STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, May 17, 2015

Wababe wa Yanga walala kwa waarabu wenzao

https://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2015/04/Etoile-du-Sahel-e1428316403743.jpg
Kikosi cha Etoile du sahel
http://www.eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/yanga%20sc%20vs%20etoile%20du%20sahel%201-1.JPG?itok=ajAcQ122
Walipoumana na Yanga jijini Dar na kutoka sare ya 1-1
WABABE wa Yanga katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka huu Etoile du Sahel ya Tunisia imekiona chamoto baada ya kutunguliwa mabao 2-0 na Raja Casablanca ya Morocco katika mchezo wa kwanza wa mtoano wa 16 Bora uliochezwa jana.
Etoile waliing'oa Yanga kwenye raundi ya pili kwa jumla ya mabao 2-1 ilikutana na kipigo hicho ugenini kupitia mabao ya kipindi cha kwanza.
Mabao hayo yaliwekwa kimiani na El Ouadi katika dakika ya 22 na Osaguona sekunde chache kabla ya mapumziko na kuwapa nafasi kubwa Wamorocco kunusa hatua ya makundi.
Hata hivyo Etoile bado wana nafasi ya kubadilisha matokeo watakaporudiana na wapinzani wao hao Juni 5 mjini Sousse, Tunisia.
Katika mechi nyingine za mtoano, Sfaxien ya Tuniais iliichapa ASEC Mimosas ya Ivory Coast kwa mabao 2-0, Stade Malien ikiwa nyumbani nchini Mali iliichjpa AS Vita ya DR Congo, Kaloum Star ya Guinea ilitandikwa nyumbani na Orlando Pirates ya Afrika Kusini Ijumaa kwa mabao 2-0.
Mechi nyingine ya mchujo huo  zinachezwa jioni hii kwa timu ya Sanga Balende (DRC) kuvaana na   Zamalek ya Misri,  AC Leopard ya Kongo kuikaribisha Warri Stars ya Nigeria, watetezi Al Ahly ya Misri itavaana na Club Africans ya Tunisia na Esperance ya Tunisia kuialika Heart of Oak ya Ghana.

Hii ndiyo ratiba ya COSAFA 2015

Stars wanaoanza kazi yao kesho Cosafa
RATIBA KAMILI COSAFA 2015
Mei 17, 2015
Namibia v Shelisheli (Saa 9:00 Alasiri, Uwanja wa Moruleng) 
Zimbabwe v Mauritius (Saa 11:30 jioni Uwanja wa Moruleng) 
Mei 18, 2015
Lesotho v  Madagascar (Saa 11:30 jioni Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace)
Tanzania v Swaziland (Saa 1:30 usiku Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace)
Mei 19, 2015
Shelisheli v Zimbabwe (Saa 11:00 jioni Uwanja wa Moruleng) 
Namibia v Mauritius (Saa 1:30 usiku Uwanja wa Moruleng) 
Mei 20, 2015
Madagascar v Tanzania (Saa 11:00 jioni Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace)
Lesotho v Swaziland (Saa 1:30, usiku Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace)
Mei 21, 2015
Namibia v  Zimbabwe (Saa 11:00 jioni Uwanja wa Moruleng) 
Shelisheli v  Mauritius (Saa 11:00 jioni Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace)
Mei 22, 2015
Lesotho  v Tanzania (Saa 11:00 jioni Uwanja wa Moruleng)
Madagascar v Swaziland (Saa 11:00 jioni Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace) 
ROBO FAINALI
Mei 24, 2015
Ghana v Mshindi Kundi B (Saa 9:00 Alasiri Uwanja wa Moruleng)
Msumbiji v Malawi (Saa 11:30 Uwanja wa Moruleng) 
Mei 25, 2015
Zambia v Mshindi Kundi A (Saa 11:30 Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace)
Afrika Kusini v Botswana (Saa 1:30 usiku Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace)
NUSU FAINALI ZA VIBONDE
Mei 27, 2015
Saa 11:00 jioni Uwanja wa Moruleng
Saa 1:30 usiku Uwanja wa Moruleng
FAINALI YA VIBONDE
Mei 29, 2015
Saa 11:00 jioni Uwanja wa Royal Bafokeng Sports Palace
NUSU FAINALI
Mei 28, 2015
Saa 11:00 jioni Uwanja wa Moruleng 
Saa 1:30 usiku Uwanja wa Moruleng 
MSHINDI WA TATU
Mei 30, 2015
Saa 9:00 Alasiri Uwanja wa Moruleng 
FAINALI
Saa 11:30 jioni Uwanja wa Moruleng

