STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, October 25, 2013

Nimeteseka vya kutosha, nisaidieni jamani ili niishi kama watoto wengine

Mtoto Honrina akionyesha kinyama kilichoota kwenye ulimi wake na kumfanya awe na ndimi mbili
 KWA namna maradhi yanayomsumbua 'yalivyoutafuna' mwili wake hasa maeneo ya usoni, kichwani na mgongoni ni vigumu kwa mtu mwenye roho na moyo mwepesi kumtupia jicho mara mbili kumuangalia.
Muonekano wake unatisha na kuogofya mbali na kutia simanzi na kuonyesha namna gani mtoto Honorina Christian (11)  anavyoumia na kuishi katika hali ya MATESO na MAUMIVU.
Kwa kinywa chake mwenyewe mtoto huyo kwa sauti ya upole anasema kuwa AMECHOKA kuishi kwa MATESO na anahitaji asaidiwe ili naye aishi kwa furaha kama watoto wengine.
Anasema maumivu anayoyapata kupitia vidonda alivyonavyo yanayotafuna ngozi yake yanamnyima raha na kumpa mateso makubwa na kwamba hana analoweza kukiokoa katika hali hiyo kama siyo serikali, watu wenye uwezo na wasamaria wema ambao wataguswa na hali yake.
"Naumia...Nateseka na sijui niseme nini. Nawaomba Watanzania kuanzia Rais, Wabunge, Mawaziri na watu waliojaliwa uwezo wanisaidie niweze kupata matibabu, nimeteseka vya kutosha, ninateseka sana na ugonjwa huu..." Honorina alisema huku akianza kulia kwa simanzi.
Anasema anapenda kurudi darasani kusoma baada ya kukwama akiwa darasa la pili baada ya kushindwa kuona kufuatia kupasuliwa jicho lake la kushoto.
"Nataka kusoma....Naomba nisaidieni...naumia sana ...."Honorina anaomboleza huku akiwa amejifunika kofia pana inayokinga kichwa chake ambacho kimetafunwa na kuacha madonda ya kuogofya.
Mama yake mzazi aliyebeba jukumu la kuhangaika na Honorina baada ya mzazi mwenzie Christian kufariki kwa ajali ya gari mwaka 2007, Grace John anasema hali ya mwanaye inamsikitisha na kumliza kila mara kwani anaamini inapa mateso makubwa mtoto wake huyo wa kwanza kati ya watatu aliyezaa na mzazi mwenzake.
Grace anasema tangu kuzaliwa kwa mwanaye kulikuwa na mambo ya kushangaza, lakini hakujua kama yangefikia hapo walipo sasa.
Akisimulia kwa simanzi, Grace anasema Honorina alizaliwa Juni 12 mwaka 2002 katika Hospitali ya Morogoro akiwa na afya njema, isipokuwa mwili wake mzima ukiwa umekaa nywele kama mwili wa mnyama.
"Hali hii ilinitisha mno kwa namna mwili mzima wa mtoto kujaa nywele, lakini nilielezwa hiyo haina tatizo na hivyo kuruhusiwa kurudi na mwanangu nyumbani nikiwa na furaha na mwenzangu (mwanaume aliyezaa naye),
Grace anasema na kuongeza kuwa, baada ya mwezi mmoja nywele hizo zote zilipukutika na kuiacha ngozi ya mtoto wake ikiwa na madoa madoa kama ngozi ya Chui jambo lililowatisha na kulazimika kurejea tena hospitali ya Morogoro na kupewa mafuta ya kumpaka kusaidia kurekebisha tatizo hilo.
"Kingine cha ajabu ni kwamba kadri alivyokuwa akikuwa ndivyo mtoto wake alivyokuwa akizidi kubadilika ikiwemo  kugundua ana ndimi saba na pia kuna vitu vigumu vilivyojitokeza pembeni ya kichwa chake kama pembe za mbuzi," anasema.
Anasema hali hiyo iliwatisha na kuhangaika kutafurta matibabu, lakini wakati wakitafuta namna ya kumsaidia baba wa mtoto huyo aliyekuwa amezaa naye mtoto mwingine wa pili aitwaye Dickson ambaye kwa sasa ana miaka 9 na kumuachia mimba ya miezi saba alipata ajali na kufa mwaka 2007.
Anadai baada ya kujifungua mwanae wa tatu akiwa anaishi katika nyumba aliyojenga na mwenzake, alienda hiospitali kumtibia mwanae baada ya jicho lake la kushoto kupoteza kiini cheusi na kushauriwa kwenda CCBRT waliomfanyia upasuaji katika jicho hilo mwaka 2008 wakati Honorina akiwa darasa la pili.
