STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, October 5, 2014

AC Milan yazinduka Italia, Muntari aibeba Juve, Roma leo

Sulley Muntari
Sulley Muntari
BAADA ya kucheza mechi tatu bila ushindi hatimaye mabingwa wa zamani wa Italia na Ulaya, AC Milan imezinduka kwenye Ligi Kuu ya Italia Seria A baada ya kupata ushindi mujarabu nyumbani kwao dhidi ya Chievo Verona.
AC Milan inayonolewa na mshambuliaji nyota wa zamani wa timu hiyo na Azzurri timu ya taifa ya Italia, Philip Inzaghi 'Pipo' ilipata ushindiwa mabao 2-0 kwenye uwanja wa Giuseppe Meazza, mjini Milano kupitia mabao ya Sulley Muntari aliyefunga dakika ya 55 na Keisuke Honda aliyeongeza la pili kwa mkwaju wa adhabu ndogo dakika ya 78 na kuifanya Milan kufikisha jumla ya pointi 11 na kuchupa hadi nafasi ya nne ya msimamo wa ligi hiyo unaoongozwa na Juventus.
Katika mechi nyingine iliyochezwa jana katika mfululizo wa ligi hiyo timu Hellas Verona ilipata ushindi mwembamba nyumbani wa bao 1-0 dhidi ya Cagliari.
Kipute cha ligi hiyo kitaendelea leo kwa michezo nan, Empoli itaumana na Palermo, Lazio dhidi ya Sassuolo, Parma itaikaribisha Genoa, Sampodoria itaialika Atalanta, wakati Udinese itaumana na Cesena.
Mechi nyingine ni kati ya vinara wa ligi hiyo Juventus na As Roma zenye pointi 15 kila mmoja zitakapochuana mjini Turin nyumbani kwa Juve, wakati Fiorentina itaumana na Inter Milan na Napoli itaikaribisha Torino.

No comments:

Post a Comment