Mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe akitafuta mbinu za kumtyoka mchezaji wa Stand Utd |
Yalaaa! Ndivyo Emmanuel Okwi akilalama baada ya kuchezewa vibaya na mchezaji wa Stand |
Shaaban Kisiga akifumua shuti mbele ya mchezaji wa Stand |
Elias Maguli akiwa chini sambamba na beki wa Stand United katika mechi yao iliyoisha kwa sare ya 1-1 |
Mashabiki wa Coastal wakiangalia mpira
Manahodha wa Ndanda Fc na Coastal wakisalimiana |
Kocha wa timu ya Coastal Union, Yusuf Chippo akihojiwa na wanahabari
Mashabiki wa timu ya Ndanda wakishindwa kuhamini macho yao ya
kinachotokea baada ya kubugizwa bao 2.1 na Coastal katika uwanja wa
Mkwakwani
Shabiki wa Ndanda aliyejitambulisha kwa jina la Kadio Rashidi akiwa amejichora mgongoni kuisapoti timu yao ambayo hata hivyo ililala Mkwakwani kwa mabao 2-1.
Raia wa kigeni kutoka mataifa
mbalimbali wakifatilia mpambano wa Ndanda na Coastal uliokuwa ukipigwa
katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.
Raia wa kigeni kutoka mataifa mbalimbali wakifatilia mpambano wa Ndanda na Coastal uliokuwa ukipigwa katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.
****
WAKATI mabingwa watetezi wakibanwa mjini Mbeya baada ya kulazimishwa suluhu na maafande wa Prisons, huku Ndanda Fc ikizamishwa uwanja wa Mkwakwani na Coastal Union kwa kufungwa mabao 2-1, hali bado si shwari kwa Simba baada ya kulazimishwa sare ya tatu mfululizo katika Ligi Kuu Tanzania Bara.
Simba ilishindwa kufurukuta mbele ya wageni wa ligi hiyo, Stand United ya Shinyanga na kutoka nao sare ya bao 1-1 ikiwa ni sare ya tatu tangu ligi ya msimu huu ianze na kuleta hali ya taharuki kwa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kongwe.
Simba ndiyo waliyokuwa wa kwanza kupata bao kama ilivyo katika mechi zao mbili za awali dhidi ya Coastal Union na Polisi Moro baada ya kiungo Shaaban Kisiga kudhihirisha kuwa 'utu uzima' dawa kwa 'kukusanya kijiji' kabla ya kufunga bao tamu lililoifanya Simba iwe mbele.
Hata hivyo dakika za mwishoni kuelekea mapumziko wageni Stand walichomoa bao hilo na kufanya timu ziende kupumzika zikiwa nguvu sawa, hali iliyoendelea hata katika kipindi cha pili na hadi mwisho wa pambano hilo na kuiacha Simba ikikusanya pointi tatu katika mechi tatu.
Katika mechi nyingine mjini Mlandizi, Ruvu Shooting ikiwa nyumbani iliambulia pointi yake ya kwanza baada ya kulazimishwa suluhu na Mbeya City katika pambano lililochezwa uwanja wa Mabatini, Mlandizi, huku Azam wakilazimishwa sare kama hiyo mjini Mbeya na maafande wa Prisons katika uwanja wa Sokoine.
Kwenye uwanja wa Mkwakwani, Coastal Union ilizinduka katika ligi hiyo kutoka kwenye kipigo kwa kuizamisha Ndanda Fc ya Mtwara kwa mabao 2-1. Mabao ya washindi katika mechi hiyo yalifungwa na Joseph Mahundi sekunde chache baada ya pambano kuanza na jingine kupitia Hussein Sued dakika ya 26 kabla ya Ndanda kuchomoa bao moja katika kipindi cha pili kupitia Nassor Kapama.
Maafande wa Polisi Moro wakiwa uwanja wao wa nyumbani wa Jamhuri Morogoro waliambulia pointi moja baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya wageni wao Kagera Sugar. Wenyeji walianza kufunga bao kupitia Nicolaus Kabipe kabla ya Kagera Sugar kuchomoa 'jioni' kupitia Rashidi Mandawa.
No comments:
Post a Comment