Mwili wa mama, na wa mmoja wa watoto unaonekana kwa mbali nyuma
yakeMume, mke na watoto wao watatu wamefariki dunia baada ya kupumua
hewa iliyojaa gesi ya “carbon monoxide” iliyokuwa ikitolewa na generator
waliloliwasha ndani ya nyumba yao .
Katika dhahama hiyo iliyotokea Lagos, Nigeria, miili ya wahanga wote
watano iligunduliwa na majirani zao. Majirani wameripoti kuwa baba wa
familia hiyo alinunua generator siku mbili kabla ya kukutwa na umauti,
na kuliweka chumbani kwake akihofia kuwa litaibwa akiliweka nje.
Siku iliyofuatia, majirani waligundua kuwa wanafamilia hao wote walikuwa
kimya, na ndani ya nyumba yao siku nzima, hivyo mmoja wao akaamua
kuangalia kujua kinachoendelea. Jirani huyo aliona miili ya marehemu, na
kuwataarifu wenzake. Walipoingia ndani ya nyumba, walistushwa na janga
walilokutana nalo.
Katika moshi unaotolewa na majenereta, kama wa mkaa, magari, pikipiki,
na mashine nyingi, kuna gesi ya “carbon monoxide (CO)” ambayo, ni sumu
inayokusababisha kuchoka, kupoteza fahamu, na hatimaye kufariki taratibu
bila onyo, maumivu, wala kujijua. Utadhani unapata usingizi na
kujilaza, kumbe ndio mauti yanakukuta. Uthithubutu kupika kwa kutumia
mkaa ndani ya nyumba bila kufungua madirisha, au kuwasha jenereta ndani
ya nyumba, au kuwasha gari katika “garage” wakati madilisha na milango
imefungwa; maana hiyo ni sawa na kucheza na kifo. Gesi ya carbon
monoxide ni tofauti na carbon dioxide (CO2) inayopumuliwa na wanyama,
ambayo si sumu na inatumiwa na mimea katika photosynthesis.
Miili ya watoto watatu wa familia hiyo.
Poleni wahanga wa tukio hili la kusikitisha
ReplyDelete