STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, May 17, 2015

Bale kuwaondoa RVP, di Maria Manchester Utd

http://images.dailystar-uk.co.uk/dynamic/58/photos/872000/83872.jpg
Bale
http://www.indobolanews.com/wp-content/uploads/2014/12/vanpersiedimaria.jpg
RVP na di Maria watampisha Bale Old Trafford?
KLABU ya Manchester United inaweza kuwaacha Robin van Persie na Angel Di Maria katika majira ya kiangazi ili waweze kuweka nafasi ya kumsajili Gareth Bale. 
United inajiandaa kuwaacha Mholanzi, RVP na Muargentina, Di Maria aliyesajiliwa kwa kitita kikubwa msimu uliopita, ili kupunguza malipo ya mshahara wa Pauni 500,000 wanaopata nyota hao na kuwawezesha kumudu gharama za kumleta Bale kutoka Real Madrid. 
Bale bado ameendelea kuwa katika mipango ya United katika usajili wa mwaka huu na inaaminika dili linaweza kukamilika na kumrejesha nyota huyo Ligi Kuu baada ya kukaa kwa kipindi cha miaka miwili Hispania. 
Kabla ya kutimkia La Liga, Bale alikuwa akikipiga Tottenham Hotspur na kujijengea jina kubwa.
Uhakika wa United kumsajili Bale unatarajiwa kuifanya timu hiyo kuwaacha Van Persie na Di Maria ambao wote kwa pamoja na wanakunja kitita cha paundi 250,000 kwa wiki.

No comments:

Post a Comment