Bale kuwaondoa RVP, di Maria Manchester Utd

http://images.dailystar-uk.co.uk/dynamic/58/photos/872000/83872.jpg
Bale
http://www.indobolanews.com/wp-content/uploads/2014/12/vanpersiedimaria.jpg
RVP na di Maria watampisha Bale Old Trafford?
KLABU ya Manchester United inaweza kuwaacha Robin van Persie na Angel Di Maria katika majira ya kiangazi ili waweze kuweka nafasi ya kumsajili Gareth Bale. 
United inajiandaa kuwaacha Mholanzi, RVP na Muargentina, Di Maria aliyesajiliwa kwa kitita kikubwa msimu uliopita, ili kupunguza malipo ya mshahara wa Pauni 500,000 wanaopata nyota hao na kuwawezesha kumudu gharama za kumleta Bale kutoka Real Madrid. 
Bale bado ameendelea kuwa katika mipango ya United katika usajili wa mwaka huu na inaaminika dili linaweza kukamilika na kumrejesha nyota huyo Ligi Kuu baada ya kukaa kwa kipindi cha miaka miwili Hispania. 
Kabla ya kutimkia La Liga, Bale alikuwa akikipiga Tottenham Hotspur na kujijengea jina kubwa.
Uhakika wa United kumsajili Bale unatarajiwa kuifanya timu hiyo kuwaacha Van Persie na Di Maria ambao wote kwa pamoja na wanakunja kitita cha paundi 250,000 kwa wiki.

Yathibitika Andre Ayew Pele anukia England

http://imguol.com/c/esporte/2014/06/21/ganes-andre-ayew-comemora-o-primeiro-gol-de-gana-contra-a-alemanha-o-jogo-terminou-empatado-por-0-a-0-1403384138218_1920x1080.jpgRAIS wa klabu ya Marseille, Vincent Labrune amedai kuwa kuna uwezekano mkubwa wa Andre Ayew kutimkia katika Ligi Kuu ya England majira ya kiangazi. 
Mkataba wa Ayew, nyota wa kimataifa wa Ghana katika klabu hiyo unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na winga huyo ameweka wazi kuwa anataka kuondoka katika timu hiyo mwishoni mwa msimu huu. 
Ayew mwenye umri wa miaka 25 aligoma kuweka saini ya mkataba mpya jambo ambalo lilizivuta klabu kadhaa kubwa barani Ulaya zikiwemo Manchester United, Arsenal na Liverpool. 
Akihojiwa Labrune amesema pamoja na umuhimu wa Ayew katika kikosi chao, ila hawataweza kumbakisha kwasababu hawawezi kumpa ya fedha kama za klabu za Ligi Kuu ya England. 
Labrune aliendelea kudai mfumo wa kifedha nchini Ufaransa ni tofauti, hivyo hawawezi kumpa fedha kama ambazo ataweza kuzipata akienda England.

Makocha 6 wawania kumrithi Goran Kopunovic Simba

http://api.ning.com/files/DIpsX3jcHzOqy3VcUw5ZNppL02DCzZoEx*Df7GwMEgLxpCoWNJYyC0meL49I8FJvuDZ0zvvBXlopTmmFTwnzFk4I7Jvt1nM-/DSC03519.jpg
Kocha Goran Kopunovic aliyepewa mkono wa Kwaheri Msimbazi
http://4.bp.blogspot.com/-pdnqIqEf_Aw/T_EyQgwSnbI/AAAAAAAAIsM/kTNXOiY_-ZA/s1600/MILOVAN+CIRKOVIC.jpg
Milovan anayetarajiwa kurudi Msimbazi