"Bahati mbaya upasuaji huo ulisababisha mwanangu kupoteza uwezo wa kuona na hivyo kurudi nyumbani na kuanza kumlea kama asiyeona kwani jicho lake jingine pia halikuwa na uwezo mzuri wa kuona mpaka sasa," anasema na kuongeza hata hivyo mwaka mmoja na ushei mwanae alianza kuota pembe.
Anadai alimpeleka hospitali ya KCMC ambapo alifanyiwa upasuaji, lakini ikamuacha mwanaye akiwa matundu wazi katika mifupa iliyokatwa na kuwalazimisha madaktari kukata nyama za paja kuziba eneo hilo na puani kulikokuwa kukimomonyoka kila uchao.
"Yaani sijui mpaka sasa mwanangu amekuwa na kitu gani kwani nyama za pua zilikuwa pia zikimomonyoka na kumdondoka na pia kuota ndimi za ziada na kufukia saba, ambazo hata hivyo zilikatwa na kubakishwa moja ambayo hata hivyo kwa sasa imeongezeka nyingine," anasema Grace kwa huzuni.
Anasema baada ya kuwauliza madaktari kwa kuwabembeleza sana juu ya ugonjwa wa mwanae walimueleza kuwa alizaliwa kama mlemavu wa ngozi (Albino Mweusi).
"Walinieleza mwanangu ni Albino Mweusi na kwamba hawana cha kumsaidia ila kumpa dawa za kupaka kabla ya kushauriwa nije Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu zaidi Hospitali ya Muhimbili ambapo hata hivyo hakuna cha maana alichofanyiwa mwanangu zaidi ya kuambiwa nirudi naye nyumbani," anasema.
Anasema  kwa kifupi amesumbuka na mwanaye na kukata tamaa asijue nini hatima ya Honolina, ambaye kwa hali yake imemfanya asiweze kufanya kazi yoyote ili kuhangaika naye kumtafutia matibabu, huku wanawe wengine wakiishi kwa mateso Mgeta-Morogoro kwani yeye mwenyewe (mama) hana ndugu wa kumsaidia.
"Sina mtu wa kunisaidia, baada ya nyumba niliyojenga na mzazi mwenzangu kuuzwa na mama mkwe kwa madai ni mali ya mtoto wao, nimekuwa natangatanga nimepanga mara mbili nyumba ya kwanza nilifukuzwa kwa kukosa kodi ya kuendelea kuishi kabla y kujipigapiga na kupata hapo Mgeta nilipowaacha watoto," anasema.
Anasema kwa jijini Dar es Salaam amekuwa akiishi kama ombaomba eneo la Ubungo ili kukidhi mahitaji yake na ya mwanaye na kudai hali hiyo imemchosha na kuungana na mwanae kuililia serikali na watu wengine wenye uwezo kumsaidia fedha za matibabu ili mwanaye atibiwe na kupona naye apumue.
"Kama mtoto anavyokueleza, nawaomba wasamaria wema, serikali na watu wenye uwezo watusaidie.. wanichangie nimuokoe mwanangu...miaka 11 ya mateso nadhani inatosha, sitaki kumpoteza mwanangu nampenda katika hali aliyonayo," anasema Grace akilengwalengwa na machozi.
Anasema hajui mwanaye alipatwaje na matatizo hayo ilihali wanae wengine waliomfuata wapo vyema kiafya bila tatizo lolote.
"Huyu ni mtoto wangu wa kwanza kuzaa na Christian niliyezaa naye watoto watatu, wengine ni Dickson (9) na mwisho aliniacha nikiwa mjamzito wa mimba yake ni Francis (6), ambao wote hawana tatizo kama dada yao, hili ndilo linalonishangaza na kuendelea kuwalilia wasamaria wema wanisaidie kumuokoa mwanangu," anasema.
Grace anayedai wapo baadhi ya watu wamekuwa wakimnyanyapaa kwa hali ya mwanae ambaye amejaa vidonda ambavyo vinatoa harufu kali, lakini akawakumbusha kuwa hayo ni matatizo ambayo hakuna aliyeyaomba pia akirejea usemi kwamba 'Hujafa Hujaumbika'.
Anamalizia kwa kumuomba yeyote atakayeguswa na tatizo la mwanae anaweza kumsaidia kwa kuwasilisha michango yao kupitia MICHARAZO MITUPU ama simu za mkononi za mama huyo za 0719-749542, 0687-402694 na 0762-425973. kwa huduma za Tigo-Pesa, M-Pesa au Airtel Money.

