STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, December 18, 2014

Chelsea wapewa Liverpool Kombe la Ligi, Spur v Sheffield Utd


http://i2.mirror.co.uk/incoming/article4591109.ece/alternates/s615/Liverpool-v-Chelsea.jpg
Kivumbi kitakuwa kwao Januari 20/27
http://www.capitalonecup.co.uk/cms_images/trophypitchside800x600304-589134_478x359.jpg
DROO ya Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Ligi maarufu kama Capital One, imetoka ikionyesha kuwa Chelsea watakutana uso kwa uso na Liverpoo ambayo usiku wa jana ilipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya timu ya AFC Bournemouth.
Vijogoo vya London ya Kaskazini, Tottenham Hotspur walioifumua Newcastle United kwa mabao 4-0 yenyewe imepangwa kumenyana na Sheffiled United katika hatua hiyo ya nusu fainali.
Chelsea walioilaza Derby Count mabao 3-1 wataanzia ugenini kwenye uwanja wa Anfield na kama mambo yataenda kwa sare watarudi nyumbani kuivutia pumzi wapinzani wake.
Kwa upande wa Spurs wenyew wataanza nyumbani kabla ya kumalizia ugenini na mechi za mkondo wa kwanza zitachezwa Januari 20, 2015 na zile za marudiano kujua timu mbili zitakazocheza fainali.

Polisi yazuia mazishi ya Aisha Madinda, kisa....!

HABARI zilizopatikana hivi punde zinasema kuwa Jeshi la Polisi limesitisha kufanyika kwa mazishi ya aliyekuwa Mnenguaji wa bendi za African Stars 'Twanga Pepeta' Aisha Madinda,ili kufanya uchunguzi wa kina juu ya kifo chake.
Akihojiwa katika kipindi cha XXL, mtoto mkubwa wa marehemu alisema wamekubaliana na serikali wafanye uchunguzi wa kinaili hata kama akizikwa basi azikwe ikifahamika kipi kilichomuua, kwa sababu mama yake hakuwa mgonjwa kabla ya kukumbwa na mauti.
Tangu jana baada ya kusambaa kwa kifo cha mnenguaji huyo aliyepitia makundi mbalimbali kabla ya kutua katika shoo za bendi, kulikuwa na maelezo ya kutatanisha juu ya kifo chake na mtoto huyo wa marehemu, aitwaye Feisal Mbegu alinukuliwa kuwa mama yake hakuwa mgonjwa na aliwasiliana naye jana yake akiwa buheri wa afya.
Inaelezwa kuwa mwili wa Aisha Madinda ulipelekwa hospitali ya Mwananyamala akiwa keshafariki na mwanamke mmoja anayetajwa kuwa rafikie aitwaye, Samira, huku ikielezwa kuwa aliondoka kwao KIgamboni ili kwenda kwenye mazoezi ya bendi ya Twanga Pepeta ambapo hata hivyo uongozi wa bendi hiyo umekana msanii wao huyo wa zamani kuwahi kwenda kufanya mazoezi kwao.
Awali mazishi hayo yalipangwa kufanyika leo nyumbani kwa wazazi ao, Kigaamboni.

Prof Tibaijuka agomaa kujiuzulu, adai hata JK atamshangaa akifanya hivyo

http://www.fullshangweblog.com/wp-content/uploads/2014/06/DSC_0019.jpg
Prof Tibaijuka
TOFAUTI na matarajio ya wengi kwamba huenda angefuata nyayo za Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema aliyetangaza kubwaga manyanga kwa hiari yake, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka amegoma kujiuzulu kwa kudai haoni sababu ya kufanya hivyo
Akziungumza mapema leo jijini Dar es Salaam, Waziri huyo alisema watu wanaona kujiuzulu ni 'fasheni' ila kwake hayupo kwenye mkumbo huo na wala hana mpango huo kabisa.
"Nikijiuzulu hata Rais atanishangaa maana katika yale mapendekezo ya Bunge hakuna sehemu iliyonitaka kujiuzulu" alisema Prof Tibaigana.
Prof Tibaijuka, alisema kilichomfanya akutane na waandishi wa habari ni kuzungumzia yale aliyokosa nafasi ya kutolea ufafanuzi juu ya tuhuma zinazomkabili katika sakata la uchotwaji wa fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow.