STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, May 17, 2015

Wababe wa Yanga walala kwa waarabu wenzao

https://hivisasa.co.tz/wp-content/uploads/2015/04/Etoile-du-Sahel-e1428316403743.jpg
Kikosi cha Etoile du sahel
http://www.eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/yanga%20sc%20vs%20etoile%20du%20sahel%201-1.JPG?itok=ajAcQ122
Walipoumana na Yanga jijini Dar na kutoka sare ya 1-1
WABABE wa Yanga katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka huu Etoile du Sahel ya Tunisia imekiona chamoto baada ya kutunguliwa mabao 2-0 na Raja Casablanca ya Morocco katika mchezo wa kwanza wa mtoano wa 16 Bora uliochezwa jana.
Etoile waliing'oa Yanga kwenye raundi ya pili kwa jumla ya mabao 2-1 ilikutana na kipigo hicho ugenini kupitia mabao ya kipindi cha kwanza.
Mabao hayo yaliwekwa kimiani na El Ouadi katika dakika ya 22 na Osaguona sekunde chache kabla ya mapumziko na kuwapa nafasi kubwa Wamorocco kunusa hatua ya makundi.
Hata hivyo Etoile bado wana nafasi ya kubadilisha matokeo watakaporudiana na wapinzani wao hao Juni 5 mjini Sousse, Tunisia.
Katika mechi nyingine za mtoano, Sfaxien ya Tuniais iliichapa ASEC Mimosas ya Ivory Coast kwa mabao 2-0, Stade Malien ikiwa nyumbani nchini Mali iliichjpa AS Vita ya DR Congo, Kaloum Star ya Guinea ilitandikwa nyumbani na Orlando Pirates ya Afrika Kusini Ijumaa kwa mabao 2-0.
Mechi nyingine ya mchujo huo  zinachezwa jioni hii kwa timu ya Sanga Balende (DRC) kuvaana na   Zamalek ya Misri,  AC Leopard ya Kongo kuikaribisha Warri Stars ya Nigeria, watetezi Al Ahly ya Misri itavaana na Club Africans ya Tunisia na Esperance ya Tunisia kuialika Heart of Oak ya Ghana.

No comments:

Post a Comment