STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, May 17, 2015

Yathibitika Andre Ayew Pele anukia England

http://imguol.com/c/esporte/2014/06/21/ganes-andre-ayew-comemora-o-primeiro-gol-de-gana-contra-a-alemanha-o-jogo-terminou-empatado-por-0-a-0-1403384138218_1920x1080.jpgRAIS wa klabu ya Marseille, Vincent Labrune amedai kuwa kuna uwezekano mkubwa wa Andre Ayew kutimkia katika Ligi Kuu ya England majira ya kiangazi. 
Mkataba wa Ayew, nyota wa kimataifa wa Ghana katika klabu hiyo unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu na winga huyo ameweka wazi kuwa anataka kuondoka katika timu hiyo mwishoni mwa msimu huu. 
Ayew mwenye umri wa miaka 25 aligoma kuweka saini ya mkataba mpya jambo ambalo lilizivuta klabu kadhaa kubwa barani Ulaya zikiwemo Manchester United, Arsenal na Liverpool. 
Akihojiwa Labrune amesema pamoja na umuhimu wa Ayew katika kikosi chao, ila hawataweza kumbakisha kwasababu hawawezi kumpa ya fedha kama za klabu za Ligi Kuu ya England. 
Labrune aliendelea kudai mfumo wa kifedha nchini Ufaransa ni tofauti, hivyo hawawezi kumpa fedha kama ambazo ataweza kuzipata akienda England.

No comments:

Post a Comment