http://www.ghanasoccernet.com/wp-content/uploads/2014/04/Piet.jpg
Kocha Piet de Mol wa Ubelgiji anayetajwa kuja kuchukua mikoba ya Goran ndani ya Simba
KLABU ya Soka imetangaza wazi kuachana na aliyekuwa kocha wao, Goran Kopunovic kutoka Serbia kutokana na kushindwa kuelewana naye juu ya dau alililotaka apewe katika mkataba wake mpya waliotarajiwa kuiingia baada ya kuiwezesha Simba kumaliza nafasi ya tatu katika Ligi Kuu.
Hata hivyo uongozi huo tayari umeanza mchakato wa kusaka kocha mkuu mpya na tayari makocha sita toka nchi za Ujerumani, Ufaransa, Bulgaria, Serbia, Ubelgiji na Croatia wametuma maombi yao na uongozi wa Simba utaanza mchakato wa kupitia wasifu wa makocha hao kabla ya kumchukua mmoja.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hanspope akiwa safari nje ya nchi aliiambia MICHARAZO kuwa, wameshindwana na Goran na sasa wanafanya taratibu za kumsaka kocha mpya ambaye atatangazwa mapema baada ya kupitiwa kwa wasifu wa makocha waliotuma maombi.
Hanspope alisema kuna orodha ya majina sita ya makocha toka barani Ulaya walioomba nafasi ya kumrithi Goran na utafanyika mchujo kabla ya kutoa jina moja la kubeba majukumu ya kuinoa Simba mpya kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
"Niko safarini, lakini taarifa nilizonazo ni kwamba tumeshindwana na Goran na tunasaka kocha mpya na tayari kuna majina sita yameshawasilisha maombi yao, kutoka nchi za Ubelgiji, Ufaransa, Serbia, Bulgaria na yatapitiwa wasifu wao na atakeyeenda na sifa ya klabu yetu tutamchukua," alisema Mwenyekiti huyo na kusisitiza kuwa ilikuwa ngumu kukubaliana na Goran juu ya masilahi.
"Goran alitaka masilahi makubwa ambayo klabu imeona isingeweza na tulimpa nafasi ya kujifikiria, lakini hata hivyo bado msimamo wake ulikuwa haujatulainisha kuafikiana naye, hivyo tumeachana naye na sasa tunaangalia mambo mengine," alisema.
Ingawa Hanspope alishindwa kutaja majina ya makocha hao walioomba kazi, lakini mmoja ya wanaotajwa kuwa na nafasi kubwa ya kumrithi Kopunovic ni Piet de Mol kutoka Ubelgiji ambaye ana rekodi na uzoefu wa soka la Afrika, huku Cirkovic Milovan akielezwa kuwa naye yu tayari kurudishwa katika kikosi hicho, huku akibebwa na rekodi zake kwa timu hiyo.
Juu ya usajili, zakaria Hanspope alisema ni mapema kwa sasa kwa sababu wanasubiri kwanza wapate kocha mpya ambaye atakuwa na mapendekezo yake, ingawa wameshaanza kuwasainisha wachezaji wao wa kikosi cha msimu ulioisha hivi karibuni.

STARS KUWAVAA SWAZILAND ROYAL BAFOKENG

https://thumbp22-ne1.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AK12imIAABVGVVdRVgrs4PR5j2U&midoffset=2_0_0_1_3717652&partid=8&f=1214&fid=Inbox&m=ThumbnailService&w=3000&h=3000
Wachezaji wa Taifa Stars wakijifua mazoezini tayari kuanza kazi katika michuano ya COSAFA
https://thumbp22-ne1.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AK12imIAABVGVVdRVgrs4PR5j2U&midoffset=2_0_0_1_3717652&partid=5&f=1214&fid=Inbox&m=ThumbnailService&w=3000&h=3000TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itacheza mchezo wake wa kwanza  wa kombe la COSAFA siku ya jumatatu dhidi ya Swaziland katika uwanja wa Royal Bafokeng pembeni kidogo ya jiji la Rustenburg kuanzia majira ya saa 1:30 jioni kwa saa za Afrika Kusini.

Awali michezo ya kundi B ilikuwa ifanyike katika uwanja wa Olympia Park, lakini waandaji wa michuano ya COSAFA Castle wamesema kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wao michezo hiyo imeshindikana kufanyika katika uwanja huo.

Uwanja wa Royal Bafokeng ni miongoni mwa viwanja viliyotumika katika Fainali za Kombe la Dunia 2010 chini Afrika kusini, ukiwa na uwezo wa kubeba watazamaji  42,000 huku timu ya Platinum Stars iliyopo Ligi Kuu ikiutumia kama uwanja wake wa nyumbani.

