wachezaji wao kupewa kadi nyekundu kwa nyakati tofauti kutokana na madhambi.
Tevez ambaye amekuwa akichuniwa kuitwa katika timu ya taifa ya Argentina, alifunga mabao yake yote kwa mikwaju ya penati katika dakika ya 27 na 45 wakati bao jingine likiwekwa kimiani na Bonucci dakika nne kabla ya pambano hilo kumalizika.
Mabao ya wageni yalifungwa na Francisco Totti pia kwa mkwaju wa penati dakika ya 32 na Iturbe dakika ya 44.
Kwa ushindi huo Juventus wamezidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 18 tatu zaidi ya wapinzani wao hao waliokuwa wametofautiana mabao ya kufunga na kufungwa kwenue msimamo huo.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo mapema leo mchana Empoli ikiwa nyumbani ilipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Palermo, huku Lazio ikiizamisha Sassuolo kwa mabao 3-2 waliowafuata nyumbani kwao, Parma walikubali kipigo cha magoli 2-1 dhidi ya wageni wao Genoa na Atalanta ikafa ugenini kwa bao 1-0 dhidi ya Sampdoria.
Timu za Udinese na Cesena zilitoshana nguvu kwa kufunga bao 1-1 na hivi sasa kuna mechi mbili zinachezwa ambazo hata hivyo haziwezi kubadilisha msimamo wa nafasi za juu za ligi hiyo.No comments:

Post a Comment