Msanii Bongo Movia anusurika 'kuliwa Kiboga', kisa pombe


MUIGIZAJI wa flamu za kibongo anayejulikana kwa jina la Danny Cloud maarufu kama Danny mtoto wa mama ambaye alipata umaarufu wa jina hilo kupitia filamu ya mtoto wa mama amenusurika kubakwa ( kuliwa kiboga )
Akizungumza na mwandishi wetu, rafiki wa karibu wa msanii huyo alidai kwamba Danny alikuwa maeneo ya Bilcanas ambapo alipewa ofa ya pombe na jamaa zake...
Rafiki huyo alidai kuwa, baada ya kupewa ofa hiyo adimu, msanii huyo alianza kuiparamia pombe mfano wa mtu mwenye kiu kali ya maji, hali iliyomfanya asijitambue na kuanza kuvua nguo...
"Kuna wakati Danny alinyanyuka na kuelea chooni huku akipepesuka...Alipofika huko alidondoka na kulala huko huko chooni, hali iliyowafanya vibaka watake kumla kiboga"...Alisema huyo rafiki yake na kuongeza:
"Baada ya kimya kirefu, ilibidi tukamwangalie ambapo tuliwakurupusha vijana watatu wakiwa wameshamvua nguo"
Source: Vituko Vya Mtaa

Wapinzani wa Twiga Stars U20 kutua nchini leo


TIMU ya Taifa ya wanawake kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 inawasili nchini leo (Ijumaa, Oktoba 25 mwaka huu) saa 8.30 mchana tayari kwa mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza ya Kombe la Dunia dhidi ya Tanzania itakayofanyika kesho Jumamosi (Oktoba 26 mwaka huu). 
Msumbiji itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ndege ya LAM ikiwa na msafara wa watu 25 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi. Timu hiyo itafikia kwenye hoteli ya Sapphire iliyopo maeneo ya Gerezani, Dar es Salaam. 
Mara baada ya kuwasili JNIA, kocha na nahodha wa timu hiyo watazungumza na waandishi wa habari juu ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni. 
Kwa upande wa U20 chini ya Kocha Rogasian Kaijage imejiandaa vizuri kwa ajili ya mechi hiyo, na leo saa 10 jioni itafanya mazoezi yake ya mwisho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Viingilio kwa mechi hiyo ni sh. 1,000 kwa viti vya rangi ya kijani, bluu na rangi ya chungwa. Viingilio vingine ni sh. 2,000 kwa VIP C, sh. 5,000 kwa VIP B wakati VIP A itakuwa sh. 10,000. 
Kamishna wa mechi hiyo Evelyn Awuor kutoka Kenya tayari amewasili nchini wakati waamuzi kutoka Burundi waliwasili jana saa 1 usiku kwa ndege ya Kenya Airways wakiunganishia safari yao Nairobi, Kenya. Maofisa wote wa mechi hiyo wanafikia hoteli ya New Africa.

Uchaguzi wa Bodi ya Ligi Kuu kufanya asubuhi hii

Uchaguzi wa Bodi ya Ligi Tanzania (Tanzania Professional League- TPL Board) unafanyika asubuhi ya leo (Oktoba 25 mwaka huu) kwenye ukumbi wa mikutano uliopo Golden Jubilee Tower kuanzia saa 3 asubuhi. 
Mgeni rasmi katika mkutano huo wa Bodi ya TPL ambao unafanyika kwa mara ya kwanza atakuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga. 
Kwa mujibu wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, wajumbe wanaounda Mkutano wa Uchaguzi ni wenyeviti kutoka klabu 24 za Ligi Daraja la Kwanza (FDL), na 14 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL). 
Viongozi wa klabu za FDL wamefikia hoteli ya Royal Valentino iliyoko Barabara ya Uhuru wakati wale wa VPL ambao pia watashiriki Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wamefikia hoteli ya Landmark iliyopo Ubungo. 
Wagombea kwenye uchaguzi huo ni Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti), Said Muhammad Said Abeid (Makamu Mwenyekiti) wakati wanaoumba ujumbe wa Kamati ya Uendeshaji ni Khatib Omari Mwindadi na Kazimoto Muzo.

