KLABU ya soka ya Yanga wameendelea kuwapa raha mashabiki wao baada ya jioni hii kupata ushindi muhimu wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Ruvu na kuendeleza ubabe kwake kwa maafande hao katika Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga ilipata ushindi huo kwenye uwanja wa Taifa na kuifanya timu hiyo kuchupa hadi nafasi ya tatu ya msimamo ikizipumulia timu za Mtibwa na Azam waliopo mbele yao.
Beki Kelvin Yondani aliianza kuiandika Yanga bao dakika ya 37 kwa mkwaju mkali ulioifanya timu yake kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao hilo.
Kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Niyonzima aliiongezea Yanga bao kipindi cha pili kabla ya Jabir Aziz kuifungia JKT Ruvu bao la kufutria machozi dakika chache kabla ya mapumziko.
Kwa ushindi huo Yanga imefikisha pointi sita wakati JKT wamendelea kusalia kwenye nafasi ya pili toka mkiani kutokana na kuwa na pointi mopja sawa na ndugu zao wa Ruvu Shooting Stars.
Mechi ijayo kwa Yanga itakuwa ni kati yao na watani zao Simba ambao wapo katika hali mbaya kwa kutoka sare katika mechi tatu mfululizo kiasi cha kubatizwa jina la wazee wa sare na watani zao.
No comments:
Post a Comment