STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, May 17, 2015

STARS KUWAVAA SWAZILAND ROYAL BAFOKENG

https://thumbp22-ne1.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AK12imIAABVGVVdRVgrs4PR5j2U&midoffset=2_0_0_1_3717652&partid=8&f=1214&fid=Inbox&m=ThumbnailService&w=3000&h=3000
Wachezaji wa Taifa Stars wakijifua mazoezini tayari kuanza kazi katika michuano ya COSAFA
https://thumbp22-ne1.mail.yahoo.com/tn?sid=2126005954&mid=AK12imIAABVGVVdRVgrs4PR5j2U&midoffset=2_0_0_1_3717652&partid=5&f=1214&fid=Inbox&m=ThumbnailService&w=3000&h=3000TIMU ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itacheza mchezo wake wa kwanza  wa kombe la COSAFA siku ya jumatatu dhidi ya Swaziland katika uwanja wa Royal Bafokeng pembeni kidogo ya jiji la Rustenburg kuanzia majira ya saa 1:30 jioni kwa saa za Afrika Kusini.

Awali michezo ya kundi B ilikuwa ifanyike katika uwanja wa Olympia Park, lakini waandaji wa michuano ya COSAFA Castle wamesema kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wao michezo hiyo imeshindikana kufanyika katika uwanja huo.

Uwanja wa Royal Bafokeng ni miongoni mwa viwanja viliyotumika katika Fainali za Kombe la Dunia 2010 chini Afrika kusini, ukiwa na uwezo wa kubeba watazamaji  42,000 huku timu ya Platinum Stars iliyopo Ligi Kuu ikiutumia kama uwanja wake wa nyumbani.

Leo asubuhi Taifa Stars imefanya mazoezi katika uwanja wa shule ya Rustenburg chini ya kocha mkuu Mart Nooij, na wachezaji wote wapo katika hali nzuri kuelekea katika mchezo huo wa jumatatu.
Kesho jioni Taifa Stars ifanya mazoezi saa jioni katika uwanja wa Rolay Bafokeng kwa ajili ya kuuzoea uwanja kabla ya mchezo wenyewe dhidi ya Swaziland.

Akiongelea hali ya hewa, kocha mkuu wa Taifa Stars Mart Nooij amesema vijana wake wanaendelea kuizoea hali ya hewa, japokuwa kuna baridi hakuna mchezaji aliyeshindwa kufanya mazoezi kutokana na hali ya hewa.

No comments:

Post a Comment