MSAIDIE MTOTO HUYU, MATESO YA MIAKA 11 IMETOSHA KWAKE

Ndivyo mtoto Honolina Cristian anavyoonekana kwa karibu

Kama umejaliwa uwezo kwa nini usitoe kwa mtoto huyu akatibiwe upate Thawabu

Hivi ndivyo mtoto huyu anavyoteseka na madonda

Mtoto akionyesha ulimi ulioota tena baada ya awali kukatwa
HUJAFA Hujaumbika! Mtoto Honolina Christian (11) yupo kwenye mateso makubwa na amewalilia Watanzania wote kuanzia Rais Jakaya Kikwete, serikali yake nzima na wanajamii akiwaomba msaada wa kumwezesha apate matibabu yatakayookoa maisha yake.
Mtoto huyo ambaye huwezi kumuangalia mara mbili bila kutokwa na machozi alisema tumaini lake ni kwa watu watakaoguswa na kilio chake akidai ameteseka vya kutosha na hivyo anadhani umefika muda na yeye afurahie maisha kama watoto wengine.
Akizungumza na MICHARAZO akiwa ameongozana na mama yake, mtoto Honolina alisema maumivu anayopata kwa madonda yanayoitafuna ngozi yake yanamnyima raha na angeomba asaidiwe aweze kwenda kufanyiwa matibabu nje ya nchi ili na yeye apumue.
"Naumia...Nateseka na sijui niseme nini. Nawaomba Watanzania kuanzia Rais, Wabunge, Mawaziri na watu waliojaliwa uwezo wanisaidie niweze kupata matibabu, nimeteseka na ninateseka sana na ugonjwa huuu..." Honolata alisema huku akianza kulia kwa simanzi.
Mama yake mzazi aliyeambatana na mtoto huyo, Grace John alisema tangu mwanaye azaliwa Juni 12, 2002 hajawahi kufurahia maisha kutokana na maradhi yaliyomuandama katika namna ya ajabu kabisa.
"Kwanza alizaliwa akiwa amejaa nywele mwili mzima na baadaye nywele hizo kupukutika kisha mwili mzima kuwa kama ngozi ya chui na kumkimbiza hospitali ya Morogoro alipopewa mafuta ya ngozi kumtibia," alisema.
Mkazi huyo wa mkoani Morogoro, anasema tangu hapo mwanaye amekuwa akiteseka na kuharibika ngozi ikiwemo kuota pembe mbili kichwani na kuwa na ndimi saba zilizofanyiwa upasuaji KCMC kabla ya mapembe hayo kumuacha na mashimo kichwani yaliyolazimisha azibwe kwa ngozi ya pajani.
"Kifupi ni kwamba nimehangaika sana na mwanangu huyu, tangu akiwa mchanga mpaka leo, bahati mbaya ni kwamba baba yake mzazi alifariki mwaka 2007 na kuniachia mzigo ambao kwa hakika nimeuvumilia na kushindwa kujua mwishowe utakuwaje," alisema Grace.
Grace aliongeza alikuja jijini Dar mwezi uliopita kwa ajili ya matibabu ya mtoto wake huyo katika Hospitali ya Muhimbili, lakini aliambiwa arejee nyumbani na mwanaye akielezwa mwanae ni mlemavu wa ngozi mweusi (Albino Mweusi).
"Kama mtoto anavyokueleza, nawaomba wasamaria wema, serikali na watu wenye uwezo watusaidie.. wanichangie nimuokoe mwanangu...miaka 11 ya mateso nadhani inatosha, sitaki kumpoteza mwanangu nampenda katika hali aliyonayo," alisema Grace akilengwalengwa na machozi.
Alisema huyo ni mmoja wa watoto wake watatu aliozaa na mwanaume ambaye bahati mbaya hakufunga naye ndoa kabla ya kufa kwa ajali ya gari wakati wakiendelea kuhangaikia kwa pamoja matibabu ya Honolina.
"Huyu ni mtoto wangu wa kwanza kuzaa na Christian niliyezaa naye watoto watatu, wengine ni Dickson (9) na mwisho aliniacha nikiwa mjamzito wa mimba yake ni Francis (6), ambao wote hawana tatizo kama dada yao," alisema.
Alisema watoto wake hao kwa sasa wanaishi pekee yao Mgeta, Morogoro wakati yeye akihangaika na Honolina apate matibabu, akidokeza pia nyumba aliyokuwa amejenga na 'mumewe' imeuzwa na mama mkwe wake na hivyo kumfanya kuwa na wakati mgumu kwa vile ana pa kuishi na hana shughuli ili kumtibia mwanae.
Aliongeza kwa yeyote atakayeguswa na tatizo la mwanae anaweza kumsaidia kwa kuwasilisha michango yao ama kwa MICHARAZO MITUPU au kupitia simu zake za mkononi kwa huduma za Tigo-Pesa, M-Pesa au Airtel Money kwa namba 0719-749542, 0687-402694 na 0762-425973.
NB:Makala ndefu ya mtoto huyu itawajia baadaye kidogo, unaweza kulia kwa jinsi inavyosikitisha