Leo asubuhi Taifa Stars imefanya mazoezi katika uwanja wa shule ya Rustenburg chini ya kocha mkuu Mart Nooij, na wachezaji wote wapo katika hali nzuri kuelekea katika mchezo huo wa jumatatu.
Kesho jioni Taifa Stars ifanya mazoezi saa jioni katika uwanja wa Rolay Bafokeng kwa ajili ya kuuzoea uwanja kabla ya mchezo wenyewe dhidi ya Swaziland.

Akiongelea hali ya hewa, kocha mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij amesema vijana wake wanaendelea kuizoea hali ya hewa, japokuwa kuna baridi hakuna mchezaji aliyeshindwa kufanya mazoezi kutokana na hali ya hewa.

Manchester Utd, Arsenal ni Ama Zao, Ama Zetu Englnad

http://i.ytimg.com/vi/IRZEf-r610s/maxresdefault.jpgLEO ndiyo Leo wakati wanaume 22 wa klabu za Manchester United na Arsenal watakapovaana katika pambano kali la Ligi Kuu ya England, huku kila timu ikihitaji ushindi ili angalau kujihakikisha nafasi ya pili ya msimamo wa ligi hiyo.
Pambano hilo litakalopigwa kwenye Uwanja wa Emirates limevuta hisia kali za mashabiki kutokana na ukweli timu zote zilipata matokeo tofauti katika mechi zao zilizopita. Arsenal inaifuata Mashetani Wekundu wakiuguza kichapo cha bao 1-0 walichopewa nyumbani na Swansea City wakati Mashetani hao wakichekelea ushindi wa ugenini dhidi ya Crystal Palace.
Arsenal waliopo nafasi ya tatu watahitaji ushindi huku wakiiombea mabaya waliokuwa mabibngwa watetezi manchjester Citrty watakaokuwa ugenini kuumana na Swansea kusudi warejeshe tumaini ya kukamata nafasi ya pili, nafasi kubwa kwa klabu hiyo kwa hivi karibuni kama wataipata mwisho wa msimu.
Mashetani wanaokamata nafasi ya nne nyuma ya Arsenal itakuwa ikihitaji ushindi ili kuipiku Wapiga Mitutu hao kwa tofauti ya pointi moja na kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kurejea kwenye namba za juu ambazo msimu uliopita walizisikia redioni.
Mechi ya leo inakumbushia Robo Fainali ya Kombe la FA lililochezwa mwezi Machi na Arsenal kuwatoa nishai wapinzani wao kwa mabao 2-1.
Ukiachana na pambano hilo la leo, matokeo ya mechi zilizochezwa wikiendi hii ni kama ifuatavyo;
 Liverpool ikiwa nyumbani ilikwanguliwa mabao 3-1 na Crystal Palace, huku
Southampton ikitafuna Aston Villa kwa mabao 6-1.
Matokeo ya mechi nyingine ni kama ilivyo hapo chini;
Burnley 0-0 Stoke
Queens Park Rangers 2-1 Newcastle United
Sunderland 0-0 Leicester City
Tottenham Spurs 2-0 Hull City
West Ham 1-2 Everton

Yanga kumburuza Kaswahili kwa kuwavuruga na Uchaguzi Mkuu

http://3.bp.blogspot.com/-EwbUOUfpjMs/VJl5rqLLBhI/AAAAAAAAZlQ/cfCofw5nm9Q/s1600/AAA.jpg

barua ya yanga kesi
UONGOZI wa klabu ya soka ya Yanga umepanga kumburuza kwenye Kamati ya Maadili kwa mwanachama wao aliyejitambulisha kama Katibu wa Kamati ya Uchaguzi, Francis Kaswahili, juu ya Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo kinyume na taratibu. Uongozi wa Yanga umesema kuwa Kaswahili siyo Katibu wa kamati hiyo kwani kamati aliyokuwa akiiongoza ilishavunjwa, pia, hakutumwa na Sekratarieti ya Yanga na hat uanachama wake una walakini kwani siyo hai kwa miaka mingi. taarifa rasmi ni hiyo inayosomeka hapo juu. Kaswahili alitangaza Yanga ingefanya Uchaguzi wake mkuu Julai 12 mwaka huu japo ambalo uongozi umeruka kimanga.